Tuesday, October 27, 2020

VENUS VS SERENA WILLIAMS: FAINALI ILIYOTAWALIWA NA HISIA, REKODI

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MELBOURNE, Australia

USHINDI wa seti 6-4, 6-4 alioupata Serena Williams dhidi ya dada yake Venus katika fainali ya kuwania taji la michuano ya wazi ya tenisi ya Australian (Australian Open) wikiendi iliyopita, ulitokana na namna ambavyo mkali huyo wa Marekani alivyojitahidi kuzizuia hisia zake kwenye mtanange huo uliokuwa na upinzani wa hali ya juu baina ya ndugu hao wawili.

Serena alifanikiwa kuweka rekodi kwa kutwaa taji lake la 23, baada ya kuishinda nguvu ya hisia ya kuchuana na ndugu yake wa damu ambapo alipambana na kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo huo ulioshuhudiwa na maelfu ya mashabiki waliohudhuria kwenye dimba la Rod Laver, Melbourne, Australia.

Aidha, hilo lilikuwa ni taji la saba la Australian Open kwa Serena, huku pia akifanikiwa kupanda hadi nafasi ya kwanza kwa mataji mengi juu ya Steffi Graf na sasa anategemea kuchukua taji jingine ili avunje rekodi ya muda mrefu ya Margaret Court ya kutwaa mataji 24.

Kama hiyo haitoshi, Serena alirudi kwenye nafasi yake ya kwanza kwenye viwango vya ubora akimshusha mwanadada Angelique Kerber, aliyeikalia nafasi hiyo baada ya kunyakua taji la U.S. Open mwaka jana.

Kwa upande wa Venus, yeye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mzee kucheza fainali akiwa na umri wa miaka 36 huku mdogo wake ambaye wamepishana mwaka mmoja (akiwa na umri wa miaka 35). Kwa miaka yao hiyo, kawaida ya wacheza tenisi huwa ndio muda wa kufurahia maisha nje ya uwanja lakini bado wanadada hao walionesha kuwa bado wapo imara mchezoni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -