Wednesday, October 28, 2020

WANAKUJA Mmoja kati ya hawa kuchukua nafasi ya Lopetegui Madrid

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

KILA kukicha mambo yanaonekana kwenda ndivyo sivyo kwa Kocha wa Real Madrid, Julien Lopetegui, ambaye amerithi mikoba ya Zinedine Zidane aliyeikacha msimu uliopita baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara tatu mfululizo.

Lakini tangu Lopetegui atangazwe kuwa kocha wa timu hiyo yenye mataji mengi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameshindwa kufanya vizuri kama vile ilivyotegemewa na mashabiki wa klabu hiyo.

Katika michezo mitano waliyocheza hivi karibuni, Real Madrid hawajafanikiwa kushinda mchezo hata mmoja, yaani wamefungwa minne na kutoa sare moja, huku wakifunga bao moja tu kwenye michezo hiyo.

Walifungwa mabao 3-0 na Sevilla, kisha wakatoa suluhu na Atletico Madrid, CSKA Moscow waliwapiga bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Alaves wakiweka pointi tatu mfukoni kwa kuichapa bao 1-0 kabla ya kukubali kipigo kingine cha mabao 2-1 kutoka kwa Levante.

Taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa Lopetegui yupo katika kuti kavu kwa kupoteza kibarua chake ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa Ulaya.

Huku tayari makocha kadhaa wakihusishwa kuchukua nafasi yake kama akitimuliwa katika viunga hivyo vya Santiago Bernabeu.

Makala haya yanakuletea makocha watatu ambao wanapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Lopetegui endapo akifukuzwa muda wowote kuanza sasa.

MAURICIO POCHETTINO

Pochettino ni kocha ambaye Real Madrid walimtolea macho na kumfuatilia kabla ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Tottenham kwa muda mrefu zaidi.

Kocha huyo mwenye miaka 46 alifuatiliwa kwa ukaribu zaidi na vigogo wa Real Madrid, ambao walikuwa tayari kumkabidhi mikoba ya Zidane lakini kwa mambo yanayoendelea ndani ya timu hiyo wanaweza kumrudia kwa mara nyingine.

Bado hajafanikiwa kushinda taji lolote akiwa na timu yake, lakini amekuwa mmoja wa makocha bora Ulaya kwa sasa kutokana na kile anachokifanya Tottenham.

Kama kweli Real Madrid wanahitaji saini ya kocha huyo itabidi wavunje mkataba wake aliosaini na Tottenham mwanzoni mwa msimu huu ambao unatarajiwa kumalizika mwaka 2023.

Huku ikitambuliwa kuwa katika mkataba huo, kuna kipengele cha kumruhusu kuondoka kama kuna timu ikimhitaji.

Kwa hali inavyoendelea ndani ya Real Madrid kuna uwezekano wakahitaji saini ya kocha huyo wa zamani wa Espanyol na Southampton.

ARSENE WENGER

Wenger hivi sasa yupo nje ya soka baada ya kuondoka Arsenal aliyoitumikia kwa miaka 22 na kuwapa mafanikio kadhaa kwa kipindi chote alichokuwa na kikosi hicho.

Wiki iliyopita Wenger alitoa ujumbe kuwa Januari atarudi kufundisha kwa mara nyingine lakini hakuweka wazi ni klabu gani ataifundisha.

Lakini kwa hali inayoendelea pale Santiago Bernabeu, inaweza kuwafanya kumfikiria kocha huyo wa zamani wa Arsenal na Monaco huku ikikumbukwa miaka ya nyuma aliwahi kupokea ofa ya kuifundisha Real Madrid.

Wenger alikataa ofa zote za Real Madrid na kuamua kubaki na Arsenal, kwa umri wake wa miaka 69 ni kocha mzoefu mwenye kujua kipi cha kufanya huku akisifika kwa kutumia bajeti ndogo ya usajili.

ANTONIO CONTE

Baada ya kuvuna mafanikio akiwa na Chelsea hivi karibuni, Antonio Conte, ameingia kwenye orodha ya makocha wanaohitajika na Real Madrid kama wakimtimua Lopetegui wa sasa.

Alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England na Kombe la FA kwa misimu miwili aliyokuwa na kikosi cha Chelsea, huku akifahamika zaidi alipowapa Juventus mataji matatu ya Ligi Kuu Italia na Copa Italia.

Lakini taarifa zilizopo zinadai kuwa Real Mdrid wameanza maongezi na Conte ya kurithi mikoba ya Lopetegui ambaye anaonekana kushindwa ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa Ulaya.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -