Sunday, January 17, 2021

VITA YA KIBABE CAMEROON VS MISRI NI PATASHIKA NGUO…

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LIBREVILLE, Gabon

JUZI usiku mashabiki wa kandanda walikuwa bize kufuatilia kile kilichokuwa kikiendelea kwenye Uwanja wa Stade de Franceville.

Cameroon walikuwa dimbani hapo kumenyana na Ghana ukiwa ni mchezo wa nusu fainali za mwaka huu za Afcon (Afcon 2017).

Katika mtanange huo, Cameroon waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kukata tiketi ya kucheza fainali dhidi ya wababe wa Kaskazini mwa Afrika, Misri.

Mabao yaliyowapa ushindi Cameroon yaliwekwa kimiani na Michael Ngadeu-Ngadjui kabla ya Christian Bassogog kugongelea msumari wa mwisho kwenye kaburi la Ghana.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopo sasa, mchezo wa fainali kati ya Cameroon na Misri utachezwa kesho Februari 5 kwenye Uwanja wa Stade d’Angondje.

Kwa upande wake, kocha wa Cameroon, Hugo Broos, amefurahia ushindi huo ingawa amekiri kikosi chake kina kibarua kizito dhidi ya Misri katika mchezo wa fainali.

“Ni kama ndoto iliyotimia kwa sisi kufika fainali,” alisema Mbelgiji huyo na kukiri kuwa mtanange dhidi ya Mafarao utakuwa wa kukata na shoka.

“Hii timu ya vijana imeonesha kitu cha kipekee hasa baada ya kufika robo fainali,  wameshapata uzoefu kidogo,” alisema kocha Broos ambaye aliwahi kuichezea timu ya taifa ya ubelgiji.

“Nilipokuja Cameroon (Februari mwaka huu), nilikuta kikosi chenye wachezaji wazee. Tulikuwa na asilimia 30 ya wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30. Huwezi kutengeneza timu ya baadaye kwa mtindo huo,” aliongeza Broos.

Kikosi cha Misri kinachonolewa na kocha raia wa Argentina, Hector Cuper, kilitinga fainali baada ya kuwatandika Burkina Faso kwa penalti 4-3.

Shukrani pekee zimwendee mlinda mlango mkongwe, Essam El Hadary, ambaye aliokoa penalti mbili.

Mchezo huo ulilazimika kufikia hatua hiyo ya changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kwa upande wake, Cuper alisema kikosi chake kilikuwa na bahati kwa kutinga fainali mbele ya Burkina Faso, lakini anamini mambo yatakuwa magumu zaidi dhidi ya Cameroon ingawa lengo lao ni kushinda mchezo huo.

“Tangu mwanzo tulijua kabisa kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Burkina Faso ni timu yenye kasi mno. Walikuwa bora kuliko sisi,” alisema Cuper.

“Tumefurahi kufika fainali. Tutajaribu kurudi kivingine kwa ajili ya mchezo ujao (dhidi ya Cameroon).”

Kesho itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana kwenye mashindano ya Afcon tangu mwaka 2010, ambapo Misri walishinda mabao 3-1.

Katika hatua ya fainali ya michuano hiyo, timu hizo zimekutana mara mbili (1986, 2008) na kwa bahati mbaya Misri alishinda zote.

Walipotoana jasho mwaka 2012 ulikuwa ni mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na Misri walishinda mabao 2-1.

Kabla ya mtanange wa kesho, rekodi zinaonesha kuwa wakali hao wameshavaana mara 26.

Katika idadi hiyo, Misri ndiye anayeonekana kuwa mbabe kwani wameshinda mara 15.

Kwa upande wao, Cameroon wameibuka kidedea katika mitanange mitano na mechi zilizobaki ziliamuliwa kwa matokeo ya suluhu.

Mechi ambayo Cameroon walipokea kipigo cha aibu ni ile ya kirafiki iliyochezwa Mei 29, 1983, baada ya  kupewa kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Mafarao hao.

Ushindi mnono pekee ambao Cameroon imewahi kuupata kwa Misri, ni ule wa mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Februari 1983 kwenye Uwanja wa Stade Omnisports Ahmadou Ahidjo uliopo jijini Yaounde.

Mpaka sasa, kikosi cha Misri kimeruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja lakini Cameroon wamefanya hivyo mara nne.

Ikumbukwe kuwa Cameroon hawajachukua taji la michuano mikubwa tangu mwaka 2007, lakini wana historia ya kuwa timu pekee barani Afrika kushiriki mara nyingi fainali za Komvbe la Dunia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -