Wednesday, October 28, 2020

WAKALI GOFU WAPANIA UBINGWA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SHARIFA MMASI

WACHEZAJI mbalimbali wa gofu nchini, wameonekana kupania kuibuka mabingwa katika mashindano ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Lugalo.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika kwa siku tatu kumpata bingwa wa mwaka, yanatarajiwa kuanza Februari 17 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa viwanja vilivyoonekana kugubikwa na wachezaji wengi asubuhi na jioni ni Uwanja wa Jeshi Lugalo na ule wa Gymkhana.

Wachezaji walioonekana kutokwa jasho mazoezini ni pamoja na Angel Eaton wa klabu ya Lugalo, aliyedai kupania kuibuka bingwa katika mashindano hayo ili aipe sifa klabu yake.

“Nafanya mazoezi ya nguvu kila siku kujihakikishia ubingwa katika mashindano yaliyopo mbele yetu, pia ushindi nitakaopata utasaidia kuitangaza klabu yangu tofauti na mchezaji wa timu nyingine,” alisema.

Kwa upande wa mchezaji tegemeo wa Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam, Amini Said, anayechezea kiwango cha juu (Hand Caps), alisema mpaka sasa yuko katika hali nzuri ya kiushindani.

“Hali yangu kiafya ni nzuri naendelea na mazoezi tayari kwa mashindano, naamini hii ni vita kubwa mbele yetu kutokana na kila mchezaji kutaka kuibuka bingwa ingawa ushindi mwaka huu unarudi   Gymkhana,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -