Saturday, November 28, 2020

WANAUME NDIO WENYE VIPAJI VYA KUPENDA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Michael Maurus, 

KARIBUNI wapenzi wasomaji wangu katika safu hii ya mambo ya mahusiano ya kimapenzi ambayo huwajia kila Jumanne na Jumamosi ikilenga kujuzana hili au lile kuhusiano na malavidavi.

Kabla ya kutua kwenye mada ya leo, nitoe shukrani zangu za dhati kwa wasomaji wangu ambao wamekuwa wakichangia mada mbalimbali kwa namna moja ama nyingine.

Baada ya salamu hizo, nigeukie mada ya leo ambayo ni mwendelezo wa mada za Jumanne na Jumamosi wiki iliyopita.

Mada hiyo ilihusiana na suala zima la kupenda ikihoji kati ya wanawake na wanaume ni akina nani ambao wakipenda wamependa kweli?

Ndugu msomaji, katika matoleo yote mawili, nilijaribu kueleza kwa ufupi juu ya mabishano yaliyozagaa huko mitaani ambapo wanaume wamekuwa wakitamba kuwa wao ndio wenye mapenzi ya kweli huku wanawake nao wakifanya hivyo.

Mwisho wa siku, nilitoa nafasi kwa wasomaji kudadili hilo ambapo ilionekana wazi kila upande kuvutiwa kwao, wanawake wakitamba kuwa wao ndio wenye mapenzi ya dhati, huku wanaume nao wakijinasibu kubarikiwa kuwa na vipaji vya kupenda.

Katika toleo lililopita, niliahidi kuwaletea ukweli juu ya mada hiyo kutokana na tafiti zilizofanywa na wataalamu mbalimbali wa mambo ya mahusiano.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania State, Marissa Harrison, wanawake wamekuwa na tahadhari kubwa linapokuja suala la kupenda na wanaume wakiwa ni wepesi wa kupenda, huku wakipenda bara bara.

Katika tafiti alizozifanya, Harrison aliwauliza wanafunzi 172 wa chuo iwapo wameshawahi kujitosa kwenye mapenzi.

Iwapo aliyeulizwa angejibu ndio, aliulizwa ilichukua muda gani kusema “nakupenda.” Haikushangaza, wanaume walikiri kwamba walichukua muda mfupi mno kufanya hivyo kuliko wanawake, wakionyesha mapenzi yao ndani ya wiki chache tofauti na ilivyo kwa wanawake, ambao walichukua miezi kadhaa.

Lakini swali halisi linalotukabili ni: Kwanini? Kwanini wanaume wamekuwa wakiwapenda wanawake kwa haraka mno kuliko ilivyo kwa wanawake?

Kwa wanawake ambao wameshawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na kushuhudia nyakati za furaha na za kushangaza kutoka kwenye upweke hadi kuwa na mwenza, wanaelewa kwanini wanaume huwa wanapenda kwa haraka mno kuliko wanawake.

Moja ya sababu inayowafanya wanaume kuwa wepesi zaidi katika kuonyesha hisia zao za kimapenzi, ni kitendo cha kukabiliana na pilikapilika nguvu za kimaisha kiasi cha wakati mwingine kujikuta wakiwa wamechoka kiasi kwamba inapotokea hisia zake zimetua kwa mwanamke, huwa ni rahisi mno kuzidhihirisha ili kutuliza nafsi yake au kuupoza moyo wake.

Jambo jingine ni hulka iliyojengeka miongoni mwa wanaume kuwa ni watawala kiasi kwamba si kazi kubwa kwao kuwasilisha hisia zao, ambapo wanapofanikiwa kuwamiliki wale waliowapenda, huwa ni kazi kubwa kwao kuwapoteza kirahisi.

Sifa nyingine ya wanaume dhidi ya wanawake ni ile ya kutojiuliza mara mbili mbili juu ya hisia zilizopo mbele yake dhidi ya mwanamke. Hali hiyo huwasaidia kuwa na sauti mbele ya wapenzi wao, lakini pia wakiwa tayari kujishusha na kuonekana kama machizi ili mradi tu, kulilinda penzi lake.

Jambo jingine linalomtofautisha pande hizo mbili ni mtazamo wao ambapo wakati mwanamke akionekana kumhitaji zaidi mwanaume kwa ajili ya tendo la ngono, hali hiyo ni tofauti kabisa na ilivyo kwa wanaume.

Wanaume wao huwa na malengo mawili, kwanza ikiwa ni tendo la ngono kama sehemu ya kujiridhisha kimwili, wakati pia wakiwachukulia wanawake kama msaada wao pale wanapohitaji katika suala zima la kuyaendesha maisha.

Ndugu msomaji, kwa leo tuishie hapo, tukutane Jumamosi ambapo nitawaletea mada nyingine kali ambayo naamini mtaipenda.

Kwa wapenzi wa hadithi, kaa mkao wa kula kwani kuna hadithi kali ipo njiani inakuja inayokwenda kwa jina la Why You Betray Me (Kwanini Umenisaliti) mtunzi akiwa ni Gabriel Aliseni Tunda ambayeoni moto wa kuotea mbali nikiamini kila mmoja ataipenda.

Kama una maoni tuwasiliane kwa kupitia namba ya simu na anuani pepe hapo juu. Ahsanteni sana. 0713 556 022, michietz@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -