Friday, December 4, 2020

WAPINZANI WA YANGA HOI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAINAB IDDY

WAPINZANI wa Yanga kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho, MC Alger, tayari wametepeta.

Miamba hiyo ya Algeria, MC Alger ambayo siku nyingi walianza kuihofia Yanga, juzi walishindwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani wa Omar Hamadi na kutoka sare ya bao 1 – 1 dhidi ya JS Kabylie.

Pamoja na MC Alger kushindwa kutamba kwenye uwanja wao wa nyumbani, wakielekeza akili zao kwenye mchezo wao na Yanga, mpango wao wa kutaka kuja Tanzania kukichunguza kikosi hicho cha Jangwani, kitakapovaana na Azam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumamosi hii umeshtukiwa.

Chanzo cha ndani cha Yanga, kimedai kwamba mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameshtukia mipango ya Waarabu kutuma mashushushu wao ili kuisoma Yanga.

“Kuna taarifa viongozi wamezinasa kwamba MC Alger watatuma mashushushu wao kuja kuangalia mechi yetu na Azam,” kilisema chanzo hicho kikizungumza na BINGWA.

“Leo (jana) kulikuwa na kikao na kumeundwa kamati kama tatu kuelekea mechi hiyo, moja ya kamati hizo itahusika na masuala ya ulinzi wa kambi ya timu, pamoja na kuthibitisha figisu figisu zozote zitakazotokea.”

Chanzo hicho kiliulizwa namna vibosile wa Yanga walivyogundua mipango ya MC Alger kutuma mashushushu na namna watakavowadhibiti, kilisema: “Ujue hapa Tanzania kuna Ubalozi wa Algeria siku nyingi sana, hivyo tumepenyezapenyeza ‘shilawadu’ wetu tumegundua watatuma mashushushu kwenye mechi yetu dhidi ya Azam.

“Kuhusu kuwadhibiti kuna njia nyingi, lakini lazima watafeli mpango wao, maana uongozi unajua figusi figisu zote,” kiliongeza chanzo hicho.

Yanga, ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiachwa alama mbili na Simba wenye alama 55, watavaana na Azam wakijua kwamba, ushindi ni lazima, ili kuweza kutetea taji lao msimu huu.

Wakati ule mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger utachezwa Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -