Sunday, October 25, 2020

MAKONDA ANAWAPENDA ZAIDI WASANII WETU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HASSAN DAUDI

KWA miaka mingi sasa vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya imekuwa ikiendelea hapa nchini bila kuwapo kwa dalili zozote za kuitokomeza.

Mbaya zaidi ni kwamba, vijana ambao wanatajwa kuwa taifa la kesho ndiyo waathirika wakubwa wa dawa hizo.

Imeelezwa kuwa kati ya vijana 20 wa Jiji la Dar es Salaam, nane wanatumia dawa hizo, ikiwamo bangi ambazo kwao zimegeuka kuwa starehe licha ya madhara makubwa wanayoyapata. Je, kwa takwimu hizo, Taifa limekuwa likipoteza vijana wangapi kwa mwaka?

Cha kusikitisha ni kwamba, takwimu zinaonesha idadi kubwa huanza kutumia mihadarati wakiwa na umri wa miaka 18 au chini ya hapo, huku wengi wao wakiwa wanatokea katika familia masikini.

Kwa kiasi kikubwa vitendo vya rushwa vimekuwa vikitajwa kuchangia kudhoofisha mapambano dhidi ya utumizi na usambazaji wa dawa hizo.

Kuna madai kuwa viongozi wa ngazi za juu serikalini au wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakilitumia Jeshi la Polisi kuhakikisha mkono wa sheria hauwafikii na kuharibu masilahi yao katika biashara hiyo ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ni mfano mzuri wa viongozi ambao wameanza kuonesha kwa vitendo chuki zao dhidi ya dawa hizo.

Habari iliyoteka vichwa vya habari hapa nchini katika siku za hivi karibuni, ni ile iliyomhusu ambapo aliwataja watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya na kutaka kukutana nao Kituo Kikuu cha Kati cha Jeshi la Polisi (Central).

Mbali na watumishi wa Jeshi la Polisi, idadi kubwa ya wale walioibuliwa na Makonda ni wasanii wa muziki na wenzao wa tasnia ya uigizaji.

Miongoni mwa mastaa hao ni Khalid Mohamed, ‘TID’, Wema Sepetu, Rashidi Makwiro ‘Chidy Benz’ na wengineo.

“Najua siku moja Mungu ataniuliza, nilipokupa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Rais wako, watoto waliangamia kwa dawa za kulevya, sitaki kufika mbinguni nisiwe na jibu. Nataka niwe na jibu kwa Mungu kuwa dawa za kulevya hazikubaliki ndani ya Jiji la Dar es Salaam,” alisema Makonda katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Kwa kweli Makonda anastahili pongezi kwani viongozi wengi wameshindwa kuwa na ujasiri alionao, kuingia kwenye vita dhidi ya wahusika wa dawa hizo haramu.

Ni wazi kuwa mheshimiwa huyo ameonesha nia ya dhati ya kujitolea uhai wake kwa maisha ya vijana wenzake ambao ndiyo wahanga wakubwa.

Kwa alichokifanya, hakuna ubishi kuwa amethibitisha kiu ya kuutokomeza mtandao wa biashara ya ‘unga’ jijini Dar.

Lakini pia, kiongozi huyo ameonyesha jinsi anavyowapenda wasanii wetu kwa kufahamu wengi wamekuwa wakipoteza uwezo wao wa iwe ni kuimba au kuigiza kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa hizo za kulevya.

Hata hivyo, tayari kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa kampeni hiyo ya mheshimiwa Makonda katika kuangamiza biashara hiyo.

Inasikitisha kusikia wapo wanaosema Makonda anatafuta ‘kiki’ ya kisiasa kupitia operesheni hiyo. Ni kweli umaarufu na uwajibikaji wa Makonda ulihitaji kiki ya namna hiyo? Sidhani.

Naamini kuwa tabia yake ya uwajibikaji ndiyo iliyomfanya akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kupata wadhifa alionao hivi sasa.

Nafikiri ifike kipindi tuache soga za kisiasa katika masuala yenye tija kwenye ustawi wa jamii.

Tatizo nililoligundua ni kwamba, kumekuwa na utamaduni wa kuruhusu mawazo hasi kukinzana na mambo ya msingi.

Hata suala hili nyeti la nguvu kazi ya Taifa kupotea vijiweni kwa dawa za kulevya linawekewa mitazamo ya kisiasa?

Binafsi, kwa hali ilivyo sasa ambapo dawa hizo zimewafanya vijana wengi kuwa waokota makopo na kurukwa na akili, sikutegemea kuona juhudi za Makonda zikidhalilishwa kupitia mitandao ya kijamii.

Makonda anapaswa kuonekana ‘malaika’ hasa kwa kauli yake ya kuwa amejitolea kufukuzwa kazi na hata kuuawa lakini si kuendelea kucheka na watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya.

Simaanishi kuwa viongozi waliomtangulia katika mkoa huu wa Dar hawakuwa na nia ya dhati ya kukomesha dawa za kulevya, lakini nafikiri Makonda amekwenda mbali zaidi kwa kutaka kukutana na wahusika.

Ni kwa namna gani mapambano hayo ya Makonda dhidi ya uhalifu huu yatafanikiwa ikiwa hatapata ushirikiano kutoka kwa jamii ambayo ndiyo chimbuko la ‘mateja’?

Watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya hawatoki nje ya mazingira tunamoishi, ni kaka, dada, wajomba, marafiki na majirani zetu.

Aliowataja Makonda ni sehemu ndogo tu ya mateja tulionao mitaani. Ni ngumu kwa mkuu huyo wa mkoa kumfikia kila mtumiaji na muuzaji wa dawa hizo ikiwa jamii haitampa ushirikiano kwa kutoa taarifa za kuwafichua.

Makonda ameanzisha lakini mapambano haya dhidi ya dawa za kulevya ni mali ya jamii nzima na hayatofanikiwa ikiwa tutamsusia. Hongera Makonda, Mungu anakusimamia katika hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -