Friday, December 4, 2020

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ASHA KIGUNDULA     

MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji wa nyota wa timu hiyo, Carlos Carlinhos na wengineo kama Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, wamepewa dili kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa leo kati ya Wanajangwani hao na Polisi Tanzania.

Mchezo huo wa raundi ya saba utakaoanza saa 10:00 jioni, utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema kuwa kikosi chao chini ya kocha mpya, Cedric Kaze, kipo tayari kucheza kandanda safi, hivyo ni jukumu la mashabiki na wapenzi wao kwa ujumla kuujaza uwanja.

Nugaz alisema kuwa kujitokeza kwa wingi kwa wapenzi wao katika mchezo huo, kutamfanya kocha huyo aone kuna ushirikiano mkubwa miongoni mwa Wanayanga.

“Kikosi chetu chini ya kocha wetu Cedric Kaze, kesho Alhamis (leo), kitakuwa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, tunaomba shabiki na mwanachama wa Yanga, kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Uhuru, tunaomba tujumuike nasi na tumuonyeshe kocha Kaze kama tumemkubali,” alisema Nugaz.

Alisema katika mchezo huo, viingilio vimewekwa vya kawaida ili kila mdau wa michezo na mwanayanga aweze kujitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo.

Alisema katika sehemu ya makujwaa ya mzunguko, kiingilio ni shilingi 5,000, jukwaa la VIP B shilingi 10,000 na VIP A ni shilingi 15,000.

Kwa upande wa kocha Kaze, ametoa ahadi kwa mashabiki wa Yanga kutarajiwa soka la pasi nyingi kama lile linalochezwa na Barcelona.

Alisema kuwa anahitaji Wanayanga kuona mabadiliko makubwa ya timu yao ambayo hivi karibuni itakuwa na kibarua kizito dhidi ya watani wao wa jadi, Simba katika mchezo uliopangwa kuchezwa Novemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Kaze amechukua nafasi ya Mserbia, Zlatko Krmpotic ambaye alitimuliwa na Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi tano za ligi, akishinda nne na kupata sare moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -