Monday, October 26, 2020

Waarabu wa Oman waijaza minoti Simba

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA

KLABU ya Fanja FC ya Oman imeijaza minoti Simba baada ya kuipatia kiasi cha dola 10,000 (sh milioni 22) kama malipo ya usajili wa straika wa zamani wa miamba hiyo ya Msimbazi, Danny Lyanga, aliyejiunga na vijana hao wa Uarabuni mwishoni mwa mwezi uliopita.

Baada ya Lyanga kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Fanja, klabu ya Simba ilitaka kulipwa dau hilo kama ada ya uhamisho na baada ya mvutano wa hapa na pale hatimaye Waarabu hao wametuma fedha hizo.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele, alisema awali Fanja walitaka kumchukua bure Lyanga, lakini timu yake iligoma na hatimaye Waarabu hao wakalainika na kukubali kutoa fedha hizo.

Kahemele alisema kuwa baada ya kupokea fedha hizo walitoa dola 3,000 (sh milioni 6.6) na kumpa Lyanga mwenyewe kwa sababu bado alikuwa akiidai klabu hiyo na kubakiwa na Dola 7,000 (sh milioni 15.4) ambazo ni faida kwao na watazitumia kwenye mambo mbalimbali.

“Fedha za Lyanga zimeshakuja,” alisema Kahemele. “Jamaa wamelipa dola 10,000, kati ya hizo tumempa Lyanga dola 3,000 ambazo alikuwa anatudai kama malimbikizo ya mshahara na deni la usajili huku klabu ikipata dola 7,000.”

Kahemele aliendelea kusema kwamba kwa kuwa Simba kwa sasa haina udhamini, fedha hizo zimesaidia matumizi kadhaa ikiwemo suala zima la kusaka ubingwa msimu huu.

“Simba haina mfadhili wala mdhamini kwa sasa, hivyo fedha zimesaidia kwenye mambo mengi ikiwemo kuhakikisha tunatwaa ubingwa safari hii,” alisema.

Simba ilimweka Lyanga sokoni baada ya kocha Joseph Omog kusema kuwa hakuwa kwenye mipango yake na kumtaka atafute timu nyingine ya kuchezea ili kulinda kipaji chake hapo ndipo staa huyo akatimkia Fanja FC.

Lyanga alitua Simba akitokea DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kusaini mkataba wa miaka miwili, lakini akatumikia mwaka mmoja kabla ya kuuzwa Uarabuni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -