Tuesday, November 24, 2020

VIWANJA NA MIJI ITAKAYOTUMIKA KWA AFCON 2017

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MIJI minne mikubwa ya Gabon imechaguliwa kwa ajili ya michuano ya Afcon 2017. Miji hiyo ni pamoja na Libreville, Franceville, Port Gentil na Oyem hii ni miji maarufu sana nchini humo na yote ina viwanja vya kisasa na miundombinu mizuri ya usafiri kwa maana ya barabara na viwanja vya ndege.

Stade d’Angondje,

Katika mji wa Libreville ambao ndio Mji Mkuu wa Gabon, uwanja utakaotumika kwa michuano hiyo ni Stade d’Angondje, upo katika eneo la Angondje kwenye Jiji la Libreville. Ni uwanja uliojengwa na Serikali ya Gabon kwa ushirika na Serikali ya China.

Uwanja huo una uwezo wa kubeba  mashabiki 40,000 na ulifunguliwa Novemba 2011 kwa mechi maalumu ya kirafiki ya kimataifa kati ya Gabon na Brazil, ambapo Brazil walishinda mabao 2-0 ndio uliotumika kwa fainali za Afcon za mwaka 2012.

Stade de Franceville

Katika mji wa Franceville, upo Uwanja wa Stade de Franceville ambao unamilikiwa na Serikali ya Gabon ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 22,000. Ulijengwa mwaka 2010 na kuzinduliwa 2011. Uwanja huu ulibomolewa na kisha kufanyiwa matengenezo makubwa yaliyouwezesha kuwa uwanja wa kisasa kabisa.

Stade d’Oyem

Kwenye Mji wa Oyem kuna uwanja maarufu uitwao Stade d’Oyem wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 20,500, ni uwanja mpya kabisa ambao umejengwa hivi karibuni na utaanza kutumika kwenye fainali hizi za Afcon

Stade de Port-Gentil

Uwanja huu unapatikana katika mji wa Port-Gentil, ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000. Ni uwanja unaomilikiwa na Serikali ya Gabon, umekamilika mwaka jana na umejengwa kwa ajili ya kufanikisha fainali za mataifa ya Afrika mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -