Friday, November 27, 2020

WACHEZAJI YANGA MSIINGIE KWENYE MTEGO WA MASHABIKI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SOSTHENES NYONI

NI ukweli ulio dhahiri mashabiki wengi wa Yanga na hata kama nikisema wa Tanzania, naamini niko sahihi walikata tamaa baada ya klabu hiyo kupangwa kuanza kampeni zake za michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuvaana na timu ya Alger ya nchini Algeria.

Wengi wanaamini Yanga tayari imetupwa nje ya michuano hiyo, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni suala la muda tu ufike.

Wengi wanaamini hivyo, ni kutokana na rekodi kuonyesha Yanga imekuwa ikishindwa kutamba kila inapokutana na  timu za Kiarabu katika michuano ya CAF.

Haijalishi Waarabu hao wanatoka katika taifa gani, tatizo hapa ni ule Uarabu ndiyo ambao umekuwa ukiisumbua Yanga.

Licha ya kwamba fikra hizi kwa asilimia kubwa kama si zote mwisho wa siku  zinakuja kuwa na kweli, pia hazifai kutiliwa maanani sana kwakua soka la Afrika kwa sasa limebadilika sana kuanzia ngazi ya klabu hadi timu za taifa.

Ukweli ni kwamba, viwango vya soka vya nchi nyingi ambazo miaka ya nyuma zilionekana wasindikizaji, sasa zimepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Kuimarika huko kwa soka la nchi ambazo miaka ya nyuma zilionekana goigoi ikiwamo nchi yetu ya Tanzania, kumezidisha ushindani katika mechi mbalimbali zinazosimamiwa na CAF.

Hali hii imesababisha zile nchi ambazo kwa miaka mingi zilionekana bora na kutawala soka la Bara la Afrika, kuonekana kama zimeporomoka kiviwango wakati kiuhalisia si kweli, kinachotokea ni kwamba, wale walioonekana dhaifu wamepambana na sasa wameimarika.

Hata Yanga ya sasa si ile ya miaka 10 iliyopita, hii imeimarika na imepiga hatua kubwa kiuchezaji licha ya kwamba haipata mafanikio makubwa.

Utakubaliana na mimi kwa kuangalia matokeo na kiwango ambacho imekuwa ikikionyesha katika mechi zake katika  miaka ya karibuni.

Hata pale inapotokea imeondolewa  mashindanoni, lakini imekuwa ikiwaridhisha mashabiki wa soka kutokana na kuonyesha kandanda safi na lenye ushindani wa kweli tofauti ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Jaribu kukumbuka Yanga ya wakati ule ilipokuwa inakutana na timu kama Al Ahly au Zamarek za Misri, nini kilitokea. Iliambulia vipigo vya mabao mengi kuanzia katika mechi za nyumbani mpaka ugenini.

Nije kwenye msingi wa kuandika makala haya leo, binafsi naamini Yanga ina uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi ya MC Alger na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kama itazingatia mambo haya.

Kwanza kabisa viongozi wa Yanga mbali ya kuhakikisha wanaiandaa vizuri kiufundi timu yao, pia wanatakiwa kuwaweka sawa kisaikolojia kwamba hakuna kinachoshindikana kama wataamua.

Wachezaji wa Yanga wanapaswa kujiuliza kwamba kama waliweza kuikabili na kufanikiwa kushinda nyumbani kabla ya kutolewa kwa mbinde Msri na Al Ahly, timu yenye mataji saba ya Ligi ya Ubingwa Afrika kwanini isiwezekane kwa MC Alger?

Jambo la msingi ni kuhakikisha kwanza wanafanikiwa kupata ushindi mnono nyumbani, ili kurahisisha kazi watakapokwenda ugenini.

Ili la kupata matokeo mazuri nyumbani ni muhimu kwa vile uzoefu unaonyesha hapa ndipo ambapo Yanga imekuwa ikijiharibia na kushindwa kufikia malengo yake ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kutokana na kuibuka na ushindi dhaifu au kupoteza kabisa mchezo.

Pia wachezaji wa Yanga wajiepushe kuingia katika mtego wa mashabiki wao ambao ni kukata tamaa na kujiona  wameondolewa mashindanoni hata kabla ya kukutana na wapinzani wao.

Kitendo tu cha kuangukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa mimi nakiita ni bahati isiyoelezeka, hivyo ni wajibu wa wachezaji wa Yanga kupambana kwa nguvu ili kujenga heshima ya klabu yao lakini pia ya Watanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -