Monday, October 26, 2020

WANAOPANGA MATOKEO KWA AJILI YA ‘KUBET’ WAKAMATWA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MADRID, Hispania


JESHI la Polisi nchini Hispania limewakamata watu 34 wanaodaiwa kupanga matokeo ya mechi ya tenisi kwa ajili ya ‘kubet’.

Kati ya watu hao 34 waliokamatwa, ni pamoja na wachezaji tenisi sita na viongozi wawili wa uwanja, ambao wamedaiwa kupanga matokeo ya mechi katika michuano 17 na kupata mamilioni ya fedha.

Wizara hiyo ya mambo ya ndani haikutaja majina ya watu hao waliowakamata, lakini uchunguzi huo uliofanywa na polisi ulianza baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa taarifa ya rushwa kwa ajili ya kushinda katika ‘kubet’.

Taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa wizara hiyo ya mambo ya ndani, ilisema: “Operesheni maalumu ya polisi imekamata wataalamu wa mchezo wa tenisi waliokuwa wakifanya matendo ya rushwa.

“Operesheni hiyo imesaidia kukamatwa kwa watu 34, sita kati ya hao ni wachezaji wa tenisi. Wengine waliobakia kuna viongozi wawili wa shirikisho la mchezo huo.”

Mpango huo wa kuangalia masuala ya rushwa ulipangwa tangu Januari mwaka huu, baada ya watu wakubwa kwenye mchezo huo kuhusishwa na masuala ya rushwa.

Bodi ya mchezo huo wa tenisi umekubali kutoa ushirikiano kwa kila ambacho kitahitajika.

Mechi hizo za tenisi zilikuwa zikihudhuriwa na watu wengi wa ‘kubet’ kwa ajili ya kufanya masuala yao ya rushwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -