Monday, January 18, 2021

VITA YA ‘TOP FIVE’ NANI KULA KRISMASI KWA RAHA ZAKE?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

LICHA ya kuwa mapumziko ya majira ya baridi, lakini kipindi cha majira ya baridi kuwa na unafuu kwa baadhi ya timu za Ligi Kuu England, kipindi cha sikukuu za Krismasi bado ni muhimu kwao.

Umuhimu huo unatokana na kuwa ni kipindi ambacho kila timu huwa zinakabiliwa na majeruhi kutokana na kukutana na mechi nyingi mfululizo na ngumu.

Ni katika kipindi hiki ambapo kila timu huwa inajitahidi kuhakikisha isiteleze na kuwapa nafasi wapinzani wake.

Katika makala haya, BINGWA itajaribu kuangalia kati ya timu tano zinazochuana kileleni mwa msimamo wa ligi itakuwa na mechi zenye unafuu na zile ambazo zinakabiliwa na kibarua kigumu.

CHELSEA

 Desemba 26 vs Bournemouth (nyumbani)

Desemba 31  vs  Stoke City (Nyumbani)

Januari  4 vs  Tottenham Hotspur (ugenini)

Mechi  dhidi ya Spurs  ndiyo inaonekana kuwa ngumu kwa vinara hao wanaoongoza ligi, lakini kikosi hicho cha kocha  Antonio Conte kitakuwa kikisaka walau pointi za kutosha kikiwa nyumbani.

Unafuu mwingine ni kwamba, kuna siku kati ya tano hadi  sita  kutoka mechi moja hadi nyingine, jambo ambalo litawapa nafasi ya kupumzika.

Maoni: Wanaweza kula vizuri sikukuu  ya  Krismasi

ARSENAL

 Desemba 26 vs West Brom (nyumbani)

Januari mosi  vs  Crystal Palace (nyumbani)

Januari 3 vs Bournemouth (ugenini)

Katika kipindi hicho za siku za sikukuu, kikosi hicho cha Kocha Arsene Wenger kitakuwa na mechi mbili ambazo kitakuwa nyumbani, jambo ambalo linaweza kuwapa unafuu kwa kiasi fulani.

Hata hivyo, ugumu uliopo ni kwamba, kitakuwa na muda wa kupumzika kwa saa zaidi ya 50 kabla ya kusafiri kwenda kuivaa Bournemouth baada ya mechi baina yake na Crystal Palace kumalizika.

Maoni: Pia nao wanaweza kula vizuri sikukuu ya Krismasi.

 LIVERPOOL

 Desemba 27 vs Stoke City (nyumbani)

Desemba 31 vs Manchester City (nyumbani)

Januari 2 vs  Sunderland (Ugenini)

Licha ya Liverpool kuwa na rekodi nzuri dhidi ya Man City ikiwa kwenye uwanja wake wa  Anfield, lakini kwa jinsi ratiba ilivyopangwa, inaonekana Reds watakuwa na kazi  ya ziada ya kufanya.

Hii ni kutokana na kwamba itakuwa na siku chache za kupumzika kabla ya kwenda ugenini kuivaa Sunderland baada ya kukutana na Man City.

Maoni: Kaa la moto

MANCHESTER CITY

 Desemba 26 vs   Hull City (ugenini)

Desemba 31 vs  Liverpool (ugenini)

Januari 2  vs  Burnley (nyumbani)

Hii itakuwa ni sikukuu ya kwanza ya Krismasi kwa kocha  Pep Guardiola kuila akiwa nchini  England.

Hata hivyo, kutokana na ratiba jinsi ilivyo, itamlazimu kocha huyo kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake wakati atakapokwenda Anfield ambako Man City huwa wana rekodi mbaya.

Maoni: Pamoja na ugumu huo, lakini wanaweza kuila vizuri sikukuu hiyo ya Krismasi.

TOTTENHAM HOTSPUR

 Desemba 28 vs Southampton (ugenini)

Januari mosi vs Watford (ugenini)

Januari 4 vs Chelsea (nyumbani)

London ‘derby’ dhidi ya Chelsea ikiwa ni baada ya kucheza mechi mbili za ugenini unaonekana ndio utakuwa mtihani mkubwa kwa Spurs ukilinganisha na wapinzani wake.

Maoni: Kaa la moto kwao

MANCHESTER UNITED

Desemba 26 vs Sunderland (nyumbani)

Desemba 31 vs Middlesbrough (nyumbani)

Desemba 2 vs  West Ham (nyumbani)

Kutokana na jinsi ratiba ilivyo, Kocha Jose Mourinho  atakuwa anajivunia kuwa na mechi mbili za nyumbani zinazoonekana zinaweza kuwa ‘kitonga’ kwake.

Mechi hizo zinaipa Man Utd nafasi ya kurejesha pengine pointi ambazo ziliwateleza na hivyo kuwakaribia zaidi wapinzani wao.

Maoni: Inaweza kuwa sikukuu njema kwao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -