Friday, October 23, 2020

WAMEANZA UPYAAA!: KAGERE ANG’ARA SIMBA WAKIIPIGA PRISONS 1-0 U/TAIFA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA WINFRIDA MTOI                 |                   


 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wameanza vyema harakati zao za kutetea taji lao la ligi hiyo kwa kukusanya pointi tatu muhimu katika mchezo wa fungua dimba dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwas na mshambuliaji wao mpya waliyemsajili msimu huu kutoka Gor Mahia, Meddie Kagere katika dakika ya pili ya mchezo huo ambao ulianza kwa kasi tofauti na walipocheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Simba ilipata bao hilo baada ya Kagere kutumia vizuri pasi ya kisigino aliyogongewa na nahodha wake John Bocco na kupiga mkwaju mkali akiwa nje kidogo ya eneo la 18.

Mchezo huo uliendelea kwa kasi na dakika ya 12 mwamuzi Hance Mabena kutoka Tanga alimwonyesha kadi ya njano beki wa Tanzania Prisons, Benjamini Asukile kwa kumchezea vibaya kiungo Hassan Dilunga.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -