Friday, December 4, 2020

WALIACHWA NA CITY, WANGEWEZA KUWA MSAADA KWA GUARDIOLA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MANCHESTER, England

ILIKUWA wikiendi mbaya kwa kocha wa Man City, Pep Guardiola, baada ya timu yake kutandikwa bila huruma na mabingwa watetezi, Leicester City, jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa kwenye dimba la King Power usiku wa kuamkia jana.

Kichapo hicho kilikuwa ni cha pili mfululizo kufuatia kichapo kingine kikali cha mabao 3-1 kutoka kwa Chelsea wikiendi iliyopita.

Bila shaka, Guardiola kwa sasa atakuwa anaelewa namna ligi hiyo ilivyo ngumu na isiyotabirika kiurahisi kutokana na changamoto lukuki anazozipata.

City ni moja kati ya klabu zilizotumia fedha nyingi kusajili msimu huu, lakini bado anapungukiwa aina ya wachezaji ambao wangefaa zaidi kwenye mfumo wake wa kumiliki mpira na pasi fupi fupi na orodha hii ya wachezaji watano ambao waliachwa na klabu hiyo, wangemfaa zaidi Guardiola iwapo wangeendelea kukipiga ndani ya klabu hiyo hadi msimu huu.

Jerome Boateng (beki wa kati)

Alipokuwa akikitumikia kikosi cha City, Boateng alitabiriwa kuwa beki imara siku za usoni, lakini hakukuwa na kocha ambaye alionekana kutaka kukiimarisha kipaji chake.

Shukrani ziwaendee makocha hawa: Jupp Heynckes na hasa Guardiola mwenyewe, ambao walimnoa vilivyo Boateng ndani ya klabu ya Bayern Munich na kumfanya Mjerumani huyo kuwa mwamba imara.

Staa huyo ni wazi angeweza kuwa nguzo thabiti katika ukuta wa City msimu huu ambao umekuwa ukimtegemea zaidi John Stones.

Edin Džeko (straika)

Ni wazi Guardiola atakuwa anaumiza kichwa kuipata dawa ya kuongeza nguvu kwa mshambuliaji wake, Sergio Aguero, ambaye hawezi kuihimili presha ya kucheza kama straika pekee kwenye mfumo tangu kocha huyo alipotua mapema mwaka huu.

Edin Dzeko, anayekipiga kwenye klabu ya AS Roma kwa sasa, anaonekana kuwa ni straika sahihi kwa Guardiola. Hadi sasa, straika huyo ana jumla ya mabao na asisti 20 na kitu ambacho kinamvutia kocha huyo ni kuona straika akifunga mabao ya kutosha, hali kadhalika kusaidia mashambulizi kwa kutoa pasi za mabao.

Denis Suárez (kiungo wa kati)

Suarez ni zao la akademi ya Celta Vigo, ingawa wengi wanadhani kiungo huyo ni zao la La Masia ya Barcelona, kutokana na uwezo mzuri alionao wa kumiliki mpira na ubunifu wa pasi fupi fupi za uhakika.

Mhispania huyo, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Barcelona, iwapo angebaki City hadi sasa angeweza kuwa mbadala mzuri wa Ilkay Gundogan.

City wamekumbwa na janga la majeraha katika eneo hilo na kama kuna mchezaji mmoja kati ya hawa watano kwa ajili ya eneo la kiungo, bila shaka Suarez angekuwa ni chaguo sahihi kwa kipaji chake na ubunifu alionao.

Javi Garcia (beki wa kati, kiungo mkabaji)

Machaguo yaliyopo kwenye safu ya ulinzi ya City ni madhaifu mno, kwani baada ya John Stones na Nico Otamendil, mchezaji mwingine ambaye analazimika kuitumikia nafasi ya beki wa kati ni Aleksandar Kolarov, ambaye kiasili ni beki wa kushoto.

City iliwahi kuwa na Javi Garcia, kabla hawajamuuza. Mhispania huyo kwa sasa ni mwamba imara ndani ya klabu ya Zenit, aliyojiunga nayo mwaka 2014 akitokea City. Garcia angeweza kuwa beki imara wa kati wa Guardiola, sambamba na kusaidia majukumu ya kiungo mkabaji.

James Milner (beki wa pembeni, winga)

Milner aliichezea City jumla ya mechi 203 na aliuzwa mwaka mmoja kabla ya Guardiola hajatua ndani ya klabu hiyo.

Hembu fikiria kama Guardiola angethubutu kumwachia kiraka huyu asiyekubali kushindwa, mwenye mapafu ya mbwa. Milner angekuwa chaguo zuri la beki wa kulia na angempa Guardiola uhuru wa kuchagua walinzi wake wa kati bila kuvuruga mfumo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -