Friday, December 4, 2020

Waliong’ara na waliochemka Ligi ya Mabingwa Ulaya

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya kwanza ilihitimishwa juzi ambapo ilishuhudia miamba mbalimbali ikichuana kutafuta ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji hilo kubwa barani humo.

Katika mitanange hiyo ambayo ilipigwa mwanzoni na katika mwa wiki hii ipo miamba ambayo  ilifanya vizuri na huku mingine ikijikuta ikiangukia pua.
Hata hivyo, pamoja na miamba mingine  kutamba na mingine kushindwa, kuna iliyofanya vizuri zaidi na huku mingine ikivurunda.
Katika makala haya tutajaribu kuangalia kila timu na wachezaji ambao waliweza kung’ara katika mechi hizo zilizopigwa Jumanne na Jumatano.
WALIONG’ARA 

Katika mfululizo wa mechi hizo miamba mitatu Ulaya ambayo ni Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid ziliweza kufunga mabao 14 katika mechi zao, licha ya Real Madrid kuwa ndiyo timu pekee iliyopata ushindi mdogo.

Kwa ushindi huo unazifanya Bayern, Barcelona  na  Real Madrid kuweka rekodi ya kupata ushindi mara nyingi katika mechi  60  zilizocheza zikiwa nyumbani ambapo kati ya mechi hizo, timu hizo ziliweza kushinda mechi  56, zikatoka sare 3 na zikafungwa moja, ambayo ilikuwa ni kati ya Bayern Munich dhidi ya  Man City, mtanange uliopigwa mwaka  2013.

Katika mechi hizo timu hizo ziliweza kuvuna mabao 192 na kuruhusu 34.

Wachezaji  waliotamba

Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar

Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa  Barcelona kuwaanzisha wachezaji wote watatu katika msimu huu na kikatokea kile ambacho kilitarajiwa.

Katika mchezo huo, Messi  aliweza kufunga mabao matatu, huku akitoa pasi iliyozaa jingine, Suarez alitupia mawili na akatoa pasi moja, wakati Neymar alifunga moja na huku akipika mengine manne.

Tangu Suarez ajiunge na  Barcelona Julai 2014, yeye, Messi  na  Neymar  tayari wameshaziona nyavu mara  266  katika mashindano yote ambayo imeyacheza  Barcelona.

Leicester City

Pamoja na soka zuri ambalo huwa inalipiga, klabu  ya Club Bruges haikuizuia  Leicester City  kuondoka na ushindi  katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  na kumfanya kocha  Claudio Ranieri azidi kujidai.

Kabla ya mechi hiyo wengi walikuwa na hofu ya kwamba Leicester City pengine ingeweza kushindwa kutokana na kuwa ni ngeni katika michuano hiyo ya Ligi  ya Mabingwa, lakini katikati mwa wiki hali hiyo haikuwa hivyo na badala yake mabingwa hao wa Ligi Kuu England wakaweza kutembeza kichapo kwa  Bruges, wakiwa ugenini.

Kutokana na ushindi huo, inaelezwa kuwa kwa kuwa  FC Copenhagen  na Bruges  zitakwenda kuikabili  Leicester, ikiwa nyumbani  kocha Ranieri ana uhakika wa kuweza kuvuna walau pointi tisa katika hatua hiyo ya makundi na hivyo kumfanya abaki anahitaji pointi moja  ama mbili katika mechi mbili ambazo atakuwa ugenini akikabiliana na  FC Porto na  ile ambayo atakuwa nchini  Denmark.

Bayern Munich

Hadi sasa Bayern Munich imeweza kushinda mechi 13  za Ligi ya Mabingwa  ikiwa nyumbani na katika mechi hizo imeweza kufunga takribani mabao 48 na huku nyota wao, Robert Lewandowski akiwa ameziona nyavu  mara tisa katika mechi 10 alizocheza.

Atletico Madrid

Kikosi hicho cha kocha Diego Simeon kwa sasa ndicho kinachotajwa kuwa na ukuta imara ikilinganishwa na timu nyingine.

Kutajwa huko kuwa imara kunatokana na kwamba hadi sasa hakijaruhusu bao katika mechi nane kati ya 12  za Ligi ya Mabingwa.

Real Madrid

Kwa upande wa mabingwa hao watetezi, anayetajwa kung’ara katika mechi yao hiyo ya kwanza ni straika wao, Cristiano Ronaldo, ambaye aliifungia timu hiyo bao la kusawazisha kwa mpira wa adhabu na kuiwezesha kurejea katika mchezo.

Kwa mara ya mwisho Real Madrid kupoteza mechi yake ya Ligi ya Mabingwa ikiwa nyumbani ilikuwa ni mwaka 2009,  ilipochapwa na AC  Milan na ilikuwa inaonekana historia hiyo ingeweza kujirudia Jumatano wiki hii.

Hata hivyo, baada ya Ronaldo kupachika bao hilo mabao yakabadilika na hatimaye ikaweza kuondoka na ushindi.

Tangu ilipopata kichapo hicho kutoka kwa AC Milan ikiwa nyumbani, rekodi zinaonesha kuwa imecheza mechi 20, imeshinda 19, imetoka sare moja na haijawahi kufungwa na huku ikiwa imevuna mabao 66 na kuruhusu 11.

Lyon

Huu ulikuwa ni ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa nyumbani baada ya miaka saba.

Katika mchezo huo vinara hao waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya D. Zagreb, licha ya kutokuwa na nyota wao  Alexandre Lacazette ambaye ni majeruhi na siku hiyo nafasi yake ilichukuliwa na  kinda mwenye umri wa miaka 19,  Maxwel Cornet, ambaye alifanya bidii na kufanikiwa kuziona nyavu alipopachika bao la tatu.

Borussia Dortmund

Wakati vigogo hao wakizidi kutamba, Borussia Dortmund nao hawakuwa nyuma, kwani waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 wakiwa ugenini dhidi  ya timu ya Legia.

Ushindi huo unatajwa kuwa ni mwanzo mzuri kwa vigogo wa soka Ujerumani kutokana  na kuwa unawaweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele, licha ya kuwa huu ni mwanzo.

WALIOCHEMKA

Bayer Leverkusen

Timu hiyo iliendeleza rekodi mbaya ya kutoshinda katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya CSKA Moscow.

Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa timu hiyo imewahi kucheza mechi  94, ikashinda 36, imeshinda sare 19      sare 39 na katika michuano hiyo iliweza kupata mabao 133.

Sporting

Timu pekee ambazo zimewahi kuifunga  Real Madrid ikiwa kwenye uwanja wake wa  Bernabeu katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, ni  Barcelona na Atletico Madrid, lakini katika mechi za wiki hii  Sporting walikaribia kufanya hivyo baada ya kuongoza ndani ya dakika mbili za mtanange huo.

Hata hivyo, vijana hao wa kocha Jorge Jesus wakiwa tayari wameshaonekana kama wangeondoka na ushindi, lakini wakajikuta wakiporwa pointi zote tatu ndani ya muda wa majeruhi.

Legia Warsaw

Kipigo  cha mabao  6-0 walichokipta  Legia Warsaw  wakiwa nyumbani kinatajwa kuwa huenda ni mwanzo mbaya kwa timu hiyo.

Benfica

Klabu hii itakuwa inajuta kumpeleka kukipiga kwa mkopo staa wake, Anderson Talisca, katika klabu ya Besiktas.

Hii ni kutokana na kuwa ndiye aliyesababisha  timu hiyo kuambulia  sare katika mechi yao hiyo ya kwanza  ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na vinara hao  wa soka nchini Ureno kutokana na kwamba Talisca ndiye aliyewaumiza  kwa mpira wa adhabu dakika ya  93 ya mtanange huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -