Tuesday, November 24, 2020

Wachezaji waulizwe kinachoimaliza Stars

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HASSAN DAUD

WENGI tumekuwa bize sana siku hizi kutokana na ugumu wa maisha. Hasa sisi wadau wa soka, huenda tumekuwa tukipitwa na baadhi ya matukio muhimu ya mchezo huo kutokana na hali hiyo.

Kuna matukio mawili ambayo yametokea katika siku za hivi karibuni ambayo si rahisi kukwepa kuyazungumzia, licha ya ubize wetu.

Kwanza, ilitoka orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Tanzania imeporomoka hadi nafasi ya 144. Ni wazi soka la Bongo liko mahututi.

Huku tukitafakari ni kitu gani kilichosababisha Tanzania kuzidi kuporomoka kwenye ulimwengu wa soka, Taifa Stars ikakubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Zimbabwe. Watoto wa mjini wanasema ni majanga mwanzo, kati na mwisho!

Mbali na majanga hayo, ambayo ndiyo kiini cha makala haya, nikukumbushe tu kwamba, wiki chache tu zilizopita, Stars ilipoteza matumaini ya kucheza Fainali za Mataifa ya Africa (AFCON 2017). Nuksi tupu.

Tukirudi kwenye matukio hayo mawili (kuporomoka kwenye viwango vya FIFA na kufungwa na Zimbabwe), hakuna shaka kuwa matukio hayo yameakisi namna soka letu linavyozidi kuchanja mbuga kutokomea kusikojulikana.

Ndiyo, huenda wengi wakadharau kwa kuwa mchezo huo dhidi ya Zimbabwe ulikuwa wa kirafiki, hivyo haukuwa na umuhimu wowote. Lakini si hivyo.

Ikumbukwe kuwa, mtanange huo ulikuwa kwenye kalenda ya FIFA, yaani unahesabika kwenye upangaji wa viwango vya ubora wa timu za taifa.

Kwa maana nyingine, kitendo cha kutopata matokeo mazuri katika mchezo huo ni kujichongea kwenye viwango vya ubora vinavyoandaliwa na Shirikisho hilo.

Hata hivyo, baada ya matukio hayo mawili, idadi kubwa ya mashabiki wameelekeza lawama zao kwa ama kocha Boniface Mkwasa, au Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF).

Wapo wanaoamini kuwa, Mkwasa hastahili kuifundisha Taifa Stars kwa madai kuwa hata Yanga alikuwa msaidizi tu. Kwa tathimini ya haraka, wao wanaamini ugonjwa wa Stars uko kwenye benchi la ufundi, linaloongozwa na Mkwasa.

Lakini pia, wengine wameibuka na madai kuwa uongozi wa TFF umeshindwa kuweka mipango madhubuti kuhakikisha soka la Bongo linapiga hatua.

Huenda wadau wa soka wa makundi hayo mawili wana hoja za msingi, lakini bado kuna tatizo ambalo sidhani kama wamepoteza hata sekunde mbili kulifikiria.

Nini kinachowasumbua wachezaji wa kizazi hiki? Hilo ndilo swali wanalotakiwa kujiuliza kabla ya kuanza na kocha au TFF.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa hata wachezaji wa kizazi hiki wakashindwa kukwambia kinachowafanya washindwe kutupeleka kwenye kilele cha mafanikio ya mchezo wa kandanda. Ngoja nikwambie kitu.

Kwa uchunguzi mdogo tu na usiohitaji elimu ya chuo kikuu, katika miaka ya hivi karibuni, asilimia kubwa ya mastaa wa Taifa Stars wamekuwa ni wale wanaozichezea Simba, Yanga na Azam.

Mbali na posho nzuri wanayopewa wanapokuwa na Taifa Stars, wachezaji hao wamekuwa wakivuna mpunga mrefu wanapokuwa na klabu hizo zenye heshima kubwa kwenye soka la hapa Bongo.

Ni ngumu kufananisha na nje ya nchi, lakini ukweli ni kwamba, hivi karibuni wachezaji wa Bongo wamekuwa wakiishi kifalme kutokana na fedha nyingi wanazovuna.

Lakini je, tukitazama kile wanachokifanya wakiwa na Taifa Stars, kinafana na fedha walizonazo kwenye akaunti zao? Bila shaka jibu ni hapana.

Wakati Tanzania inashiriki fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1980, ni mchezaji gani aliyekuwa akimiliki japo usafiri wa milioni 10?

Kipindi kile, tunaweza kusema lilikuwa ni soka la ridhaa tu na wala hakuna mchezaji aliyekuwa akitegemea kujenga nyumba, kumiliki gari kupitia mchezo huo.

Kuthibitisha hilo, jaribu kuwatembelea wachezaji wa zamani hasa wale waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars mwaka 1980.

Wengi wamekufa masikini na hata waliopo wanaishi maisha ya kuungaunga kama wasemavyo watoto wa Uswahilini. Asilimia 99 wanajutia muda waliupoteza kwenye soka wakiamini wangekuwa matajiri leo hii kama wangefanya kazi nyingine.

Hakuna ubishi kuwa wachezaji wa kizazi hiki wana bahati kubwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliopo kwenye soka. Tofauti na kipindi hicho, leo hii mchezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ana uhakika wa kuvuna mshahara wa milioni 2 kila mwezi huku akiwa amezungukwa na vifaa vya kisasa vya kujifua.

Simaanishi wachezaji wa Stars wanapaswa kubebeshwa lawama kwa timu hiyo kufungwa na Zimbabwe au kufanya vibaya kwenye viwango vya FIFA, ila wajitathimini upya.

Wanachotakiwa kujiuliza ni je, wanatekeleza wajibu wao ipasavyo? Pia, wamejipanga vipi kulipa fadhila kwenye mchezo wa soka, ambao umewafanya waishi peponi wakiwa duniani? Naomba kuwasilisha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -