Monday, November 23, 2020

WANAFUNZI WENYE VIPAJI ‘KUTIA TIMU’ LORD BADEN JUMAMOSI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

WANAFUNZI wenye vipaji katika mchezo wa soka, riadha na mpira wa kikapu, wanatarajiwa kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Lord Baden Memorial iliyopo Bagamoyo, mkoani Pwani tayari kwa majaribio ya kupata udhamini wa masomo shuleni hapo.

Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa mpango huo, Michael Maurus, alisema kuwa wanafunzi walioomba nafasi hiyo kupitia fomu zilizotolewa kwenye magazeti ya BINGWA na DIMBA, wanatakiwa kuwasili ofisi za New Habari (2006) Limited zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam, Jumamosi ya Desemba 31, kuanzia saa 10:00 hadi 11:00 jioni tayari kwa safari ya Lord Baden.

Alisema wanafunzi hao watakaa shuleni hapo kwa siku tatu wakinolewa na kushindanishwa ili kupata wale wenye vipaji vya hali ya juu ambao watapata udhamini wa masomo kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Lord Baden Sekondari, Kanali mstaafu, Iddi Kipingu pamoja na wadau wengine.

Alisema wamewaalika makocha wa timu za vijana wa Yanga, Simba na timu ya Taifa pamoja na wadau wengine ili waweze kuwachagua vijana ambao mwisho wa siku watawasomesha na kuwaendeleza kimichezo na klabu zao.

“Kwa wale ambao wameshawasiliana na mratibu wa mpango huu, wawalete watoto wao ofisi za New Habari zilizopo Sinza Kijiweni, siku iliyotajwa na wale wa mikoani, watasubiriwa katika stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Ubungo,” alisema.

Maurus aliwataka wazazi wote ambao watoto wao walijaza fomu hizo kuwasiliana naye kupitia namba ya simu 0713 556022/0783 324232 au kufika ofisi za New Habari kwa ufafanuzi na taratibu zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -