Thursday, October 29, 2020

Wakili kiboko anunua kesi ya Morrison

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

WAKALI aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na uwezo na rekodi yake ya kushinda kesi kubwa nchini, Alex Mgongolwa, amelivalia njuga suala la mchezaji Bernard Morrison dhidi ya Yanga, akiapa kula sahani moja na Mghana huyo.

Morrison amekuwa gumzo ndani ya siku chache zilizopita kutokana na sakala la kesi yake dhidi ya Yanga iliyokuwa mikononi mwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Morrison aliishtaki Yanga kwa kamati hiyo akipinga kuwa na mkataba mpya na Wanajangwani hao, baada ya ule wa awali wa miezi sita uliomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Wakati Yanga wakisisitiza kumwongeza mkataba wa miaka miwili Morrison ambao ungefikia tamati mwaka 2022, mchezaji huyo raia wa Ghana alikana hilo, huku akionekana akiwa anasaini kandarasi nyingine na Klabu ya Simba.

Na baada ya kesi hiyo kuendeshwa kwa siku tatu, hatimaye juzi Kamati hiyo ilitoa majibu kuwa mkataba mpya wa Morrison na Yanga ulikuwa na kasoro hivyo hautambuliki, ikimaanisha mchezaji huyo yupo huru.

Baada ya kupewa nakala ya hukumu hiyo, Yanga jana ilikutana na vyombo vya habari na kuanika msimamo wao juu ya sakata hilo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mgongolwa aliyekuwa mwanasheria wa TFF, alisema kuwa kimsingi Yanga imeonewa kwani kuna kila ushahidi unaoonyesha kuwa Morrison alisaini mkataba mpya Yanga.

“Shauri lililokuwapo mbele ya kamati ni kama mkataba wa Morrison uliongezwa ama hapana. Kisheria, vyombo vilivyopewa mamlaka ya kutoa haki ambavyo sio mahakama, vinatakiwa kujikita katika lile shauri lililopo mbele yake tu.

“Kilichotokea katika kamati, pande zote mbili ziliitwa kutoa ushahidi. Yanga ilitoa ushahidi ilivyopakua (upload) mkataba wa Morrison kutoka kwenye mfumo wa TMS na Yanga walieleza inahusiana na kuongeza mkataba wa Morrison,” alisema.

Alisema kuwa ushahidi mwingine uliotolewa na Yanga kwa kamati ni mkataba wenyewe uliosainiwa na Morrison na Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla kwa makubaliano ya mchezaji huyo kulipwa dau la usajili la Dola za Marekani 50,000 kwa miaka miwili, mwaka wa kwanza Dola 25,000 na mwaka wa pili Dola 25,000.

Alisema kuwa pia pande hizo mbili zilikubaliana Morrison kuongezwa mshahara kutoka Dola 2,500 hadi Dola 5,000 na kwamba Yanga walionyesha risiti katika kamati na Morrison hakubisha hilo.

“Ushahidi mwingine ni mawasiliano mara baada ya kusaini ule mkataba, mchezaji alianza kuonyesha hisia za kutaka kuvunja mkataba ulioongezwa na alifanya hivyo kwa mawasiliano ya whatsapp na ulitolewa huo ujumbe wa whatsapp kuonyesha kuna hizo jitihada mchezaji alizifanya,” alisema.

Alisema kuwa kuna ushahidi mwingine ambao Yanga waliutoa wa Morrison kusikika akilalamika kurubuniwa na watu wa klabu fulani wakimtaka aende kuchezea hiyo yao, ikiwamo picha zilizoonyesha mchezaji huyo akisaini mkataba na Wanajangwani hao.

Alisema kwa upande wa Morrison, alijitetea kuwa picha zile alizokuwa akionekana akisaini mkataba Yanga, alikuwa akiigiza jambo ambalo Wakili Mgongolwa alisema hoja hiyo haina mashiko mbele ya sheria kwamba huwezi kufanya maigizo kwa kutia saini ukajipatia Dola 25,000 na baadaye Dola 5,000.

Alisema kwa kuwa hoja ni iwapo Morrison aliongeza mkataba au la, Yanga ndiyo walitakiwa kupewa ushindi juu ya shauri hilo kwani hata Kamati ya TFF ilikiri mkataba ulikuwapo ila ulikuwa na kasoro (mapungufu).

“Kamati ilipotambua tu kuwa kulikuwa na mkataba, ilitakiwa shauri hilo liishie hapo kwa kutambua kuwa yule aliyesema hakukuwa na mkataba ameshindwa,” alisema.

Alisema kutokana na uzoefu wake katika mambo ya kisheria, yeye na klabu ya Yanga wamefikia uamuzi wa kukata rufaa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).

Kwa upande wake, Dk. Msolla, alisema suala hilo hawawezi kulirudisha katika kamati za TFF kama walivyotakiwa, bali  wanakwenda moja kwa moja CAS.

Msolla alisema hawana imani na kamati za TFF kwa sababu kuna malalamiko yao kabla ya hilo hayajafanyiwa kazi.

“Kitendo cha kamati kushindwa kutoa uamuzi kwa siku tatu kwa jambo dogo la kutumia dakika, tunatilia shaka weledi na uwezo wa kamati ile, ina maana kuna vitu vingi nje ya taratibu.

“Sisi kama klabu jambo lile halijatufurahisha na tunahisi walikuwa wanapata shinikizo nje ya taaluma yao, lakini kingine tunailaumu TFF, huwezi kuunda kamati ya hadhi za wachezaji na ndani kuna kiongozi wa klabu,” alisema Msolla.

Alisema kuna mambo mengi wamepeleka yamekuwa hayafanyiwi kazi, hasa sauti ya Morrison aliyosema kuna watu wanamshawishi kujiunga na timu nyingine.

“Tulipeleka TFF tangu tarehe 15 Juni, hadi leo hilo shauri halijasikilizwa, hii inapunguza imani kwa wanachama wake,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -