Wednesday, October 28, 2020

VITA YA KIATU CHA DHAHABU WAZAWA, WAGENI NI MWENDO KUKABANA KOO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

SWALI ambalo wadau wengi wa soka wanajiuliza kwa sasa ni hili, nani atatwaa tuzo ya ufungaji bora ‘kiatu cha dhahabu’ msimu huu wa Ligi Kuu Bara itanyakuliwa na mzawa au nyota wa kigeni wataendeleza ubabe?

Ni swali linalotokana na ushindani wa hali ya juu uliopo kwa sasa miongoni mwa wachezaji wazawa na wale wa kigeni katika upachikaji mabao.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Agosti 20, tayari mechi 12 zimekwishacheza huku chache tu zikiwa  zina michezo 11.

Kupitia michezo hiyo, tumeshuhudia juhudi kubwa zikifanywa na wachezaji wa timu mbalimbali hususani katika kufunga mabao ambayo huzisaidia  kuibuka na ushindi.

BINGWA linakuletea orodha ya wachezaji ambao msimu huu wameonyesha nia ya dhati ya kutaka tuzo ya ufungaji bora ambayo msimu uliopita ilitwaliwa na straika Mrundi wa Yanga, Amis Tambwe aliyefunga mabao 21.

Tuzo hiyo ni ya pili kutwaa kwa Tambwe baada ya awali kuitwaa akiwa Simba msimu wa  2013/14 alipofunga mabao 19.

 

Shiza Kichuya

Kwa mara ya kwanza winga huyu machachari aliyesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar ameingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya ufungaji, ambapo mpaka sasa amefunga mabao saba kati ya 21 yaliyofungwa na timu yake.

Staa huyu mpya mzawa anaonekana kuwa tishio kwenye nyavu za wapinzani kiasi kwamba imefikia wakati mabeki wa timu pinzani wamekuwa wakimkamia kwa lengo la kumkata makali.

 

Amis Tambwe

Mrundi huyu mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao ya kichwa mpaka sasa amefanikiwa kuifungia Yanga mabao sita kati ya 24 iliyofunga timu yake.

Licha ya kuwa ligi bado mbichi, Tambwe anapewa nafasi kubwa ya kuibuka kwa mara nyingine mfungaji bora msimu huu.

Tambwe anapewa nafasi hiyo kutokana na ukweli kwamba ni mshambuliaji mwenye uchu wa kufumania nyavu na tayari ameonyesha nia ya kuhitaji heshima hiyo kwa mara nyingine.

 

Rashid Mandawa

Amejiunga na Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Mwadui FC.

Straika huyu mzawa ameifungia Mtibwa mabao sita sawa na Tambwe.

Kama ataendelea na kasi yake hii si ajabu kama atanyakua tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Obrey Chirwa

Inadaiwa huyu ndiye mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa kuliko mchezaji mwingine yeyote katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

Aliianza ligi kwa kusuasua lakini sasa anaonekana kushika kasi kwani tayari amepachika mabao matano.

Kwa kasi hii ya Chirwa haitashangaza  kama raia huyu wa Zambia akafanya mambo ya kushangaza msimu huu kwa kutwaa tuzo ya ufungaji bora.

 

Omary Mponda

Licha ya kwamba hazungumziwi sana na mashabiki wa soka lakini ukweli  ni kwamba mshambuliji huyu wa Ndanda FC ni miongoni mwa wachezaji wazawa walioonyesha nia ya dhati ya kuihitaji tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu msimu huu.

Katika michezo 12 ambayo Ndanda imekwishacheza mpaka sasa amefanikiwa kucheka na nyavu mara 10.

 

Simon Msuva

Kama ilivyokuwa kwa mwenzake Chirwa ndiyo ilivyokuwa kwa Msuva ambaye naye hakuuanza msimu vizuri.

Lakini sasa upepo unaonekana kuanza kumwendea vizuri Msuva ambaye amefunga mabao matano mpaka sasa huku akionekana kucheza kwa kiwango cha juu.

Msuva ana uzoefu na heshima ya kuwa mfungaji  bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kufanikiwa kufanya hivyo msimu wa 2014/15, ambapo alifunga mabao 17.

Sababu hizo zinatosha kumwingiza moja kwa moja kwenye vita hii ya kusaka tuzo yau fungaji bora.

 

Donald Ngoma

Msimu uliopita alimaliza msimu akiwa amefunga mabao 17 na kumfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji waliofanya vizuri licha ya kwamba heshima hiyo ilikwenda kwa Tambwe aliyefunga mabao 21.

Kutokana na uzoefu alionao straika huyu katika Ligi Kuu Bara anapewa nafasi ya kutwaa tuzo ya ufungaji.

Mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao manne kati ya 24 ambayo Yanga imejikusanyia kutupia mechi zake 12.

 

John Bocco

Aliwahi kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2011/12 baada ya kufunga mabao 19.

Baada ya hapo amekuwa akiingia mara kwa mara kwenye kinyang’anyiro hicho lakini mwisho wa siku amekua akiambulia patupu.

Katika michezo 11 iliyocheza timu yake ya Azam mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao manne.

 

Laudit Mavugo

Licha ya hivi sasa kuonekana hayupo kwenye ubora uliotarajiwa na wengi, lakini mshambuliaji huyu wa Simba kutoka Burundi bado huwezi kumtenga na orodha ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya ufungaji bora msimu huu.

Straika huyu aliyetua Simba msimu huu akitokea Vita O’ ya kwao Burundi,  mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao manne kati ya 21 waliyopachika Wekundu hao.

Msimu uliopita alifanikiwa kuifungia Vital O’ mabao 32 yaliyomfanya aibuke mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Burundi.

Wachezaji wengine wanaopewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo msimu huu wakiwa na mabao matatu kila mmoja ni Ibrahim Ajibu (Simba), Deus Kaseke (Yanga), Hood Mayanja (African Lyon), Rapher Daud (Mbeya City), Haruna Chanongo (Mtibwa), Peter Mapunda (Majimaji) na Riphat Hamis (Ndanda).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -