Wednesday, November 25, 2020

Wachambuzi wanena ubora wa vikosi Simba, Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

ITAFAHAMIKA tu baada ya dakika 90, hivyo ndivyo wanavyosema wachambuzi wengi wa soka hapa nchini, wakitoa maoni yao kuelekea pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga.

Kipute cha Simba na Yanga, timu zenye ushawishi mkubwa wa mashabiki, kitapigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kila upande umetamba kuibuka wababe kutokana na ubora wa kikosi chake.

Yanga inajivunia kasi ya wachezaji wake ambao wamekaa pamoja kwa muda mrefu, wakati Simba wanaringia usajili makini walioufanya msimu huu.

Ieleweke kuwa Simba itaingia uwanjani leo ikiwa na shauku ya kutaka kulipa kisasi cha kucharazwa mabao 2-0 na Yanga katika mechi zote mbili za Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

BINGWA limefanikiwa kuzungumza na baadhi ya wachambuzi wa soka ambao wanatoa maoni yao kuhusiana na nafasi ya kila upande kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Ally Mayay

Ni mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka.

Anasema ni vigumu kwake kutabiri mchezo huo kwavile kila upande unaonekana kuwa vizuri.

“Msimu huu Yanga haijafanya usajili mkubwa lakini  wachezaji wake wamekaa pamoja kwa muda mrefu, tofauti na Simba ambayo  kocha wake, Joseph Omog ndiyo kwanza yupo kwenye mchakato wa kuijenga kuishindani.

“Ukiangalia Yanga wachezaji wake wengi wanaonekana kuchoka, kwani hawajapata muda wa kupumzika, ingawa hiyo haiwezi kuwa sababu moja kwa moja ya kuwafanya washindwe  kung’ara katika mchezo huo.

“Pia ni vigumu kujua kocha Pluijm atakuja na mbinu gani mpya dhidi ya mahasimu wao. Ukiangalia Simba wamebadilika sana kwa sasa, kwani kikosi chao kina kasi, wanamiliki mpira na beki yao ipo imara sana,” anasema Mayay.

“Ubora wa Simba upo katika kumiliki mpira kwenye viungo kuanzia kwa Jonas Mkude, Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Jamal Mnyate na  Mohamed Huusen, lakini  Yanga wapo vizuri katika kufanya  mashambulizi ya kushtukiza(counter attacks) kupitia kwa Simon Msuva na hata Juma Mahadhi.

“Hii inatosha kuwapa uwezo wa kufunga bao hata kama watashindwa katika kumiliki mpira katika sehemu ya kiungo.

Anasema watu wengi wanatarajia kuiona Simba ikiendelea kutumia mfumo wao wa 4-3-3 ambao ndio wenye nafasi ya kuwapa ushindi mbele ya watani zao, lakini kwa Yanga waliotoka kupoteza mechi mbele ya Stand United wanahitaji kurejesha imani kwa mashabiki wao, hivyo kuna uwezekano  kocha Pluijm asitumie viungo wakabaji wawili kama  ilivyozoeleka.

Joseph Kanakamfumu

Kocha huyo anasema timu zote zina nafasi nzuri ya kushinda, ingawa hadi sasa Yanga haina kikosi kipana kama ilivyo kwa Simba.

“Ukiangalia katika safu ya ulinzi, Yanga ndiyo inaonekana kuwa na mabeki mahiri kwa maana ya wale wanaoanza na wale wanaosubiri benchi, lakini ukija kwenye  ushambuliaji hapo ndipo tatizo lililo, kwani yupo Amiss Tambwe na Ngoma tu na ukienda kwa viungo kama asipokuwepo Thaban Kamusoko ni lazima timu icheze chini ya kiwango.

“Kitu kitakachoibeba Yanga katika mchezo huo ni mbinu za kocha tu ambaye kwa kiasi kikubwa tayari analijua soka la Tanzania na hata mechi za watani ,” anasema Kanakamfumu.

Kanakamfumu anasema, Simba wana nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo, lakini anaitaja sababu ambayo inaweza kuwa kikwazo kuwa ni idadi kubwa ya  wachezaji  wapya.

Ulimboka Mwakingwe

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba ambaye alistaafu kwa  heshima kubwa anasema kwa mtazamo wake na kuangalia ubora wa timu zote mbili, Simba wana  nafasi nzuri ya kuishinda Yanga.

“Ukikiangalia kikosi cha Simba unaweza kukiita cha mwendo kasi  na hiyo ni kutokana na kasi waliyonayo, ni tofauti na msimu uliopita. Kama ubora waliouonyesha katika michezo iliyopita ya ligi ndio utakaoonekana kwenye mechi yao na Yanga, basi watashinda.

“Usajili walioufanya Simba umetulia na una faida kwao, ukianza kuangalia kazi anayoifanya Kichuya, Mwanjali, Mzamiru na wengine ni wazi kuwa walikaa chini na kuumiza kichwa juu ya mchezaji gani anastahili kuwemo kikosini mwao,” anasema Mwakingwe, ambaye enzi zake alisifika kwa kasi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -