Saturday, November 28, 2020

Walcot, tusubiri kuisoma kurasa ya mwisho kwenye kitabu chake

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ALLY KAMWE,

KAMA umepata bahati ya kuitazama Arsenal msimu huu, bila shaka utakuwa umegundua mambo mawili makubwa kutoka kwao.

Moja wamepata tiba ya kiungo mkabaji, pili na kubwa zaidi ni Theo Walcot aliyekuwa akisubiriwa tangu Agosti 2006 alipocheza pambano lake la kwanza pale Emirates, ameanza kuonekana.

Ndio, kwa miaka 10 mashabiki wa Arsenal wamekuwa kwenye ganzi kubwa wakisubiri kuona makubwa walioyaamini kwa Theo na wakayakosa.

Katika kipindi chote hicho masika kwa kiangazi, Walcot amefanikiwa kubeba mataji mawili tu ya Kombe la FA, zaidi ya hapo ni idadi kubwa ya ‘selfie’ alizopiga.

Hili lilikuwa jeraha kubwa kwa mashabiki wa Arsenal, kila walipomtazama Walcot hakika walikosa majibu ya kwanini anashindwa kukua kisoka.

Nani amesubiriwa kwa muda mrefu kama yeye pale England? Wayne Rooney alichukua miezi michache tu kuonyesha ubora wake, leo akielekea mwishoni ameshajitengenezea ufalme Old Trafford.

Lakini mtazame Walcot, wakati huu akionekana kuwa kwenye nyakati zake za mwisho ndio ameanza kuonyesha ukomavu wake kisoka. Nini kimekuchelewesha hivi Theo?

Zikumbuke fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006, kijana wa miaka 17 mwenye kasi, akili na tishio kwa mabeki alivyoishtua dunia kwa kujumuishwa kwenye kikosi cha England, hakika makubwa zaidi yalitarajiwa kutoka kwake.

Lakini akaanza kuufuata ukweli kwa kasi ya jongoo. Katika misimu yake minne ya kwanza ambayo Wenger alijipa ujasiri wa kumtumia Walcot alifunga mabao 18 kwenye michezo136.

Msimu wake bora zaidi ulikuwa ni 2012-13 alipofunga mabao 21 katika michezo yote aliyocheza, hapa akaleta faraja japo baadhi walishaanza kumkatia tamaa.

Lakini nini kilifuata kutoka pale? Akaanza kuandamwa na majeraha na baadaye kidogo jina lake likaingizwa katika orodha ya wachezaji walioshindwa kuipa mafanikio Arsenal tangu mwaka 2004 walipotwaa taji la mwisho la EPL.

Licha ya kushuka kiwango bado mashabiki wa Arsenal waliendelea kushikilia imani yao, akabaki kuwa Walcot mwenye kasi asiyekuwa na malengo.

Msimu uliopita rekodi yake kwa msimu ilisimama kwa kufunga mabao 9 kwenye michezo 42, kuna aliyeshtushwa na hili? Hakuna ila mshtuko mkubwa ulikuja alipotemwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki Euro 2016.

Lakini baada ya safari hiyo ndefu ya Theo, msimu huu kuna kitu tofauti kinaonekana kwenye uchezaji wake. Kwenye mechi nane alizocheza mpaka sasa amefunga mabao matano na kuasisti mawili.

“Naamini kuna mabadiliko makubwa yatakuja kwa Walcot,” alinukuliwa akisema Arsene Wenger mwanzoni mwa Septemba. “Yuko tayari kwa ajili ya kupambana na ana nguvu kubwa ya mashabiki nyuma yake, natarajia kuona mabadiliko.”

Kwa sasa ana miaka 27 na bila shaka Walcot atakuwa akifahamu ni namna gani anatakiwa kuzichanga tena karata zake, ni wakati wake wa kuutumia wakati kabla wakati haujamtumia.

Walcott anaonekana mwenye ari zaidi msimu huu, anashambulia na anatoa mchango mkubwa timu inaposhambuliwa.

Misimu michache iliyopita alikuwa akitumia asilimia 90 kwa ajili ya kushambulia, lakini hivi sasa ameweza kujiweka sawa, nusu anakaba nusu anashambulia.

Wengi tunatamani kuona Theo akiendelea na kasi hii na litakuwa jambo la kupendeza endapo akirudisha angalau nusu ya deni analodaiwa na mashabiki wa Arsenal kwa kufunga mabao mengi msimu huu.

Nani hapendi kuona Walcot akiwa bora? Bila shaka hakuna, kila mpenda soka anataka kuona vizuri kwa Theo, lakini mwenyewe yuko tayari kupambania hili? Kwa miaka yake 27, ataweza kugeuza kurasa ya pili ya simulizi yake?

Bado tuko katikati ya Oktoba, ni mapema kwa sasa kusherehekea kitu chochote kutoka kwa Walcot, tusubiri Mei mwakani kufahamu namna nyota huyu atakavyomaliza kurasa ya mwisho ya kitabu chake cha miaka 10 aliyokaa Arsenal.

Changamoto kubwa inayomkabili ni majeraha, kama akiwa fiti mpaka mwisho wa msimu huenda akatuachia simulizi nzuri, tumuombee kwa hilo.

Mashabiki wa soka wanasubiri kitu kutoka kwake, wahuni wa Emirates bado wanatamani kuimba jina lake, kazi imebaki kwake kuamua hatima yake kisoka.

Akipanga kushindwa atashindwa, akipanga kuweza ataweza, mwandishi wa kitabu cha miaka 10 aliyokaa Arsenal yupo kwenye hatua za mwisho kabisa, kazi kwake!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -