Monday, October 26, 2020

Vigogo TFF waburuzwa kortini

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA KULWA MZEE

ALIYEKUWA Msaidizi Binafsi wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Juma Matandika na Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo, Martin Chacha, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh milioni 25.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alidai washtakiwa walitenda makosa hayo Februari 4 mwaka huu.

“Mheshimiwa Hakimu mshtakiwa wa kwanza, Matandika na Chacha, wanashtakiwa kwa kosa moja la kuomba rushwa kinyume cha sheria ya kuzuia rushwa.

“Washtakiwa mnadaiwa Februali 4 mwaka huu, Makao Makuu ya TFF mkiwa waajiriwa wa TFF mlishawishi kuomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Salum Kulunge na Constantine Morandi.

“Kulunge na Morandi ni maofisa kutoka Chama cha Soka Mkoa wa Geita na klabu ya mpira wa miguu, Geita.

“Washtakiwa mliwaomba rushwa kama kishawishi kwa TFF na Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa uamuzi dhidi ya klabu ya mpira wa miguu Polisi Tabora ili kuisaidia klabu ya Geita kupanda katika Ligi Kuu Tanzania,” alidai Swai.

Baada ya kusomewa mashtaka, washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi umekamilika.

Swai aliomba kesi ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hata hivyo, Mahakama ilikubali kuwapa dhamana washtakiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, wenye barua na vitambulisho watakaosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano kila mmoja.

Washtakiwa wametimiza masharti ya dhamana wako nje hadi Novemba 30 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -