Friday, November 27, 2020

WAAMUZI WAWE MAKINI HATUA HII YA LIGI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LIGI Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara imefika katika hatua tamu na ngumu mno kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo. Mbio za ubingwa zimenoga kwa miamba ya soka hapa nchini, Simba na Yanga wakati vita ya kukwepa kushuka daraja pia nayo imenoga sana.

BINGWA tunafahamu kwamba ligi inapofika katika hatua hii, mambo mengi sana yanajitokeza kwa timu kutafuta matokeo kwa mbinu mbalimbali za ndani na nje ya uwanja ili tu zifanikishe malengo yake.

Kutokana na hilo la kila timu kutaka matokeo mazuri, waamuzi wamekuwa katika wakati mgumu sana kwani mara zote wamekuwa waathirika wakubwa wa matokeo ya uwanjani hasa kutokana na dhana iliyojengeka miaka mingi kwenye ligi yetu kwamba waamuzi huingia wakiwa na matokeo mfukoni.

Kuingia na mtokeo mfukoni, ni dhana ambayo imejengeka kutokana na dhana ya kuwepo kwa rushwa ambapo waamuzi wamekuwa wakihusishwa na kupewa mlungula ili kupindisha sheria 17 za soka kwa manufaa ya timu fulani.

Tumeshuhudia waamuzi kwenye ligi yetu wakifanya maamuzi ambayo yamekuwa na utata mkubwa hasa katika mechi za siku za hivi karibuni.  Kuthibitisha kwamba maamuzi yao yamekuwa na mkanganyiko, ni pamoja  kutenguliwa kwa maamuzi yao na Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambayo mara kadhaa imekuwa ikitengua uamuzi wa uwanja wa waamuzi wetu.

BINGWA tunapenda kuwaasa waamuzi wanaochezesha mechi za ligi kuu kuwa makini, kuchezesha kwa kufuata sheria na kanuni ili kuepusha malalamiko dhidi yao na kuepuka kudhalilika kwa maamuzi yao kutenguliwa kutokana na kuwa wameyatoa visivyo.

Haikupendeza kwa mwamuzi Ahmed Simba kulikataa goli na Obrey Chirwa na kumpa kadi ya njano ambayo ilisababisha kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting. Udhaifu wa aina hii kwa waamuzi lazima udhibitiwe ili kuhakikisha ligi inakwisha salama na kwa amani na kila timu inavuna ilichostahili kwa haki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -