Monday, November 30, 2020

WANAOHUJUMU MASOKO YA MUZIKI TUWAITE WAHUJUMU UCHUMI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

HATUTEGEMEI tena shoo kama chanzo kikuu cha mapato kwa msanii anayefanya muziki, maonyesho yamebaki kuwa sehemu ya mwanamuziki kukutana na kuwaburudisha mashabiki, soko hasa la muziki limehamia kwenye mtandao, huko ndiko biashara ya muziki imepamba moto.

Masoko ya kimtandao yameingia kwenye ushindani, yanashindana kwa ubora wa huduma wanazozitoa kwa wasanii na mashabiki wao kitu kinachokwenda kuongeza thamani ya muziki wa kibongo.

Jambo jema zaidi ni pale ambapo masoko hayo yanabuniwa na vijana wa Tanzania na kufanya uzalendo utawale zaidi katika biashara hii inayofanyika ulimwenguni kote.

Wakati mwanzo tulitegemea mitandao kutoka nje ndiyo iuze kazi za wasanii wetu hivi sasa msanii hana shaka anapotoa kazi yake sababu akipeleka kwenye tovuti ya kitanzania inamuwia rahisi kufuatilia mapato yake. Mwaka huu umeendelea kuwa wa mapinduzi kwenye suala zima la teknolojia kwa njia ya mtandao upande wa burudani.

Kwa mara ya kwanza tovuti ya mkito.com ilianza kufanya biashara hii, wasanii walipeleka audio za nyimbo zao ili mashabiki wao wanunue kwa bei ambayo ilipangwa. Hakika wasanii wengi walinufaika na wanaendelea kunufaika kutokana na mashabiki wao kupakua hizo kazi.

Wiki tatu zilizopita Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Gabriel, alizindua tovuti ya Afro Premiere, soko jipya la wasanii kuuza na mashabiki kununua video za muziki.

Pia Ijumaa iliyopita msanii nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, naye amezindua tovuti yake ya wasafi.com ambayo lengo lake ni lile lile la kuuza muziki wa wasanii wa Tanzania na hata wale wa mataifa mengine.

Mfululizo wa vijana wa Tanzania kuwekeza kwenye teknolojia kwa lengo la kuupa thamani muziki wetu ili msanii anufaike na kazi zake hali kadhalika Serikali ipate kodi, ni ishara njema ya sanaa kutoa mchango wake kikamilifu kwenye pato la Taifa.

Katika uibukaji wa masoko haya kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zinayakumba masoko haya ya kimtandao kiasi kwamba fedha nyingi zinapotea. Unaweza kuona jinsi tovuti hizi zilivyo na mipango kabambe ya kuhakikisha Serikali inapata kodi na msanii ananufaika.

Sasa wanapoibuka watu wachache na kuanza kuhujumu mifumo hii kwa kupakua kazi za wasanii na kuzisambaza katika chaneli zao za YouTube, hakika inaumiza na inarudisha nyuma jitihada za kuikomboa sanaa hali kadhalika inapoteza mapato ya Serikali.

Nikupe mfano mdogo ambao umetokea wiki kadhaa zilizopita. Msanii Baghdad na Roma kupitia kolabo yao ya ‘K’ pamoja na G Nako akishirikiana na Jux kupitia wimbo wao wa ‘Go Low’, walitambulisha video zao kwenye tovuti ya Afro Premiere ili mashabiki waangalie kwa kununua.

Siku chache baada ya video hizo kuwekwa tovutini, likaibuka kundi la watu wa mitandao hasa blogas ambao walikwenda kupakua video zile na kuziweka kwenye tovuti zao ili maelfu ya mashabiki wazitazame bure. Hii ni mbaya sana.

Ndani ya wiki moja wasanii hao walikuwa wamepoteza shilingi milioni 30 kwa mtindo huo ambapo Serikali pia ilipoteza kodi zake. Maana kila shabiki anapolipia ili kununua kazi ya sanaa kuna asilimia kadhaa zinakwenda serikalini.

Sasa kwanini hawa wanaohujumu jitihada hizi tusiwaite wahujumu uchumi? Sanaa ni miongoni mwa sekta zinazokuja juu katika kuchangia mapato ya mataifa mengi duniani, iweje sisi tunakuwa na mifumo ya sanaa kutoa mchango wake kwenye pato la Taifa letu halafu wanaibuka watu wachache wanahujumu?

Lazima litazamwe hili, kwenye muziki kuna fedha na endapo tukadhibiti watu wanaohujumu masoko haya mapya ya muziki tunaweza kufika mbali kwa maana ya wasanii kunufaika hali hata Serikali kupata pato lake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -