Saturday, January 16, 2021

WANACHAMA WA YANGA ARUSHA KUKUTANA LEO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA JACKLINE LAIZER, ARUSHA

WANACHAMA, wakereketwa, wadau na wapenzi wa timu ya Yanga wa mkoani Arusha, wanatarajiwa kukutana leo kujadili na kupanga mikakati ya kuimarisha tawi la klabu hiyo mkoani hapa.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Anex Hotel ambapo utakutanisha Wana-Yanga mbalimbali kutoka katika kila Wilaya ya Mkoa wa Arusha.

Akizungumza mjini hapa jana, Katibu wa tawi hilo mkoani hapa, Dietrich Kateule, alisema wamefikia hatua ya kukutana baada ya kuona umuhimu wa kuisaidia timu yao iweze kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kateule alisema Yanga ina wapenzi wengi mkoani hapa, hivyo kama wataweza kuimarisha tawi kwa kila mwanachama kuwa na kadi na kulipa ada ya uanachama, wana nafasi kubwa ya kuisaidia timu yao katika mambo mbalimbali.

Alisema katika mkutano huo, watahakikisha wanahamasishana wanachama kulipia kadi zao kila mwezi na wale wasio na kadi kujiunga rasmi ili waweze kutambulika na kuwa wanachama hai.

Alisema hoja nyingine zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuandaa siku maalumu ya kumkaribisha Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Athuman Kihamia, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

“Nawaomba wapenzi wa Yanga wafike kwa wingi ili tuweze kuweka na kupanga mikakati kabambe ya kuweza kuisaidia timu yetu hata kwa mawazo na kutambuana wenyewe kwa wenyewe kwani tukiwa wamoja lazima kila kitu kitakwenda sawa,” alisema Kateule.

Kateule alisema wapenzi wa Yanga wapo wengi mkoani hapa ila tatizo ni kutojuana ila kupitia mkutano huo utawapa fursa wadau wote kukaa pamoja na kujuana, huku wakipanga mikakati kabambe ya kuiwezesha timu yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -