Wednesday, October 28, 2020

YANGA VS SIMBA ;WAMEJILETA WENYEWE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

HAKUNA namna. Watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga, mwaka huu watacheza mapambano matatu.

Mechi ya kwanza ya watani hao ni hii ya kesho ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi wakati mechi ya pili itakuwa ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2016/17 na ya tatu itakuwa ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18.

Hali hiyo imetokana na ukweli kwamba, Simba jana ilifanikiwa kuongoza Kundi A kwa kufikisha pointi 10 ikishinda michezo mitatu na kutoka sare mmoja huku Yanga ikishika nafasi ya pili katika Kundi B kutokana na pointi sita, wakishinda michezo miwili na kufungwa mmoja.

Hata hivyo, timu hizo zimekutana mapema kabla ya mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopangwa kufanyika Februari 17 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umewahi sana kuja kumaliza ubishi baina ya mahasimu hao ambao katika mechi yao ya Oktoba mosi mwaka jana timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na kuibua vurumai kubwa zilizosababisha uharibufu wa mali kwenye Uwanja wa Taifa.

Tangu sare hiyo timu hizo zimekuwa katika mvutano mkali na tambo za kila mmoja kujiona ni timu bora jambo ambalo sasa linaweza kumalizwa katika mchezo wa kesho ambao kwa namna yoyote hautakuwa na sare kwa kuwa lazima timu moja ishinde hata kwa mikwaju ya penalti

Katika mchezo wa jana, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys, kwenye Uwanja wa Amaan na kumaliza wakiwa ni vinara wa kundi hilo.

Mabao yote mawili ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wao, Laudit Mavugo, ambaye alionekana kuwachachafya vilivyo mabeki wa Jang’ombe Boys.

Mavugo alifunga bao la kwanza dakika ya 17 akimalizia mpira uliogonga nguzo na kurudi uwanjani kufuatia shuti la Shiza Ramadhan ‘Kichuya’, aliyepokea pasi nzuri ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Juma Luizio.

Baadaye, Simba waliendelea kufanya mashambulizi ambapo dakika ya 15, Kichuya alikosa bao la wazi kufuatia shuti lake kuondolewa na kipa wa Jang’ombe Boys, Hashim Ruga.

Simba walifanya shambulizi lingine dakika ya 17, lakini Mzamiru Yassin, alishindwa baada ya kupiga shuti kali  ambalo liliokolewa na kipa Ruga na kuwa kona tasa.
Jang’ombe Boys licha ya kutafuta bao la kusawazisha, lakini walijikuta wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.

Simba walifanya mabadiliko dakika ya 49 kwa kocha wa timu hiyo, Joseph Omog, kumtoa Mzamiru na nafasi yake kuchukuliwa na James Kotei ambayo yalionekana kuwa na manufaa kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Mavugo alifunga bao la pili dakika ya 53 kwa shuti kali baada ya kupenyezewa pasi na Kichuya na kumkokota beki wa Jang’ombe Boys hadi eneo la 18 na kufunga.

Simba: Peter Manyika, Janvier Bokungu/Vincent Costa (dk 78), Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjale, Jonas Mkude, Shiza Ramadhan ‘Kichuya’/Hija Ugando (dk.71), Muzamiru Yassin/James Kotei (dk.46), Pastory Athanas, Laudit Mavugo/Jamal Mnayte (dk.55) na Juma Luizio/Moses Kitundu (dk.63).
Jang’ombe Boys:  Hashim Ruga, Shomary Ismail, Muharami Issa, Ibrahim Said/Abubakar Ali (dk.72), Ali Badru, Yakoub Omar, Abdi Kassim, Khamis Makame, Hafidh Juma, Juma Ali/Ali Suleiman (dk.67) na Abdulsamad Ali.

Fainali ya michuano hiyo inatarajia kupigwa Januari 12 mwaka huu, siku ambayo ni kilele cha kusherehekea Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -