Wednesday, October 28, 2020

WANARUDI NYUMBANI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


Nyota hawa watakipiga dhidi ya timu zao za zamani Ulaya

BAADA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kupangwa hivi karibuni, kumeamsha hisia za wadau wa soka duniani kutokana na makundi hayo kuaminika kuwa yataleta changamoto kubwa msimu huu.

Wengi wameyabatiza baadhi ya makundi kuwa ya kifo kutokana na timu zilizopangwa kama Kundi B lenye Barcelona, Inter Milan, Tottenham na PSV, hata Kundi C lina PSG, Liverpool, Napoli na Belgrade lingine ni Kundi H walilopangwa Juventus, Manchester United, Valencia na Young Boys.

Kubwa linalovutia katika michezo hiyo ya makundi ni baadhi ya wachezaji kucheza dhidi ya klabu zao za zamani walizowahi kuchezea kabla ya kuondoka.

Makala haya yanakuletea wachezaji wanane wanaotarajiwa kucheza dhidi ya timu zao za zamani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

CRISTIANO RONALDO (JUVENTUS v MAN UNITED)

Baada ya makundi kupangwa kila mmoja alikuwa tayari anafahamu kuwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid atacheza dhidi ya Manchester United klabu ambayo ilimsajili kutoka Sporting Lisbon miaka 15 iliyopita.

Akifanikiwa kucheza michezo yote miwili dhidi ya Manchester United, atakamilisha mechi tano dhidi ya klabu hiyo iliyomfanya kuwa maarufu ulimwenguni.

Wakati yupo Real Mdrid alicheza michezo mitatu dhidi ya Manchester United na kufanikiwa kufunga mabao mawili, michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mmoja ulikuwa wa UEFA Super Cup.

PAUL POGBA (MAN UNITED v JUVENTUS)

Mwaka 2012, Juventus walimsajili Paul Pogba ambaye alikuwa huru kutoka Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson.

Wakati ule lilikuwa pigo kubwa sana kwa Manchester United huku miaka minne mbele walilipa dau la pauni milioni 89 kumsajili kiungo huyo aliyekulia katika akademi yao.

Pogba atakutana na Juventus akiwa na kibarua cha kuhakikisha hawaondoki na pointi yoyote katika michezo miwili watakayokutana katika Uwanja wa Old Trafford na Turin.

RADAMEL FALCAO (MONACO v ATLETICO MADRID)

Nyota huyo raia wa Colombia ni moja ya washambuliaji bora katika uso wa dunia akiwa na rekodi za kufunga mabao katika kila klabu aliyocheza.

Falcao atakuwa katika mtihani mkubwa wa kuhakikisha anaiangamiza timu yake ya zamani Atletico Madrid ambao watakipiga dhidi ya AS Monaco.

Nahodha huyo wa Monaco alijiunga na klabu hiyo ya Ufaransa akitokea Atletico Madrid ambayo aliitumikia kwa zaidi ya misimu mitatu.

EDINSON CAVANI (PSG v NAPOLI)

Wakati anakipiga katika klabu ya Napoli, Cavani, alijitambulisha kuwa mmoja wa washambuliaji moja katika Bara la Ulaya huku akipiga mabao zaidi ya 30 kwa misimu mitatu aliyokuwa hapo.

Jumla alifanikiwa kufunga mabao 104 katika michezo 138 aliyovaa jezi ya Napoli, baada ya miaka mitano kupita anarejea akiwa na umri wa miaka 31 huku akitarajiwa kuiongoza PSG dhidi ya Napoli.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timu zote zinaundwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa, Cavani atafanikiwa kuwafunga waajiri wake wa zamani? Muda bado upo, tusubiri.

THOMAS LEMAR (ATLETICO MADRID v MONACO)

Kwa misimu mitatu aliyokipiga AS Monaco, Lemar aliifanya dunia imtambue kuwa ni mchezaji wa aina gani huku akiziweka klabu mbalimbali katika wakati mgumu pindi zilipohitaji saini yake.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa, anatarajiwa kukutana na Monaco huku akiwa amevalia uzi wa Atletico Madrid katika michezo itakayopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano na Stade Louis II.

Lemar alifanikiwa kucheza michezo 127 na kufunga mabao 22 kwa misimu mitatu aliyoitumikia Monaco.

JUAN MATA (MAN UNITED v VALENCIA)

Moja ya viungo wenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mabao katika Ligi Kuu England ni Juan Mata anayekipiga Manchester United hivi sasa.

Mata alijiunga na United akitokea Chelsea lakini klabu hiyo ya London ilimsajili kiungo huyo katika timu ya Valencia huko nchini Hispania.

Katika Kundi H walilopangwa Manchester United, Mata anatarajia kukutana na Valencia ambayo aliitumikia kwa miaka minne na kufanikiwa kucheza michezo 129 huku akipachika mabao 33.

FERNANDINHO (MAN CITY v SHAKHTAR DONETSK)

Kiungo huyo raia wa Brazil aliitumikia Shakhtar Donetsk kuanzia mwaka 2005 hadi 2013 kwa kucheza michezo 284 na kufunga mabao 53.

Baada ya hapo, Fernandinho mwenye miaka 33 hivi sasa alijiunga na mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.

Lakini staa huyo wa Manchester City anatarajia kucheza dhidi ya Shakhtar Donetsk hivi karibuni licha ya kucheza dhidi ya klabu hiyo msimu uliopita katika michuano hiyo ya Ulaya.

PHILIPPE COUTINHO (BARCELONA v INTER MILAN)

Anatajwa kuwa mmoja wa viungo bora ulimwenguni kwa sasa akiwa anakipiga katika klabu ya Barcelona ambao walimsajili kutoka Liverpool.

Kubwa zaidi kwa mchezaji huyo wa Brazil anatarajiwa kucheza dhidi ya Inter Milan ambao aliitumikia kwa miaka mitano huku akicheza michezo 28 na kupachika mabao matatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -