Sunday, November 29, 2020

Wachezaji Yanga wamkingia kifua Pluijm

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

WAKATI kukiwa na  tetesi za Yanga kutaka kumbadilisha majukumu kocha wao mkuu, Hans van der Pluijm, kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo ya kusuasua Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, winga wa kikosi hicho, Simon Msuva, amesema tatizo si kocha bali ni uchovu wa wachezaji.

Akizungumza na BINGWA juzi, Msuva alisema matokeo yanayopatikana yanatokana na wachezaji kutopumzika kwani walicheza mfululizo.

“Sina uhakika kama taarifa hizo ni za kweli, lakini iwapo kama ni mpango uliopo watakuwa wanamwonea Pluijm,  kwani wachezaji tumechoka kutokana na kukosa muda wa kupumzika.

Ukiangalia kibinadamu tumemaliza ligi msimu uliopita tukacheza Kombe la FA, tukaingia kwenye Ligi ya Mabingwa kabla ya Kombe la Shirikisho Afrika  tumetoka,” alisema.

Alisema ana imani wana nafasi ya kutetea taji lao iwapo wataendelea kumwamini Pluijm, kwani hata msimu uliopita walianza kwa kutoa sare.

Nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema kufanya kwao vibaya kwa baadhi ya mechi  hakutokani na kocha wao kwani wana uchovu.

Cannavaro alisema wao kama wachezaji kwa upande wao hawana taarifa zozote kutoka kwa viongozi wa timu hiyo juu ya ujio wa kocha huyo mpya.

“Sisi kama wachezaji hatuna taarifa hizo, kwa kweli kimsingi tunaona na kusoma tu katika magazeti, mimi kama kiongozi wa wachezaji sijaambiwa lolote na uongozi kuhusu kuja kocha mpya,” alisema Cannavaro.

Alisema wachezaji bado wana imani na kocha Pluijm pamoja na uvumi unaonea kwamba ameishiwa mbinu za ufundishaji na hana jipya ndani ya kikosi hicho cha Jangwani.

“Kocha hana tatizo, katupa ubingwa bara, ubingwa wa FA, tumefika robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika ni mafanikio makubwa ambayo mimi kwa upande wangu naamini kocha Pluijm hana tatizo.”

Alisisitiza kuwa tatizo linaloikabili timu hiyo hivi sasa ni uchovu kwa wachezaji uliotokana na kucheza mechi nyingi mfululizo za kimataifa na kitaifa na wala si kocha kama wengi wanavyofikiri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -