Tuesday, November 24, 2020

Wanamuziki waliowahi kutoka na wanenguaji wao

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NEW YORK, Marekani

NI kama hadithi vile, msanii wa kike au wa kiume anaenda ziara katika nchi mbalimbali sambamba na wanenguaji wake na baada ya muda mfupi hujikuta akiwa karibu zaidi na ‘dansa’ mmojawapo.

Baada ya wiki kadhaa na hata baada ya miezi michache tu, zinaibuka habari kwamba staa huyo ameanzisha uhusiano na mmoja wa wanenguaji wake.

Hilo si jambo geni katika tasnia ya muziki lakini mara nyingi huja kwa kushtukiza. Makala haya yatakupatia orodha ya wasanii waliowahi kutoka kimapenzi na ‘madansa’ wao iwe mara moja au katika nyakati kadhaa.

Jennifer Lopez ‘J.Lo’

Kipindi hicho alichokuwa akitamba na wimbo wake wa ‘Jenny from the Block’, J.Lo alizama kwenye penzi la dansa, Cris Judd, mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Wawili hao waliamua kufunga ndoa mwaka 2001, lakini ndoa hiyo ilidumu hadi mwaka 2003 na J.Lo akaolewa na mwanamuziki, Marc Anthony, lakini kwa bahati mbaya akatengana tena na msanii huyo mwaka 2011.

Kwa mara nyingine tena, J.Lo akaingia kwenye uhusiano na dansa wake, Casper Smart ambapo uhusiano wao ulivunjika mapema mwaka huu baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Smart anachepuka.

Britney Spears

Mwaka 2003, Britney Spears alitamba mno na wimbo wake wa ‘Toxic’ na akajikuta akiingia kwenye uhusiano na dansa wake, Kevin Federline, ambapo walifunga ndoa mwaka 2004.

Wawili hao walifanikiwa kupata watoto wawili wa kiume, Jayden James Federline na Sean Preston Federline. Spears na Federline waliachana rasmi mwaka 2007.

LeAnn Rimes

Mwimbaji huyo wa muziki wa Country na Pop, kabla ya kuzama kwenye penzi zito na mumewe, Eddie Cibrian, aliolewa na dansa Dean Sheremet.

Rimes na Sheremet walikutana kwenye hafla ya tuzo za Country Music mwaka 2001 ambapo Sheremet aliteuliwa kuwa dansa wa mwanadada huyo wakati wa kutumbuiza.

Kwa mujibu wa Rimes, uhusiano wao ulitokana na mahaba yaliyowatawala tangu walipokutana hapo kwa mara ya kwanza na wakafunga ndoa mwaka uliofuatia kabla ya kuachana mwaka 2009.

Mel B

Kimwana huyo aliyewahi kuunda kundi la Spice Girls ambalo lilitesa mno miaka ya 1998, aliingia kwenye mahusiano na dansa, Jimmy Gulzar.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 1998 na kupata mtoto mmoja wa kike, Phoenix Gulzar, lakini ndoa yao hiyo haikudumu sana, kwani waliachana mwaka 2000.

  1. Kelly

Jina lake kamili, Robert Kelly. Akitamba na ngoma yake ya ‘Ignition’, R. Kelly alifunga pingu za maisha na dansa, Andrea Lee mwaka 1996 na ndoa yao ilidumu kwa muda wa miaka 13 ambapo waliachana mwaka 2009 baada ya mkali huyo wa masauti kukutwa na skendo ya kuwa na mahusiano na wasichana wadogo.

Ashley Tisdale

Tisdale alipata umaarufu mno na matamasha ya High School Musical, lakini pia aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na dansa, mchumba wake wa muda mrefu, Jared Murillo, kabla ya kuachana mwaka 2009.

Christina Aguilera

Mkali huyo wa mtindo wa Pop, Aguilera, alizama kwenye penzi zito na dansa Jorge Santos, ambaye alikutana naye kwenye ziara yake ya mwaka 2000.

Waliachana rasmi Septemba 2001, lakini waliendelea kufanya kazi pamoja hadi 2002.

Madonna

Mkongwe huyo wa muziki duniani, alikutana na dansa Brahim Zaibat katika hafla ya uzinduzi wa mavazi wa mwanawe.

Kitu kilichowaacha wadau na mshangao ni namna umri wa Madonna ulivyokuwa mkubwa kwa Zaibat, lakini kama Waswahili wanavyosema, penzi halichagui na wawili hao walishazama kwenye penzi lililodumu kwa muda wa miaka mitatu tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -