Wednesday, October 21, 2020

Waamuzi wabovu kichaka cha mapungufu ya timu zetu

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MWANDISHI WETU,

FEBRUARI 13, 1960 katika mji wa Bologna nchini Italia, alizaliwa mwanadamu aliyeaminika ndiye refa bora kabisa wa soka wa kizazi chake. Huyu si mwingine bali ni Peirluigi Collina.

Alikuwa na sura ya majukumu na macho ya kukera ya ‘paka’ yaliyomfanya aweze kuuona mpira mara nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote pale uwanjani.

Refa huyu bora wa karne ya 21, aliwahi kusema: “My job is not to change the game, but to work to everyone’s satisfaction’’, yaani, ‘kazi yangu si kubadili uelekeo wa mchezo bali kufanya kila liwezakanalo kukidhi haja za kila mmoja.”

Kazi ya mwamuzi si kutenda haki pekee, bali ni kumpatia kila mtu anachostahili. Hiki ndicho wanachokikosa waamuzi wetu wengi katika michezo ya ligi mbalimbali hapa nchini, kuanzia ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza na mashindano mengine yanayotambulika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Soka letu linapita katika wakati ambao waamuzi wamekuwa wahanga wa matokeo uwanjani, timu ifungwe kihalali au kwa makosa ya uamuzi wa marefa ndio watakuwa hoja ya mazungumzo na bahati mbaya sana, makocha wengi kwa sasa hasa wa ligi kuu na daraja la kwanza  ndio wameona chanzo au kichaka cha kujificha pindi timu yake inapopoteza mchezo. Yawezekana tukawa hatuna waamuzi wazuri wa kusimamia michezo yetu japo si kila wakati, kuna wakati mwamuzi anashindwa kulimudu pambano aidha kwa makosa yake, ya mwamuzi msaidizi au presha ya mchezo na mwendokasi wa mechi yenyewe.

Tukio la hivi karibuni la mashabiki wa Coastal Union ya mjini Tanga kuamua kumvamia na kumpiga mwamuzi wa mchezo baina yao na KMC si la kiungwana na ni la kukemewa kwa kiwango kikubwa sana.

Katika hali yoyote ile kitendo cha washabiki kumvamia mwamuzi na kumshushia kichapo katika dunia  ambayo michezo hutumika kama lugha ya mawasiliano, kuunganisha pande zinazosigana ili kuleta umoja na ushirikiano ni dalili tosha kuwa soka letu  linazama. Wakati Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) likiamini mpira ni mchezo wa kiungwana na uungwana huu si tu kwa wachezaji, makocha na viongozi bali pia kwa mashabiki na wadau wengine wakiamini katika  kuvumiliana na kuheshimiana.

Matokeo yoyote mazuri au mabaya yanapotokea mathalani yanayotokana na mwamuzi ni ya kuvumilia pasipo kuleta athari yoyote ile. Moja ya mambo mazuri katika mpira wa miguu ni kutotengua matokeo ndani ya dakika 90 za mchezo husika. Haijalishi matokeo yamesababishwa na mapungufu ya mwamuzi au vinginevyo. Hii imekuja ili kutengeneza taswira ya uungwana na kuheshimiana mchezoni.

Ndani ya mchezo wenyewe wachezaji ni watu muhimu sana katika kumsaidia refa kutenda haki na kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake, mchezo wa mpira wa miguu huchezwa hadharani na kwa miaka mingi sheria zake mama zimeendelea kuwa zile zile pamoja na kufanyiwa maboresho ili kukidhi mahitaji kwa wakati, kwa hiyo ni lazima mashabiki na wachezaji na wadau wote wapate kuelewa dhana hii ya ‘Fair Play’ katika kuendelea kuufanya mchezo huu uwe wa kiungwana, unaopendwa na watu mamilioni kote duniani.

Kumpiga mwamuzi ni kitendo ambacho si kwamba kinadidimiza soka letu na kulitia doa bali pia kinatoa tafsiri hasi kwa jamii kwamba mchezo huu hupendwa na wahuni katika mazingira kama haya huwezi mshawishi mwekezaji kuweka fedha zake kwenye mazingira kama haya.

Katika mchezo wa watani wa jadi mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi kwa mashabiki yalitoa picha ya mbali kuwa pamoja na kuwa na uwanja mzuri wa kukufanya uwe huru hata kwenda na familia, lakini ulileta mtazamo mwingine kabisa kwa watoto wanaopenda kwenda uwanjani.

Baadhi ya picha zilionesha namna ambavyo shabiki akiwa amembeba mtoto na kumkumbatia wakati mabomu yakirushwa. Lakini pia tutatengeneza kizazi cha woga.

Waamuzi chipukizi ambao wanashauku ya kuingia kwenye nafasi ya uamuzi. Paolo Di Canio pamoja na ukorofi wake kama mchezaji, Fifa ilimshamtambua kama mwanamichezo muungwana.

Kuna wakati chama cha soka cha Ireland Kaskazini mwishoni mwa mwaka 1988 kiliandaa mchezo wa mpira wa miguu ili kuwaunganisha Wakristo wa madhehebu ya Kikatoliki na Kiprotestanti waliokuwa kwenye mvutano mkubwa wa kiimani.

Pia, wakati Ivory Coast wakiwa kwenye mgogoro mkubwa kipindi cha utawala wa Laurent Ggadbo, soka ilitumika kama sehemu ya kuwaunganisha watu waliokuwa kwenye mgogoro mkubwa wa kikabila kati ya watu wa Kusini waliokuwa wanawakilishwa na Aruna Dindane na Kaskazini wakiongozwa na Didier Drogba.

Wakati Serikali ikilazimisha timu ya Taifa icheze jijini Abidjan kwa kuhofia usalama wa watu na mali zao, Didier na Aruna walilazimisha Serikali kupeleka mechi kijijini kuchezwa tena bure sehemu ambayo kulikuwa na mapigano makali ya kikabila, lengo likiwa ni kuwaonesha wananchi tofauti zao za kikabila haziwafanyi wauane.

Mchezo wa mpira wa miguu unavunja pingu za ukabila na chuki, dini na rangi, soka huwaleta watu karibu na kusahau shida zao na tofauti zao. Ni wakati wa FRAT sasa kuamka kuwasaidia wadau wao, yaani marefa.

Mwandishi wa makala haya ni James Munuo ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari John Baptist iliyopo Boko, Dar es Salaam, akiwa ni mmoja wa wachangiaji wa gazeti hili anayepatikana kwa simu namba 0675325272.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -