Tuesday, November 24, 2020

‘WANAUME’ SITA VING’ANG’ANIZI LIGI KUU BARA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SALMA MPELI

LIGI Kuu soka Tanzania Bara tunayoishuhudia imepitia katika vipindi tofauti na majina tofauti.

Ligi hiyo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Ligi ya Taifa mara tu baada ya kuanzishwa mwaka 1965 kabla ya kubadilishwa na kuitwa Ligi Daraja la Kwanza na baadaye mwaka 1997 kubadilishwa tena na kuitwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba na Yanga, ndizo timu kongwe zaidi katika ligi hiyo zikiwa zimefanikiwa kutwaa taji la ubingwa mara nyingi zaidi.

Yanga ndiyo inaongoza ikiwa imefanikiwa kutwaa taji hilo mara 25, huku Simba ikifanikiwa kulibeba mara 18. Timu hizi hazijawahi kushuka daraja tangu zilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965.

BINGWA kupitia makaya haya linakuletea orodha ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo tangu zilipofanikiwa kupanda daraja hazijawahi kushuka licha ya changamoto  kadhaa zilizowahi kukutana nazo.

Yanga SC

Yanga ndiyo timu kongwe zaidi nchini, ilianzishwa mwaka 1935. Ilipoanzishwa ilikuwa ikijulikana kama New Youngs, ilipofika mwaka 1936 baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walijiengua na kwenda kuanzisha timu nyingine iliyojulikana kama  Sunderland ambayo baadaye ilikuja kubadilishwa na kuitwa Simba ambayo wengi wetu tunaifahamu sasa ambayo ni mpinzani mkuu wa Yanga.
Wachezaji waliobaki waliamua kubadili jina na kuitwa Young Africans.

Tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 1965, Yanga haijawahi kushuka daraja.

Simba SC

Timu hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa Sunderland ilianzishwa mwaka 1936.

Timu hiyo ilianzishwa na wale baadhi ya waliojitenga kutoka New Young ambao wengi wao walikuwa wasomi ambao walisisitiza wanataka mambo yao yaendeshwe kisomi.

Waliungana na timu iliyokuwa inaitwa Eagle Night na katika miaka ya 1940 kabla ya kuibadilisha jina na kujiita Sunderland.

Hapo ndiyo chimbuko la kuvaa jezi za rangi nyekundu kama ilivyo kwa timu ya  Sunderland ya England lilipoanzia kabla ya mwaka 1971 kubadilishwa tena na kuamua kuiita Simba.

Simba imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara 18 na haijawaji kushuka tangu ilipoanzishwa na kuwa ni miongoni mwa timu zilizodumu.

Azam FC

Timu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara, Said Salim Bakhressa, ilipanda daraja na kuanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2007 ikiwa ni miaka mitatu tangu ilipoanzishwa na wafanyakazi wa viwanda vinavyomilikiwa na tajiri huyo mwaka 2004.

Kabla ya kubadilishwa jina na kuanza kutumia Azam FC, timu hiyo ilikuwa ikifahamika kama Mzizima FC.

Lengo la kuanzishwa kwa timu hiyo ni kuimarisha afya za wafanyakazi.

Tangu ilipofanikiwa kupanda daraja  timu hiyo imekuwa ikishiriki mfululizo Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali yakiwemo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Kagame na Kombe la Mapinduzi.

JKT Ruvu

Ni miongoni mwa timu zilizofanikiwa kulinda hadhi yake kwa kuhakikisha haishuki daraja tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Haijawahi kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini imekuwa ikifanya vizuri na mara kadhaa imemaliza msimu ikiwa kwenye nafasi tano za juu, ukiondoa misimu miwili iliyopita ambayo imeyumba.

Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutoka kikosi cha 832, ilianza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2002.

Kagera Sugar

Timu hiyo ilianzishwa katikati ya miaka ya 80 wakati huo ikiitwa RTC Kagera ikimilikiwa na kampuni ya biashara ya Mkoa wa Kagera.

Kutokana na kushuka kwa uchumi, wamiliki walishindwa kuiendesha timu hiyo na kuchukuliwa na wadau wa soka wa mkoa huo ambao waliamua kuibadili jina na kuiita Kagera Shooting Stars.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 timu hiyo ilichukuliwa rasmi na kampuni ya sukari na kufanikiwa kupanda Ligi Kuu mwaka 2004.

Kagera Sugar ni miongoni mwa timu ambazo hazijawahi kushuka daraja tangu ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, pia ni miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa katika ligi hiyo ikiwa tishio kwa vigogo, Simba na Yanga.

Mtibwa Sugar          

Mtibwa ni miongoni mwa timu zenye historia nchini kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara hiyo ilikuwa mwaka 1999 na mwaka 2000.

Kama ilivyo kwa Kagera Sugar, Mtibwa Sugar pia inamilikiwa na Kampuni ya Sukari ya Mtibwa Estates ya mkoani Morogoro.

Mtibwa ilianzishwa mwaka 1988 na wafanyakazi wa kiwanda hicho kabla ya kupanda Ligi Kuu mwaka 1997.

Ni miongoni mwa timu bora na zenye ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara ikifahamika kwa kuwa na upinzani wa hali ya juu dhidi ya timu vigogo za Simba na Yanga.

Pia Mtibwa Sugar inasifika kwa kuibua vipaji ambavyo vimepata kuwika katika klabu za Simba, Yanga na Taifa Stars.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -