Wednesday, November 25, 2020

WAPYA VPL WAONYESHE MAKALI MAPINDUZI CUP

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

KOMBE la Mapinduzi ni moja ya michuano  ambayo imekuwa na mvuto mkubwa hivi sasa. Michuano hii imekuwa moja ya matukio makubwa ya soka hapa Tanzania kutokana na kushirikisha timu mchanganyiko.

Michuano hii imejipenyeza katikati ya ligi mbili za Tanzania Bara na Visiwani na hatimaye sasa imepata nafasi yake, kwani ligi zote mbili zimeamua kuipisha inayochezwa kwa siku takribani 10 au 12.

Kwa sasa michuano hii imekuwa ikifanyika huku Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiwa imefika patamu, japo inahusisha timu tatu za juu katika msimu uliopita, lakini ni wazi kwamba michuano hii inachezwa wakati ambao ligi imekuwa na ushindani mkubwa.

Kwa kawaida timu za Bara zinazoshiriki ni zile zilizoonyesha upinzani mkubwa kwenye ligi, ambapo mwaka huu ni Simba, Yanga na Azam FC lakini michuano iliyopita ilikuwapo na Mtibwa Sugar.

Upinzani wa timu hizi zinapofika kwenye Kombe la Mapinduzi unakuwa wa hali ya juu zaidi ya ule wa kwenye ligi, hii ni kwa sababu kila mmoja anataka kuzima ngebe za mwenzake hasa wale wanaofukuzia ubingwa wa Bara.

Tofauti na upinzani uliopo, michuano hii hufanyika kipindi ambacho timu hizi zimetoka kufanya usajili wa dirisha dogo hivyo kutumia mashindano hayo kuwapima wachezaji wao wapya waliowasajili kwa wakati huo.

Hata katika mahojiano mbalimbali na viongozi wa timu hizi, wamesikika wakisema kuwa watapata muda mzuri wa kuwapima wachezaji wapya waliowasajili.

Wapo wachezaji wengi waliosajiliwa kipindi cha dirisha dogo na timu hizi. Simba wamesajili wachezaji watatu ambao ni  Waghana James Kotei, kipa Daniel Agyei na Pastory Athanas, Yanga imewasajili Justine Zulu na Emmanuel Martin.

Kwa upande wa Azam FC, ni Yakubu Mohammed, Stephan Kingue Mpondo, Enock Atta Agyei, Joseph Mahundi, Yahaya Mohammed na Samuel Afful.

Macho ya mashabiki wa klabu hizi yatakuwa  kwa wachezaji hawa wapya, kuona kuwa fedha zilizotolewa zimeenda kihalali au ndio yale yale kama  ilivyo kwa wengine waliosajiliwa kwa mbwembwe nyingi lakini hakuna kikubwa walichokifanya hadi sasa.

Mashabiki wengi wa soka wanapenda kuona usajili uliofanywa na timu zao unaleta mafanikio, kinyume na hapo lazima wapige kelele.

Katika kikosi cha Simba, usaliji wa awali wa msimu huu imeonekana wachezaji wazawa  kama  Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Mzamiru Yassin, wameonekana kufanya vizuri kuliko wageni na kuwafanya mashabiki wavutiwe na wachezaji hawa.

Kati ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, Andrew Vincent ‘Dante’ pekee ndiye aliyeweza kuonyesha uwezo huku mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha nyingi Obrey Chirwa akiwa bado hajaonyesha kile kilichotarajiwa na wengi.

Kipimo cha wachezaji waliosajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, kimeonekana kwenye mechi 15, kibarua kilichobaki ni kwa wale walioingia kwenye timu hizi Desemba kwani kila mtu ana hamu ya kujua walichonacho.

Kama ilivyokuwa kwa Kichuya na wachezaji wengine wazawa kung’aa, sasa ni zamu ya Pastory Athanas aliyesajiliwa na Simba na Emmanuel Martin wa Yanga. Kuonyesha uwezo kwenye michuano ya Mapinduzi ili waweze kuaminika zaidi kwenye vikosi vyao.

Viwango walivyoonyesha kwenye timu zao walizotoka ndivyo vilivyowafanya wapate nafasi ya kusajiliwa na timu hizi kubwa ambapo Athanas alitokea Stand United na Martin JKU ya Zanzibar.

Katika mechi tatu za ligi za duru ya pili kabla ya kuelekea Zanzibar, wachezaji hawa walipewa nafasi ya kucheza kwenye vikosi vyao vipya na kuonyesha viwango vizuri.

Hiyo haitoshi, matumaini ya mashabiki wengi ni kuendelea kuona wachezaji hawa wanafanya vizuri michuano hiyo ili kujiaminisha kuwa wamesajili vifaa vinavyostahili kuchezea timu zao.

Si hilo tu, pia michuano ya Mapinduzi itaweza kuwaongezea uzoefu wachezaji hawa wa kuendana na mfumo wa makocha wa klabu hizo zenye ushindani wa namba kama alivyothibitisha Athanas.

“Ni mara yangu ya kwanza kushiriki Mapinduzi, itakuwa ni nafasi nzuri ya kuwa pamoja na wachezaji wenzangu kama unavyojua mimi ni mgeni katika timu hii. Naamini nitafanya vizuri endapo nitapata muda mwingi wa kucheza na kuzoeana na wachezaji wenzangu,” alisema Athanas.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -