Friday, December 4, 2020

WAKIFANYA KWELI LEO… NIYONZIMA, CHIRWA, MSUVA KUOGA NOTI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

WAKATI Yanga ikishuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuivaa MC Alger ya Algeria leo, macho na masikio ya wapenzi wa timu hiyo yataelekezwa kwa wakali wao, Haruna Niyonzima, Obrey Chirwa, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Vincent Bossou, Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na wengineo kuona iwapo wataamua kufanya kweli ili kuwafuta machozi au la.

Hakuna ubishi kuwa Yanga ina wachezaji wenye kila aina ya ubora wa kufanya lolote ndani ya dakika yoyote, japo tatizo limekuwa ni morali, kiasi kwamba wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kufanya kile kilichotarajiwa na wapenzi wao na mwisho wa siku kuigharimu timu yao.

Katika baadhi ya mechi za timu hiyo, iwe ni za Ligi Kuu Tanzania Bara au za kimataifa, pale ilipotarajiwa kushinda, wachezaji walishindwa kufanya kweli kutokana na ama kubweteka au kukosa morali.

Hilo lilijidhihirisha pia katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo pamoja na kupata bao la kuongoza mapema, wachezaji wa timu hiyo walijikuta wakibweteka na kuwaruhusu wapinzani wao hao kupata bao la ugenini lililowabeba na kusonga mbele baada ya suluhu kwenye mchezo wa marudiano wakiwa kwao.

Kwa hali kama hiyo, inadhihirisha kuwa iwapo wachezaji wa Yanga leo wataamua kufanya kweli, wanaweza kujikuta wakiwafanya mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo kujawa na furaha isiyo kifani na hivyo kuamua kuwamwagia noti vijana wao hao.

Kama ilivyo kawaida ya wapenzi wa klabu hizi kongwe za Simba na Yanga, timu zao zinapofanya vema, hujikuta wakipandwa na mzuka na kuwarushia noti kama sehemu ya kuwapongeza.

Mbali ya fedha, kuna wakati mashabiki wa Yanga waliwahi kumpa kiroba cha mchele Msuva, baada ya kukoshwa na kiwango chake.

Vile vile, wapo wachezaji waliowahi kupewa zawadi za magari, nyumba au kuongezewa mshahara baada ya kufanya mambo makubwa uwanjani kuzibeba timu zao.

Ni wazi kuwa, iwapo wachezaji wa Yanga watafanya kweli leo na kuiwezesha timu yao kupata ushindi mnono, haitashangaza kuona wapenzi wa timu hiyo wakiwamwagia noti mashujaa wao hao kama sehemu ya shukrani zao kwao.

Na kwa kuwa ‘mpira ni mabao’, mchezaji atakayefunga au kutoa pasi kali ya bao, hatatoka kapa Uwanja wa Taifa leo, lakini iwapo timu itashinda.

Miongoni mwa wachezaji watakaokuwa na nafasi ya kuoga noti leo ni winga hatari Msuva, mzee wa mapande Niyonzima, mkali wa kucheka na nyavu Chirwa na wengineo watakaofanya mambo adimu dhidi ya Waalgeria hao.

Akizungumzia mchezo huo wa leo, Niyonzima alisema kwa pamoja wameamua kuyasahau kwa muda matatizo yao ya kifedha ya kutolipwa mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu na kufanya kweli na kuwatoa Waarabu hao.

“Ni kweli tuna matatizo ya kifedha, lakini hayo hatuyapi nafasi, naomba wachezaji wenzangu kwanza tufanye kazi, unajua ukishaifanya kazi yako vizuri, hata bosi atakuwa na moyo wa kukulipa au kukupa chochote kitu,” alisema Niyonzima.

Aliongeza kuwa, Yanga ni klabu kubwa ambayo ina matajiri wengi wanaopenda kuona timu ikifanya vizuri na kusisitiza watacheza kufa au kupona kuhakikisha wanaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Alisema endapo watashinda mchezo huo na kuingia hatua ya makundi, wanaamini matajiri wengi watajitokeza kuwatunza fedha, lakini pia kumbuka ukiingia hatua ya makundi kuna mzigo tutapata, hivyo lazima tupigane kufa na kupona,” aliongeza Niyonzima.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, aliliambia BINGWA: “Sisi kama viongozi tumemaliza majukumu yetu ya ushindi kwa zaidi ya asilimia 90, kazi kubwa imebaki kwao wachezaji, nawaomba wacheze, wajitoe tushinde, mwisho wa siku kuna mambo mazuri zaidi yanakuja mbeleni kama walivyosema wao wenyewe,” aliongeza Mkwasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -