Sunday, November 29, 2020

WAOGELEAJI 172 KUSAKA UBINGWA WA TAIFA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

WAOGELEAJI 172 nchini wanatarajiwa kushindana kesho na kesho kutwa kuwania ubingwa wa Taifa kwenye Bwalo la Shule ya Hopac, jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yatafanyika kukiwa na ujio wa kocha wa klabu na Mkurugenzi wa Shule ya St. Felix, nchini Uingereza, Sue Purchase.

Purchase ambaye ni mkurugenzi wa mchezo wa kuogelea wa shule hiyo, atahudhuria mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), lengo ni kusaka vipaji.

Akizungumza na BINGWA jana Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhani Namkoveka, alisema ujio wa Purchase unatokana na uwezo mkubwa wa waogeleaji wa Tanzania wanaosoma katika shule hiyo.

Namkoveka alisema waogeleaji hao wanaosoma kwa udhamini ni Sonia Tumiotto, Collins Saliboko, Anjani Taylor,  Smriti Gokarn na Aliasgar Karimjee.

Alisema wachezaji hao ambao wanasoma Uingereza tayari wameshawasili nchini kushiriki mashindano ya Taifa.

Namkoveka alisema waogeleaji wameonyesha viwango vya hali ya juu kiasi cha kumfanya Purchase kuamua kufunga safari ya kuja nchini kushuhudia waogeleaji wengine wa Tanzania.

“Ni faraja kubwa sana kupata ujio huu, Purchase ni kocha maarufu na mwenye heshima kubwa nchini Uingereza, amesaidia waogeleaji wengi sana ambao kwa sasa ni nyota katika mchezo huo duniani,” alisema Namkoveka.

Alisema mbali ya kushuhudia mashindano hayo na kusaka vipaji, kocha huyo atakutana na wazazi, makocha, waogeleaji wa Klabu ya Dar Swim Club na kufanya mazungumzo nao.

Mashindano hayo yatashirikisha klabu 15 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zitashindana katika staili za backstroke, freestyle, breaststrokes, Butterfly na Individual Medley (IM).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -