Monday, October 26, 2020

Wachezaji 20 kushiriki taekwondo Kenya

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA JACKLINE LAIZER, ARUSHA

WACHEZAJI 20 wa Taekwondo wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice, iliyopo mkoani hapa, wanatarajiwa kushiriki michuano ya wazi itakayofanyika kesho jijini Nairobi, nchini Kenya.

Michuano hiyo inayojulikana kama ‘Loreto Valley Road Tekwondo Championship and National Cadet & Team Build up’, itashirikisha wachezaji waliochini ya umri wa miaka 13-18.

Akizungumza mkoani hapa jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Taekwondo Tanzania (TTF), Richard Kitolo, alisema michuano hiyo itashirikisha wachezaji mbalimbali kutoka shule na vyuo nchini humo.

Kitolo alisema wamepata mwaliko wa kwenda kushiriki michuano hiyo na watakuwa na kikosi cha wachezaji 20 kinachoundwa na wasichana na wavulana.

Alisema kikosi hicho kitaunda makundi manne yenye wachezaji watano kwa kila moja, kwani anaamini watafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kitolo alisema michuano hiyo imeandaliwa na  Chama cha Taekwondo kutoka shule na vyuo, wakishirikiana na shirikisho la mchezo wa taekwondo nchini Kenya (KTF),  lengo likiwa ni kupata timu ya nchi hiyo  itakayoshiriki michuano ya kimataifa nchini Canada.

“Tumepeleka wachezaji wa shule moja kutokana na shule hiyo kuwa na mwamko wa mchezo huu, hivyo ninawaomba wadau kushirikiana na Chama cha Taekwondo Tanzania kwa pamoja kuhamasisha mchezo huu uchezwe shuleni na vyuoni,” alisema Kitolo.

Alisema ili mchezo huo uweze kupiga hatua, unatakiwa kuanzia kuchezwa shuleni ambako kuna vipaji vingi chipukizi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -