Wednesday, October 28, 2020

WALIONGOZA UFUNGAJI HADI KRISMASI, WALIMALIZAJE MWISHO WA MSIMU?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KILA mdau wa soka anapenda kuona mabao yakitinga nyavuni. Na mashabiki wa Ligi Kuu England wangependa kuona Sikukuu ya Krismasi ikipendezeshwa kwa timu kufungana mabao ya kutosha. Raha ya mchezo bao bwana!

Hata hivyo, timu nyingi ndani ya ligi hiyo zinamkosa yule straika hatari mwenye uwezo mzuri wa kupachika mabao, licha ya nafasi lukuki zinazotengenezwa.

Mfano, klabu kama Southampton inakamata nafasi ya 15 kwa kutengeneza nafasi nyingi kati ya zile ligi tano kubwa za Ulaya (wastani wa nafasi 11.47 kwa mchezo) lakini kwenye suala la mabao ya kufunga kikosi hicho ni cha 72, kikiwa na wastani wa kufunga bao 1.00 kwa mchezo.

Hebu vuta picha wangekuwa na mshambuliaji kama Diego Costa. Mhispania anayeongoza kwa ufungaji pale England ndani ya klabu ya Chelsea msimu huu, bila huyu jamaa ni wazi tungeishuhudia Chelsea isiyo na makali kabisa kutokana na mabao yake yaliyoiwezesha timu hiyo kukalia kiti cha usukani wa ligi.

Lakini pia tujiulize swali, Costa ataendeleza balaa lake hilo? Au uchovu, majeraha na presha ya ligi itasimamisha kasi yake?

Kuliweka hili sawa, mtandao wa takwimu wa Squawka umechambua wafungaji bora wa miaka 10 iliyopita ya Ligi Kuu England ambao waliongoza kwa mabao hadi Krismasi na walimalizaje .
2006/07 – Didier Drogba

Hadi Krismasi:  10
Mwisho wa msimu: 20

Gwiji huyu wa klabu ya Chelsea alikuwa ni moto wa kuotea mbali miaka 10 iliyopita ambapo kiwango chake cha utupiaji mabao kilikaribia kumpatia kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, taji la tatu mfululizo la Ligi Kuu England.

Baada ya Krismasi hakumaliza na mabao mengi, lakini hayo hayo 10 na kunyakua kiatu cha dhahabu.

2007/08 – Fernando Torres

 Hadi Krismasi: 11
Mwisho wa msimu: 24

Alijulikana kwa jina la utani la ‘El Nino’ (kijana mdogo), mwaka huo ulikuwa wa kwake kwenye Ligi Kuu England ambapo hadi kufikia sikukuu alikuwa na mabao 11 kabla ya kuendeleza mengine 13 yaliyomfanya amalize msimu na mabao 24.

2007/08 – Cristiano Ronaldo

 Hadi Krismasi: 11
Mwisho wa msimu: 31

Mreno huyu alikuwa na moto kama aliokuwa nao kipindi hicho, lakini mabao yake hayo yaliipa nafasi nzuri Manchester United kunyakua taji la pili mfululizo la Ligi Kuu England.

2008/09 – Nicolas Anelka

 Hadi Krismasi: 14
Mwisho wa msimu: 19

Mfaransa huyu alikuwa na mwenendo mzuri wa ufungaji mabao ambapo hadi kufikia Krismasi msimu wa 2008/09, alifikisha mabao 14, lakini baada ya sikukuu alishindwa kuiendeleza kasi yake hiyo na akaishia kufunga mabao matano, akiisaidia Chelsea kumaliza msimamo ikiwa nafasi ya tatu, na kwa bahati nzuri alinyakua kiatu cha ufungaji bora.

2009/10 – Jermain Defoe

 Hadi Krismasi: 13
Mwisho wa msimu: 18

Hadi kufikia nusu ya msimu wa 2009/10, Chelsea ilikuwa inakimbia zaidi kulifuata taji la ligi, huku Defoe akiongoza kwa ufungaji mabao hadi kufikia Krismasi, lakini mabao matano tu yalifuatia baada ya sikukuu ambapo aliisaidia Spurs kukamata nafasi ya nne.

2011/12 – Robin van Persie

 Hadi Krismasi: 16
Mwisho wa msimu: 30

Hutokea mara chache kwa Ligi Kuu ya England kutokea mshambuliaji akawa na mwenendo bora wa ufungaji mabao, mmoja wa wachache hao alikuwa ni Robin van Persie msimu wa 2011/12.

Mabao 16 hadi Krismasi na mengine 14 baada ya sikukuu hiyo, yalimfanya Mholanzi huyo anyakue kiatu cha ufungaji bora huku akiibeba Arsenal hadi nafasi ya tatu.

2013/14 – Luis Suárez

 Hadi Krismasi: 19
Mwisho wa msimu: 31

Nguvu ya mpachika mabao huyu mwenye njaa kali ilikaribia kuwapa Liverpool taji, ambapo umuhimu wake kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo msimu wa 2013/14 ulionekana wazi kwa kupachika mabao 19 hadi kufikia kipindi cha sikukuu, huku akiongeza mengine 12 na kunyakua kiatu cha ufungaji bora.

2014/15 – Sergio Aguero

 Hadi Krismasi: 14
Mwisho wa msimu: 26

Huyu ni mshambuliaji hatari aliyedumu England kwa kipindi kirefu, lakini msimu wa 2014/15 ndani ya klabu ya Manchester City aliisaidia timu yake hiyo kuwapa changamoto mabingwa halisi msimu huo, Chelsea.

Baada ya kuweka nyavuni mabao 14 hadi Krismasi, Aguero aliendeleza ukali wake kwa kupachika mengine 12 hadi alipofanikiwa kunyakua kiatu cha dhahabu.

2015/16 – Jamie Vardy

 Hadi Krismasi: 15
Mwisho wa msimu: 24

Kasi aliyokuwa nayo Jamie Vardy msimu uliopita haikuwa nzuri kwa afya ya mabeki wa timu pinzani.

Hadi kufikia kipindi cha sikukuu, jamaa alipiga mabao 15, lakini baada ya Krismasi alifunga mabao tisa tu baada ya presha kuwazidi, lakini aliibuka Riyad Mahrez na kubeba mzigo huo hadi Leicester iliponyakua taji lake la kwanza la Ligi Kuu England.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -