Friday, October 30, 2020

Wachezaji Man United wanaendana na Mourinho?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

HIVI sasa hali si shwari kwa Jose Mourinho wa klabu ya Manchester United na juzi aliwajia juu wachezaji wake akiwaambia wanatakiwa kujituma zaidi.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, wachezaji waliopo Old Trafford hawana sifa anazozitaka kocha huyo raia wa Ureno.

Alipochukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Porto, Mourinho alishangaza wengi lakini hakuna aliyeshangaa alipoiwezesha Inter Milan kunyakua taji hilo mwaka 2010 na ndipo uwezo wa Mourinho ulipofahamika.

Ni katika kipindi hicho ndipo alipochukuwa mataji matatu kwa mpigo na hata Rais wa Inter, Massimo Moratti, aliwahi kukiri kuwa Mourinho alikuwa kwenye ubora wake.

“Tulikuwa ni timu ya mashujaa. Tulikuwa hatari,” alisema Moratti.

Mafanikio ya Mourinho yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na kikosi cha Inter kilichokuwa kikiundwa na mastaa wengi akiwemo mkongwe Javier Zanetti.

Baada ya kuichapa Barcelona katika mchezo wa hatua ya nusu fainali kabla ya kuchukua ‘ndoo’, Mourinho alitamka wazi kuwa hakuwahi kufundisha timu bora kama Inter.

Akiwa na umri wa miaka 26, ilikuwa  ngumu kumtofautisha Wesley Sneijder na kinda wa miaka 18, alijitoa kwa kiwango kikubwa huku Marco Materazzi akiwa kwenye ubora wa hali ya juu.

Pale Old Trafford, kwa sasa Mourinho haonekani kuwa na nguvu ya kikosi alichokuwa nacho na hata yeye aliwahi kukiri hilo aliposema: “Ingekuwa rahisi kwangu kama ningesajili wachezaji wapya 20 na kuanza upya.”

Hata baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Swansea, kocha huyo alitoa kauli ambayo iliwalenga mastaa, Chris Smalling na Luke Shaw ambao ni majeruhi.

“Smalling hahisi kama anaweza kucheza kwa asilimia 100 kutokana na maumivu. Shaw aliniambia asubuhi (Jumapili ya wiki iliyopita) kuwa hawezi kucheza, hivyo tulitakiwa kuimarisha safu ya ulinzi.

“Kuna tofauti kati ya shujaa anayeweza kujitoa kwa namna yoyote na yule anayekaa nje kwa majeruhi kidogo,” alisema Mourinho ikiwa ni ‘dongo’ lake kwa wachezaji hao.

Katika kuthibitisha kuwa Mourinho hana aina ya wachezaji anaowahitaji, itakumbukwa kuwa, alipokuwa na Inter, beki wake kisiki Cristian Chivu alicheza michezo mingi licha ya kupata majeraha ya fuvu.

Kinachomsumbua Mourinho kwa sasa ni kibarua cha kuinoa Man United ambapo anatakiwa kuwekeza katika vijana kuliko kuingia sokoni na ni wazi kuwa anafanya kazi na kundi la ‘watoto’ wasio na uzoefu. Mfano; David de Gea, ni mchezaji mdogo kuliko wote aliokuwa nao Inter.

“Tulianza msimu vizuri sana. Lakini nilifikiri kazi imeisha na tuko fit? Hapana. Nilijua wazi kuwa tuna mapungufu na kuna wachezaji ambao ni wachanga na wanaoweza kufanya makosa,” alisema Mourinho.

Kabla ya kupata majeraha, Eric Bailly alionyesha umuhimu kwenye safu ya ulinzi lakini hata Mourinho amewahi kukiri kuwa alimsajili nyota huyo akiwa hamwamini.

Kuthibitisha alichokisema Mourinho, katika mchezo wa Manchester derby dhidi ya Man City, Mwafrika huyo alishindwa kucheza michezo ya juu, hivyo bado si mchezaji aliyekamilika na madudu ya Daley Blind yalisababisha Kevin De Bruyne kupachika bao la kuongoza.

Katika mchezo ambao waliambulia kichapo cha mabao 4-0, Blind na Smalling walicheza fyongo na kumpa nafasi Pedro kufunga bao la kwanza la Chelsea.

Mourinho anaamini mbinu zake za ufundishaji ziko sawa, ila tatizo ni wachezaji kushindwa kufuata maelekezo yake.

“Kama ungeondoa makosa ya safu ya ulinzi katika mchezo huo (dhidi ya Chelsea), ningesema mchezo ulikuwa mzuri,” alisema Mourinho baada ya kichapo cha mabao 4-0 kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridghe.

“Uwezo wa hali ya juu, kumiliki mpira, kutumia mipira, kutengeneza nafasi za mabao na kupandisha mashambulizi. Lakini hatuwezi kufuta makosa,” alisema Mourinho.

Wachambuzi wanaomuunga mkono kocha huyo wa zamani wa Real Madrid wamedai kuwa si sahihi kusema mbinu zake zimekwisha ila amekutana na rundo la wachezaji wasio na uzoefu.

Kwa mujibu wao, Mourinho amezoea kufanya kazi na wachezaji wenye umri mkubwa na wanaojiamini na ndiyo maana historia yake katika kukuza vipaji vya makinda si ya kuvutia.

Hata Zlatan Ibrahimovic alipokuwa kwenye ukame wa mabao, kocha huyo alisema hana shaka kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Sweden atazinduka na kurejesha makali yake mbele ya lango la wapinzani wao.

Hao ndio aina ya wachezaji anaowahitaji Mourinho na hata baada ya kuchapwa na Chelsea pale Stamford Brudge, Mreno huyo alikaririwa akisema: “Soka si mchezo wa watoto.”

Kwa kile alichokisema kocha huyo, ni ngumu kwa wachezaji vijana kuhimili presha za ndani na nje ya uwanja, ni tofauti na majembe aliyoyakuta Inter mwaka 2010.

Ili Mourinho aweze kurejesha heshima yake na klabu hiyo ambayo imekuwa kwenye hali mbaya tangu ilipoachana na ‘babu’ Sir Alex Ferguson, wachambuzi wamemtaka kuingia sokoni Januari ili kutengeneza upya kikosi alichonacho kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -