Tuesday, October 27, 2020

VICHWA VINAVYOTARAJIWA KUWASHA MOTO RBA 2017

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SHARIFA MMASI

PILIKAPILIKA za maandalizi ya Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), zinaendelea huku kila timu ikijiimarisha kuanza mtanange wa michuano hiyo Januari 28 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini.

Kila kocha amekuwa akifanya maandalizi kwa timu yake kunoa wachezaji wake kwa siri na hadi sasa bado imekuwa siri kubwa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kwani hakuna timu iliyoanika kikosi chake hadharani.

Wakati hayo yakiendelea, kuna wachezaji mahiri ambao wanatabiriwa kuwasha moto kwenye mashindano hayo msimu huu. Wachezaji hao wanatarajiwa kuleta chachu na kuongeza hamasa ya ushindani kwa timu wanazozitumikia.

Muhammed Mchenga

Kwa wadau wa mpira wa kikapu, Dar es Salaam, hakuna asiyemjua mchezeshaji huyu mahiri anayechezea nafasi ya juu (Point Gard) mwenye umbo la kati na urefu wa futi tano na nchi 10, anakipiga katika timu ya Savio ambayo ameisaidia vilivyo timu hiyo kunyakua taji la ubingwa katika michuano ya Taifa (NBL) na ile ya RBA msimu wa mwaka 2015/2016.

Savio walipoiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya  Kanda ya Tano (Zone 5) mwaka 2015 kule jijini Kigali nchini Rwanda, Mchenga alikuwa nguzo imara kwani aliwadhibiti vilivyo washambuliaji wa timu mbalimbali zilizoshiriki ikiwemo ile ya Uganda, Kenya, Rwanda na nyinginezo, ingawaje walitupwa nje ya michuano hiyo.

Kutokana na uwezo wake mkubwa alionao, wachezaji mbalimbali wa timu za hapa nyumbani hususani zile zinazotarajiwa kushiriki Ligi ya RBA, wanakazi ya ziada kummiliki nyota huyo, ili waweze kushinda.

Evans Mwaseba

Amekuwa kwenye ubora wake kila awapo uwanjani na kuwafanya mashabiki kuona Taifa lao lina kiungo mahiri, kwani amekuwa akicheza kwa jitihada kubwa kujitangaza kwenye soko la michezo hususani kikapu ndani na nje ya nchi.

Mwaseba anaweza kutofautishwa na baadhi ya wachezaji nyota wanaoendelea kung’aa hapa nchini, kutokana na uwezo wake wa kushambulia timu pinzani, kufunga bila kubahatisha, kumiliki mpira wenye manufaa kwa timu yake, lakini pia linapokuja suala la mitupo huru (Free Through) ni fundi wa kuwatungua wapinzani wake vikapu vya kutosha.

Achana na hayo, Mwaseba anaposimama kwenye eneo la timu pinzani akiwa uwanjani, huwa hacheki na mtu badala yake lazima afunge, kitu ambacho kimekuwa kikiwaogopesha baadhi ya wachezaji nyota  wa timu pinzani hususani zile zinazoshiriki RBA.

Kwa sasa Mwaseba anaendelea kujifua asubuhi na jioni akiwa chini ya kocha wake Edward Bezuidenhout, tafsiri ya maandalizi hayo ni kuzitaka timu pinzani kujiandaa kupokea kichapo kutoka kwake na klabu kwa ujumla.

Maria Mabella

Ni kijana mwenye umri wa miaka (24), anayekipiga katika klabu ya wanawake ya Donbosco Lioness, inayoshiriki ligi mbalimbali za hapa nyumbani ikiwemo hiyo ya RBA, inayonukia kila kona ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza kiwango chake kilionekana akiwa Shule ya Sekondari ya Air Wing iliyopo maeneo ya Banana jijini Dar es Salaam, ambapo uongozi wa Donbosco Lioness, ukishirikiana na wazazi wa mchezaji huyo, ulikubaliana kumjumuisha katika kikosi cha timu anayoendelea kuitumikia hadi sasa.

Hakuna shaka, Maria anajua wazi timu yake inahitaji kuchukua ubingwa msimu ujao wa 2017, kufuta machungu ya kupoteza taji lao mwaka jana lililong’ang’aniwa na Vijana Queens.

Kwa namna yoyote ile na kwa kiwango alichonacho mchezaji huyu, bila shaka amejipanga imara kukabiliana na vita kali dhidi ya wapinzani kurudisha heshima ya timu yake.

Asha Chenge

Mashabiki wa mpira wa kikapu hapa nchini  wanajua shughuli ya mwanadada huyu ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Jeshi ya JKT mabingwa wa RBA mwaka 2014/15, kabla ya Savio kuwapora taji hilo wanaloendelea kulimiliki hadi hivi sasa.

Washambuliaji wa timu pinzani wanajua fika kwamba, Asha si aina ya wachezaji wakumwendea ovyo ovyo kutokana na staili zake anazotumia akiwa uwanjani na timu pinzani na kama huamini waulize wadau mbalimbali wa kikapu hapa nchini,  shughuli yake wanaitambua.

Mahfudh Simba

Kiwango cha mchezaji huyo wa klabu ya Donbosco Young Stars, kinaimarika kila kukicha na kocha wake hakuona ajabu kuwaweka benchi wakali kibao na kumuunganisha yeye katika kile kikosi cha timu ya Savio kilichokwenda Rwanda mwaka juzi, kuiwakilisha nchi katika michuano ya Zone 5 kule jijini Kigali.

Uwezo wake ndio unaoendelea kuzifanya  baadhi ya timu kubwa hapa nchini, kufukuzia saini yake ili kumng’oa Young Stars kwani ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuzidi kuuwasha moto wa Ligi ya RBA hivi karibuni tayari kwa kuipatia ubingwa klabu yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -