Saturday, November 28, 2020

WAAMUZI WALIOTIWA DOA NA ‘KARIAKOO DERBY’

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMARI NA HASSAN DAUDI

LEO ndiyo siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka hapa nchini na kwingineko kwani ule mtanange ‘Kariakoo Derby’ wa kukata na shoka baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga, unatarajiwa kutimua vumbi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Wanapokutana wababe hao wa soka la Tanzania, matukio mengi ya ndani na nje ya uwanja yamekuwa yakijitokeza na kuwa kivutio kikubwa na kugeuka kumbukumbu inayochukua muda mrefu kusahaulika.

Moja ya matukio hayo ni suala la waamuzi kubebeshwa lawama baada ya filimbi ya mwisho katika mchezo wa timu hizo.

Katika historia ya mchezo unaowakutanisha wababe hao, kuna waamuzi ambao wamejikuta wakiwa maadui wa aidha Simba au Yanga kwa kuhusishwa kuwa na mapenzi na moja ya timu hizo.

Makala haya yanakuletea waamuzi ambao wamewahi kukumbana na maneno makali ya mashabiki wa timu hizo huku makosa ya kibinadamu waliyowahi kuyafanya katika Kariakoo Derby yakionekana kuwa ni mapenzi ya upande mmoja.

Martin Saanya

Ni mwamuzi ambaye alikabidhiwa kibarua cha kuchezesha Kariakoo Derby uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana. Mtanange huo ulikuwa wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo, Saanya alionekana kuwa adui kwa mashabiki wa Simba kwa kitendo chake cha kukubali bao lililotajwa kuwa si halali la straika wa Yanga, Amissi Tambwe.

Kwa mujibu wa mashabiki wa Simba, Tambwe alikuwa ameunawa mpira kabla ya kuutumbukiza kimiani.

Lakini pia, aliongeza hasira kwa mashabiki hao wa Wekundu wa Msimbazi kwa kitendo chake cha kumpa kadi nyekundu nahodha wao, Jonas Mkude. Kitendo hicho kilisababisha mashabiki wa Simba kufanya vurugu uwanjani hapo na kuharibu miundombinu ikiwamo kuvunja viti na mageti.

Hashimu Abdalah

Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha mchezo wa Mei 5, 2012 ambapo Yanga waliambulia kipigo cha aibu cha mabao 5-0.

Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Mganda, Emmanuel Okwi aliyepasia nyavu mara mbili, Felix Sunzu, mlinda mlango, Juma Kaseja na Patrick Mafisango ambaye ni marehemu.

Inadaiwa kuwa mwamuzi Abdallah alikuwa mwanachama wa Yanga lakini kilichowakera mashabiki wa timu hiyo ni kitendo chake cha kushindwa kuipa ushindi.

Hivi sasa Abdallah ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga baada ya hivi karibuni yeye na wenzake, Ayoub Nyenzi na Salum Mkemi, kusamehewa makosa yao na kurejeshewa uanachama wao.

Jonesia Rukyaa

Rukyaa ndiye aliyeshika kipenga wakati Simba na Yanga zilipokutana Februari 20, mwaka jana.

Kilichomponza mwanamama huyo ni kitendo chake cha kumlima kadi nyekundu nyota wa Simba, Abdi Banda, katika mtanange huo wa raundi ya pili wa Ligi Kuu ambapo Yanga walishinda mabao 2-0.

Tukio hilo lililotokea dakika ya 25, liliwakera mashabiki wa Simba na kuamini kuwa mwamuzi huyo alikuwa amewabeba wapinzani wao Yanga.

Kutoka kwa Banda kuliirahisishia kazi Yanga na ndipo mabao mawili yalipoingia na kuwaumiza zaidi mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi.

Itakumbukwa kuwa huo ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kuchezesha Kariakoo Derby kwenye ligi baada ya kufanya hivyo kwenye Mtani Jembe, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kuchapwa mabao 2-0.

Israel Nkongo

Nkongo ndiye aliyesimama katikati ya uwanja wakati Yanga na Simba zilipoavaana Machi mwaka jana. Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulimalizika kwa Simba kuibuka kidedea na ushindi wa mabao 2-0.

Mashabiki wa Yanga walikuwa wakimshutumu Nkongo kwa madai kuwa ‘aliwaua’ katika mchezo huo kwa kuwa alikuwa na mapenzi na Simba.

Itakumbukwa kuwa Nkongo aliwahi kuchezea kichapo kutoka kwa wachezaji wa Yanga katika mchezo dhidi ya Azam. Katika mtanange huo uliochezwa Taifa, Yanga walikufa mabao 3-1.

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stefano Mwasyika, walimvaa mwamuzi huyo baada ya kumpa kadi nyekundu Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ikiwa ni baada ya kumfanyia hivyo Haruna Niyonzima.

Kitendo hicho kiliwakera mashabiki wa Yanga na kuanzia hapo wamemfanya Nkongo kuwa adui yao mkubwa.

Othman Kazi

Kazi ni miongoni mwa waamuzi waliowahi kufanya vizuri kwenye soka la Bongo kabla ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kisha kutangaza kustaafu.

Mwamuzi huyo hakuwa akikubalika kwa mashabiki wa Yanga na chuki zao kwake ni kitendo chake cha kupuliza filimbi ya mapumziko wakati Yanga walipokuwa wakielekea kulishambulia lango la Simba.

Sababu nyingine ambayo mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiitoa kumpinga Kazi ni kuwa mara nyingi timu yao imekuwa ikichapwa na Simba, jambo ambalo limekuwa likiwatia wasiwasi kuwa ‘anawanyonga’.

“Sijawahi kuipendelea Simba na hata ukichunguza mechi zao nilizowahi kuchezesha nilitoa kadi nyekundu kwa wachezaji wao lakini bado wakashinda mechi,” alisema Kazi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -