Friday, November 27, 2020

Wafungeni mabao, asifunge CR-Saba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NILIULIZA wiki iliyopita nani aanze kati ya Morata na Benzema. Pia nani aanze kati ya Bale na James au James na Isco. Mwingine ni nani aanze kati ya Isco na Lucas Vazquez au Marco Asensio. Wote hawa ni wachezaji wazuri kikosini.

Kila mmoja anaweza kukupatia kitu kinachofaa kwa timu. Asensio amefunga mabao kila mechi aliyopangwa. Yeye ni mechi-bao. Kocha yeyote atakuwa anatamani kuona mabao hayo yanapatikana kila mechi.

Inabidi ajiulize nani aanze kati ya Asensio na James au nani aingie kama mchezaji wa akiba kati ya Vazquez na Asensio. Morata na Benzema ni wachezaji tofauti. Nilionyesha maarifa ya Benzema na Morata.

Nilionyesha ufundi wa James na Isco. Uzuri wa Isco anakufanya timu icheze mabegani mwake, yaani anaendesha timu kila upande. Sasa tatizo jukumu hilo analo Luka Modric. Nani utampanga hapa? Modric pia anakaribiwa na Matteo Kovacic. Shughuli pevu.

Sasa katika kufunga mabao ndipo tatizo linaanza. Kila mchezaji anatakiwa kufunga bao. Mabeki wafunge mabao. Viungo wakabaji wafunge mabao. Mawinga wafunge mabao. Viungo washambuliaji wafunge mabao. Washambuliaji wafunge mabao.

Hapo ndipo unakutana na changamoto ya mchezaji anayetakiwa kuanza katika mechi. Utajiuliza nani aanze kati ya Pepe na Varane. Utajiuliza nani aanze kati ya Mzee wa Madoido Marcelo au mdambwidambwi Fabio Coentrao. Au utatamani kumpanga kinda mwenye mashuti makali na mabavu Mariano Diaz?

Matokeo ya maswali hayo ni haya; mechi za hivi karibuni Cristiano Ronaldo (CR-SABA) hakufunga mabao, lakini timu iliibuka na ushindi wa pointi tatu. Katika mabao hayo utaona viungo wametupia. Mabeki wanatupia. Mawinga wanatupia.

Lakini kinara wa mabao CR-Saba hakutupia, bali alitengeneza mabao. Mabadiliko hayo ndiyo yamefanywa na Zinedine Zidane. Kutoka kumtegemea CR-Saba kama mpachikaji mabao wa kutegemewa hadi kuitegemea timu nzima. Rekodi hazidanganyi.

Mechi za hivi karibuni mabeki wetu Raphael Varane, Pepe, Marcelo, Nacho, Sergio Ramos, Carvajal wametupia mabao. James, Morata, Vazquez, Asensio, Isco, Kovacic wote wamefanikiwa kutupia mabao. Mechi ya juzi imeleta kitu kingine.

Wapigaji wa mipira ya adhabu wamebadilika. Kwa sasa adhabu zinapigwa na wachezaji watatu, James Rodriguez, Gareth Bale na CR-Saba yaani CR7. Zidane alipoulizwa na wanahabari alijibu kifupi tu; tunao wapigaji watatu na hilo ni jukumu lao.

Bila shaka kila mmoja angetamani kuona Ronaldo anafunga mabao. Lakini sasa Zidane anataka kuifanya timu iwe inatupia mabao mengi. Kwamba asipofunga Benzema basi tunaona Morata anatupia.

Akikosa kufunga CR-SABA basi James, Bale, Varane, Kovacic, Modric nao watatupia. Ni suala hilo ndilo linatufanya tusishtuke kumwona suspataa wetu CR-SABA kutofunga.

Kwakuwa tunajua anatengeneza mabao kwa wengine ili kumpunguzia majukumu. Amekuwa akitumia sehemu kidogo ya nguvu zake ili kuwapa nafasi wengine. Tunafunga kutoka kila upande. Viungo watapiga mashuti. James, Bale na CR-SABA watapiga faulo. Yaani timu hii imefanywa kuwa mabao ni jukumu la wote kuyafunga.

Haina maana kwamba akikosa Ronaldo basi timu iwe inaugua kipindupindu. Haina maana kwamba Benzema akiwa na siku mbaya basi isababishe timu iugue kipindupindu. Hatutaki na hatupendi kuyaona hayo. Tunachotaka ni kuona timu inatupia tu.

Timu inawafunga na tutamfunga yeyote aliye mbele yetu. Si mechi nyingine tu, hata ya Desemba 3 dhidi ya Barcelona tutafunga mabao kutoka kwa kila mmoja. Hatutaki kutabirika nani atatupia mabao kwani kila mmoja anao uwezo wa kufunga pale anapopangwa. Na hilo tutachuana nalo tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -