Tuesday, November 24, 2020

WALIOHUSIKA KUWACHEZESHA WACHEZAJI BILA VIBALI WASIACHWE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

GUMZO kubwa wiki hii katika mchezo wa soka, lilikuwa ni juu ya kukosekana kwa vibali kwa wachezaji wa kigeni waliosajiliwa kwenye klabu tatu kubwa  hapa nchini.

Suala hilo liliibuliwa na viongozi wa timu ya Ndanda FC baada ya kutoa malalamiko kwa kudai kuwa Simba wamewatumia wachezaji wa kigeni wasiokuwa na vibali katika mchezo wao wa kufungua pazia la duru ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baada ya jambo hilo kushika kasi, Idara ya Uhamiaji nchini waliamua kufuatilia  na kubaini kuwepo kwa waajiriwa katika klabu hizo ambao ni makocha na wachezaji wanaofanya kazi bila kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa kwa mgeni ili aweze kufanya kazi.

Kutokana na hilo kila klabu ilitakiwa kupeleka nyaraka zote zinazowahusu wachezaji wageni na makocha kwenye idara zinazohusika na vibali vya kuishi na kufanya kazi kwa wageni nchini ili kukaguliwa.

Wakati mchakato wa kukamilisha taratibu unaendelea, Idara ya Uhamiaji  ilizipiga marufuku klabu hizo, kuwatumia wachezaji na makocha hao hadi watakapokamilisha taratibu zote.

Ninachofahamu mgeni kuishi nchini kinyume cha sheria ni sawa na kosa la jinai na mtu akibainika anatakiwa kupelekwa mahakamani  ili hatua stahiki zichukuliwe.

Sasa kitendo cha wachezaji kufanya kazi kwenye klabu hizi bila vibali, wahusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua kama wanavyofanyiwa waajiriwa wengine wanapobainika kufanya kazi bila kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na nchi husika.

Sidhani kama kitendo hicho kingefanywa na kampuni au mtu mwingine wa kawaida angeachwa kirahisi hivyo bila hatua zozote kuchukuliwa kwa sababu hivi sasa tunasikia klabu hizo zikitamba kuwa tayari zimeshakamilisha taratibu.

Huwezi kukamilisha taratibu baada ya kushtuliwa kwani siku zote ulikuwa hujui kitu unachotakiwa kufanya? Kama Serikali imeamua kuvalia njuga kuhusu vibali vya kazi basi wale wanaobainika  kwenda kinyume wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine kwa sababu  kuendelea hivyo ni kulea matatizo yatakayoweza kuleta shida kwa vizazi vijavyo.

Ifahamike kuwa suala la kufuata sheria na taratibu za nchi ni jambo la lazima na ni la kila taasisi, kampuni au mtu binafsi.

Mfano mzuri tumeona mchezaji wa timu ya Azam FC, Farid Mussa, baada ya kupata nafasi ya kwenda kucheza soka Hispania lakini suala la vibali vya  kwenda kufanya kazi nchini humo lilikuwa gumu kupata kutokana na taratibu zake kuchukua muda mrefu.

Ilikuwa hawezi kuruhusiwa kuingia nchini humo bila kukamilika kwa upatikanaji wa vibali na ndiyo ikawa kikwazo kikubwa kwake hadi kuifanya safari yake kuchelewa.

Huu ni moja ya mfano lakini wapo wachezaji wengine wa Tanzania walipata bahati ya kucheza soka nje ya nchi ila taratibu za kule zikawashinda na hii ni kutokana na kuzoea mteremko hapa nchini.

Wachezaji hawa wanaweza wakawa mashahidi ya kuwa ni jinsi gani nchi za wenzetu wanazingatia na kufuata sheria bila kujali tabaka la mtu.

Ilifikia mahali wachezaji wengine wanapata  nafasi za kucheza soka la kulipwa nje lakini wanashindwa kudumu huko kwa kile wanachodai fedha wanayopata haitoshelezi kutokana na kuwepo kwa makato mengi ikiwamo kodi.

Pia zipo kesi nyingi zilizowakumba wachezaji wakubwa duniani  hadi kupandishwa kizimbani kwa makosa  mbalimbali ya kuvunja taratibu za nchi kama vile kutolipa kodi inavyotakiwa au kukiuka kanuni wakati wanasajiliwa na klabu zao.

Si klabu za Simba, Yanga Azam ndio zina wachezaji wa kigeni, inachotakiwa ni Shirikisho la Soka Tanzania kushirikiana na wizara kusika kuweka mambo sawa, naamini wapo wageni wengi wanaofanya kazi bila kuzingatia sheria.

Mambo haya yakizingatiwa, tutaona faida ya ujio wa wachezaji wa kigeni katika klabu zetu kwa kufaidika kimapato kuliko kile kinachoendelea kwa sasa ambapo Tanzania imekuwa sehemu rahisi kwa mchezaji wa kigeni kunufaika huku wachezaji wetu wakipata shida huko wanakokwenda kutafuta maisha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -