Sunday, November 29, 2020

WAJUE WABABE WA ‘DERBY’ YA SIMBA, AZAM FC

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

MASHABIKI wa soka hapa nchini leo watalazimika kusahau kwa muda shughuli zao nyingine na kuhamishia akili zao kwenye Uwanja wa  Taifa jijini Dar es Salaam ambako inatarajiwa kupigwa mechi kati ya Azam FC dhidi ya Simba.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na sababu kubwa mbili, kwanza kabisa kila moja itataka kuibuka na ushindi ili kuvuna pointi tatu na kujiimarisha katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Sababu ya pili, Simba itataka kutumia fursa hiyo kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Azam katika mchezo wa fainali za Kombe la Mapinduzi lililofanyika hivi karibuni mjini Unguja na wakati huo huo Azam wakikusudia kuendeleza ubabe wao.

Rekodi zinaonyesha kabla ya mchezo wa leo  timu hizo zimeshakutana mara 17 katika mechi za  Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mechi hizo 17 ambazo timu hizo zimekutana, Simba imeinyanyasa Azam mara nyingi zaidi ikiibuka na ushindi mara nane, wakati Azam imeshinda mara nne, huku mara tano zikitoka sare, ambapo jumla ya mabao 42 yaliwekwa kimiani.

Kuelekea mtangane huo, BINGWA linakupa orodha ya wachezaji waliowahi kutikisa nyavu kwenye mechi  zilizozikutanisha Azam na Simba.

John Bocco

Ni straika na nahodha wa kikosi cha Azam aliyeitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu.

Ndiye mchezaji anayeongoza kufunga mabao mengi katika mechi baina ya Azam na Simba.

Hadi sasa Bocco amepachika wavuni mabao saba katika mechi dhidi ya Simba.

Anapewa nafasi kubwa ya kuendelea kulichungulia lango la Wanamsimbazi kutokana na umahiri wake wa kutumia nafasi vizuri.

Bocco aliifunga Simba kwa mara ya kwanza Januari 23, 2011, alipofunga mabao mawili, Azam ikishinda mabao 3-2, kabla ya kufunga la tatu Oktoba 27, 2012 Azam ilipofungwa mabao 3-1, huku 2013/14 akifunga bao la nne.

Desemba 12, 2015 alifunga mabao mawili, Azam ikitoka sare ya bao 2-2 na kufanya idadi  ya  mabao saba aliyofunga mpaka sasa.

Emmanuel Okwi

Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya hivi karibuni kuvunja mkataba wake na klabu ya Sonderjyske ya Denmark.

Ndiye mchezaji anayefuata kwa kufunga mabao mengi katika mchezo baina ya Azam na Simba akiwa amezamisha wavuni matano.

Katika mchezo wa leo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba aliyopata kuichezea kabla ya kutimkia Sonderjyske.

Kwa mara ya kwanza kuifunga Azam ilikuwa  Februari 11, 2012, msimu wa 2011/12 ,Okwi alifunga mabao mawili na Simba kuibuka na ushindi wa mabao  2-0 dhidi ya Azam.

Oktoba 27, 2012, Mganda huyo alimchungulia tena kipa wa Azam, Mwadini Ally Mwadini, baada ya kufunga mabao mawili kabla ya kufunga bao moja 2014/15 na kutimiza idadi ya mabao matano pale timu hizo zilipotoka sare ya 1-1.

Kipre Tchetche

Staa huyu wa zamani wa Azam hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo, kwani kwa sasa anacheza soka ya kulipwa barani Asia.

Kabla ya kuihama Azam FC straika huyu raia wa Ivory Coast alikuwa ameifungia timu hiyo mabao manne katika mechi dhidi ya Simba.

Kipre alianza kuzitikisa nyavu za Simba Aprili 14 msimu wa 2012/13, baada ya  kufunga bao moja katika sare ya mabao 2-2.

Tchetche aliendelea kuitesa Simba baada ya kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi Azam wa mabao 2-1 hiyo ilikuwa msimu wa 2013/14.

Tchetche alikamilisha idadi ya mabao manne Januari 25, msimu wa 2014/15 alipofunga bao moja kwenye matokeo ya sare ya 1-1.

Ramadhan Singano

Kitu kinachomtofautisha na wachezaji wengine niliowataja hapo juu ni kwamba, amezitumikia timu zote mbili (Simba na Azam) kwa nyakati tofauti.

Singano ambaye kwa sasa anakipiga Azam ana mabao manne aliyofunga akiwa na Simba katika mechi dhidi ya Wana lambalamba hao.

Singano alianza kuonja raha ya bao katika mechi baina ya timu hizo msimu wa 2012/13, baada ya kufunga mabao mawili huku Simba ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam.

Aprili 14, 2013 ukiwa  msimu wa 2013/14,Singano  aliifungia Simba bao pekee pale  iliapochapwa mabao 2-1 na Azam kabla  kufunga bao lake la nne msimu wa 2014/15  pale Simba iliposhinda mabao  2-1, hiyo ilikuwa  Mei 3, 2015.

Ibrahim Ajib

Inaelezwa kuwa hana muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na kukataa kuongezewa mkataba mpya, lakini  katika michezo aliyoichezea hadi sasa ameweza kufunga mabao matatu.

Ajib alianza kuifunga Azam Mei 3, 2015 ukiwa ni msimu wa 2014/15,  pale Simba iliposhinda mabao 2-1kabla ya kuiumiza tena Desemba 12, 2015 pale alipachika mabao mawili  kwenye sare ya 2-2.

Mussa Hassan Mgosi

Ndiye anayekamilisha idadi ya wanasoka waliofunga mabao si chini ya matatu katika mechi baina ya Simba na Azam.

Kwa sasa Mgosi amepewa jukumu la umeneja ndani ya Simba alichokichezea kwa mafanikio makubwa.

Mgosi aliyekuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji, alianza kuwaadhibu Azam katika mchezo wa Oktoba 24 msimu wa 2009/10 alipofunga bao la pekee na timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0, aliendeleza wimbi la kuziona nyavu za Azam msimu uliofuata kwa kufunga 1-0 Simba ikimaliza kwa kuwa mbele kwa 2-1 kabla ya kuhitimisha la tatu Januari 23, 2011, ingawa hapa Simba ilifungwa 3-2.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -