Friday, October 23, 2020

VITA YA SELINE NA THE INDUSTRY

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Na JOHANES RESPISHIUS,

MIONGONI mwa stori zinazobamba kwa sasa katika mitandao ya kijamii, hususan Instagram ni kuhusiana na ugomvi uliopo kati ya msanii chipukizi aliyekuwa chini ya lebo ya The Industry inayomilikiwa na wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale ‘Aika’ na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’, Roseline Muhagachi, maarufu kama Seline na uongozi wake huo.

Juzi kati BINGWA lilipiga stori na Seline, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Dollar, ambapo alifunguka mambo mengi kuhusiana na kile kinachoitwa ‘bifu’ kati yake na uongozi, The Industry.

Bingwa: Seline nini hasa kimekufanya ukajiondoa The Industry?

Seline: Nilijitoa mwenyewe The Industry, hakuna aliyenitoa, kwanza nilikwenda pale kama mteja, wakataka kunisaini kwenye lebo, nikakubali, lakini nilikuwa najilipia kila kitu kuanzia ‘production hadi promotion’.

Baada ya kuona nauliza maendeleo ya muziki wangu mbona nyimbo haifiki sehemu wakawa hawanipi jibu sahihi, wakawa wanasema kwamba nina haraka, jambo ambalo si kweli na ilikuwa haki yangu, kwani kama mtu umeweka fedha kwenye biashara lazima ujue maendeleo yake kila wakati.

Kutokana na hali hiyo ilifika hatua ya Aika kufuta wimbo wangu wa ‘Njoo’ kwenye mtandao wa Youtube ili usiendelee kuangaliwa. Nilipoona mambo hayo nikasema haina haja ya kuendelea, nikajivua mkataba na kujitoa.

Bingwa: Inakuwaje msanii yupo chini ya lebo halafu gharama anajilipia mwenyewe?

Seline: Najua kuwa ukiwa chini ya lebo unagharimiwa kila kitu, iwe kwenye kurekodi au kushuti, lakini niliambiwa nisiseme kama najilipia mwenyewe ili watu wasijekunipotezea, kwani nikisema wao wameshajulikana sana nitapata mashabiki wengi.

Kuhakikisha hilo, hata wimbo wangu wa ‘Njoo’ nililipa fedha kwa Nahreel ili anitengenezee audio, matengenezo ya video pamoja na promosheni  zilikuwa gharama zangu.

Bingwa: Kuna tetesi kwamba Aika amekufanyia ‘Mtimanyongo’ kwasababu alihofia unaweza kutoka na Nahreel?

Seline: Mmh! Hapana, hayo ni maneno ya watu tu ambao wanaamua kusema wanavyojisikia, lakini mimi sijawahi kuwa karibu sana na Nahreel nje ya kazi… siwezi kuwa katika mahusiano na Nahreel, namhesimu kama ‘mshikaji’ na kakaangu.

Bingwa: Labda wewe hukuwahi kuhisi hivyo?

Seline: No! Aika amenifanya hayo aliyoyafanya … labda ndio roho yake ilivyo, kwani sikuwa mtu wa kwanza kutoka, maana Star One haikuwezekana pia, hivyo hivyo kwa Chin Beez, kwa hiyo imekuwa historia yao kuwa na tofauti na wasanii wao.

Bingwa: Baada ya kuachana na uongozi wako, vipi utaendelea kuwa peke yako au lebo nyingine ambayo unatarajia kujiunga.

Seline: Kwa sasa nafanya kazi kivyangu, ila sina kinyongo na mtu, najua kama Mungu kaniandikia nitakuwa nani hakuna anayeweza kubadilisha na cha msingi ni kuwaomba mashabiki zangu waendelee kuzisapoti kazi zangu na wasiangalie nani kasema nini.

Baada ya kumsikia Selina, BINGWA mdogo mdogo likaamua kwenda kupata ufafanuzi kwa The Industry, ambapo Aika alifunguka mambo kadhaa kuhusiana na kilichotokea.

Bingwa: Kama mmoja wa wamiliki wa The Industry, unazungumziaje suala la msanii wenu, Selina kuamua  kujitoa kwenye lebo yenu?

Aika: The Industry imeanzishwa ikiwa na kanuni zake, kwa hiyo kama msanii inabidi ufuate kile ambacho uongozi unakuambia, ukikwambia fanya kitu fanya au subiri basi huna budi kusubiri, maana uongozi unajua unafanya nini.

Lakini yeye alitaka afanyiwe kile ambacho anakitaka kwa uharaka, ndiyo maana alikuwa anaamua kutumia fedha yake ili atoke haraka zaidi, jambo ambalo si zuri, kwa hiyo The Industry ilivyoshindwa kuendana naye ikabidi atoke aende na haraka zake.

Bingwa: Inakuwaje msanii yupo chini ya lebo halafu gharama akajilipia mwenyewe?

Aika: Ni kweli lebo ndiyo inatakiwa kubeba gharama zote za msanii wake, lakini si kwa muda anaoutaka yeye, kuna mpangilio wa kila kitu kinavyokwenda kwa muda husika, hivyo itakuwa vigumu kufanya kazi na mtu anayejiamulia peke yake na haheshimu maadili ya kampuni.

Pia The Industry tulikuwa na utaratibu kwamba tutawapa kipaumbele kikubwa wasichana wanaohitaji msaada zaidi na isitoshe Seline alikuja akiwa wa mwisho, lakini alikuwa anataka yeye atoke kabla ya wengine aliowakuta.

Kutokana na hali hiyo ya kutaka kufanikiwa haraka, ndiyo maana alikuwa anaamua kujilipia baadhi ya gharama ili awahi na alikuwa mtu wa kulalamika karibu asilimia 90 ya muda wake, ilikuwa ni kulalamika tu.

Bingwa: Baada ya Seline kuvunja mkataba labda kuna hatua yoyote ambayo mnatarajia kuzichukua dhidi yake?

Aika: Hatua za kuchukua zipo, lakini hatukupenda kuchukua hatua yoyote, tumemwacha aende zake kwa sababu hatuna muda wa kupoteza, kwa hiyo ikitokea chochote kuna penati ya kulipa na si msanii wa kwanza kufanya hivi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -