Friday, November 27, 2020

VIUNGO SIMBA WAMPA JEURI OMOG

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

SAADA SALIM NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amefichua siri ya mafanikio anayoyapata kwa kila timu anayofundisha, akisema mara nyingi huwa anategemea safu ya kiungo.

Omog alitoboa siri hiyo akiwa visiwani  Zanzibar ambapo aliliambia BINGWA kwamba amekuwa muumini mzuri wa kujaza viungo wengi kutokana na kuamini mafanikio yake makubwa kwa timu alizopita yalitokana na mfumo huo.

Alisema falsafa yake hiyo imemsaidia pia kupata matokeo mazuri wakati akiwa kocha wa Azam FC na iliisaidia kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Vodaom Tanzania Bara (VPL) kwa mara ya kwanza tangu ipande daraja.

“Kila safu naipa nafasi na kuwa makini, lakini suala la kutumia viungo wengi katika kikosi changu naamini ndio moyo wa timu, ambao wanaweza kuleta matokeo mazuri muda wowote,” alisema.

“Tayari katika safu yangu ya viungo sina shida, kikubwa natumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kuimarisha kwa kujenga vyema safu ya ushambuliaji ili kupata idadi kubwa ya mabao,” alisema.

Omog alisema licha ya mechi zote kupata ushindi bado anahitaji kuona timu yake inafunga mabao mengi kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Yanga.

Alisema baada ya kuendelea kuboresha safu yake ya ushambuliaji lakini pia atagusia sehemu zote huku akihakikisha anaendelea kuimarisha moyo wa timu yake ambayo ni safu ya kiungo.

Omog aliongeza kuwa kulingana na falsafa yake hiyo ameweza kutengeneza wasifu wake vizuri katika timu alizotoka ikiwamo kutwaa mataji mbalimbali akiwa na timu tofauti.

Kikosi cha timu hiyo kipo visiwani Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika katika Uwanja wa Amaan.

Simba ilianza vyema mchezo wake kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Taifa Jang`ombe.

Katika hatua nyingine, Simba watashuka dimbani leo kuvaana na KVZ ya Zanzibar katika mashindano hayo na mchezo huo wa Kundi A utakuwa wa pili kwa kila timu.

Wekundu wa Msimbazi wataingia uwanjani wakiwa na uchu wa matokeo hasa baada ya kulingana pointi na URA ya Uganda.

Kwa upande wa KVZ, wao wataingia uwanjani wakiwa na machungu ya kupoteza mchezo wao uliopita baada ya kufungwa mabao 2-0 na URA.

Mbali na mchezo huo, mechi nyingine itakayochezwa leo jioni ni ile itakayozikutanisha URA dhidi ya Taifa Jang’ombe.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa mkali kwani Jang’ombe nao walifungwa na Simba katika mchezo wa kwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -