Wednesday, October 21, 2020

Warembo Miss Tanzania ‘meno nje’ kuwapiga chenga mapedeshee wa Dar

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI,

NENO mapedeshee si geni kwa wadau wa urembo, lakini pia mastaa mbalimbali hapa nchini.

Kwa wasiofahamu, kwa tafsiri isiyo rasmi, pedeshee ni mtu ambaye yupo tayari kutumia fedha zake kufanya atakalo bila kujali madhara yake.

Kwa upande wa warembo, pedeshee amekuwa akitafsiriwa kama mtu aliye tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kumpata mrembo kimapenzi, wakati mwingine wakijitambulisha kama wafadhili au wadhamini.

Baadhi ya warembo wanaoshiriki mashindano hayo na hata mastaa wa kike wa fani nyinginezo, wamejikuta wakinaswa kirahisi na mapedeshee kutokana na tamaa zao za aidha magari, simu, kupangiwa vyumba vya kifahari au hata kununulia vitu kama nguo na vinginevyo.

Mwisho wa siku, warembo hao walijikuta wakichanganywa na mapedeshee hao na kuishia ‘kujuta kuwafahamu’.

Na kwa kiasi kikubwa, kwa kuwa mashindano ya urembo yamekuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam, mapendeshee ilikuwa ni rahisi kwao kutumia mbinu wanazozifahamu kuwanasa.

Lakini kwa mwaka huu baada ya kufunguliwa kwa mashindano hayo yaliyokuwa yamesimamishwa kwa mwaka mmoja, fainali zake hazitafanyika Dar es Salaam, jambo ambalo linaweza kuwa pigo kwa mapedeshee waroho wa mabinti za watu.

Kwa mujibu wa Kamati ya Miss Tanzania, mashindano hayo mwaka huu fainali zake zinafanyika jijini Mwanza mwezi ujao, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa tukio hilo kubwa kabisa la fani ya urembo nchini kufanyika nje ya Dar es Salaam.

Siku moja kabla ya kambi ya warembo hao kuhamishiwa Mwanza kutoka Dar es Salaam, BINGWA lilipata fursa ya kufanya mahojiano na washiriki kujua nini mtazamo wao juu ya hilo.

Ikumbukwe kuwa shindano hilo linajumuisha warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania kama ambavyo imekuwa miaka iliyopita.

Maria Peter (Mwanza)

Mimi naona Kamati ya Miss Tanzania  imeangalia hili jambo kwa upande wa pili, zaidi ya miaka 20 lilikuwa linafanyika Dar es Salaam na kuwafanya watu kulazimika kusafiri kwa ajili ya kushiriki shindano hili wakijua ndio sehemu yenye mwamko wa mambo ya urembo lakini suala la kupelekwa mkoa  mwingine itakuwa ni faraja kwa wakazi wa mikoani kushuhudia na kuelewa kuwa mahali popote Miss Tanzania inaweza kufanyika. Pia nimefurahi shindano kufanyika katika mkoa wangu na ninawaomba wakazi wa Mwanza walipokee kama ilivyo kwa matukio mengine na ninawaahidi nitawakilisha  vizuri.

Grace Christopher (Ilala)

Shindano hili kufanyika Mwanza ni jambo jipya, lazima watu watashangaa kidogo lakini ni nzuri kwa sababu tumebadilisha mazingira  itatufanya tujifunze mambo mengi  na kinachotakiwa ni kuangalia ni kitu gani kizuri kinaweza kupatikana  Mwanza kwa ajili ya kusaidia kukuza  mashindano ya urembo.

Anitha Mlay (Iringa)

Watu inaweza ikawashtua  kusikia shindano hili linafanyika Mwanza tofauti na sehemu  iliyozoeleka, ila nawaomba watu waliojipanga kusafiri kwenda Dar kushuhudia shindano hili wajitokeze. Mimi mwenyewe sijawahi kufika Mwanza, itakuwa ni mara yangu ya kwanza ndio sababu nina hamu sana kufika huko na kinachonivutia ni kwenda kuona Ziwa Victoria ambalo nalisikia tu.

Abella John (Morogoro)

Mabadiliko ni kitu kizuri katika maisha kila mtu tumezoea kuona  shindano hili Dar es Salaam, ila mwaka huu ni Mwanza hata mimi nafurahi kwa  kuwa warembo wanatoka mikoa tofauti si Dar pekee yake hivyo hali hii inaleta ukaribu kwa washiriki wa kanda hiyo na mikoa ya jirani. Naomba warembo wa Mwanza waliowahi kushiriki shindano hili watuandalie vizuri na wajitokeze kushuhudia.

Irene Massawe (Singida)

Hii imekuwa ‘surprise’ kwetu kwa sababu haijawahi kutokea nawaambia wakazi wa Mwanza wategemee kitu kizuri kutoka kwetu kutokana na mabadiliko mengi yalifanyika kama kauli mbiu inavyosema ‘Urembo na Mazingira’ ukizingatia kule kuna vivutio vingi. Mfano mimi sijawahi kufika huko itakuwa ni nafasi kwangu kutembelea jiji hilo.

Hafsa Abdul (Sinza, Kinondoni)

Kama tunavyojua Tanzania ni kubwa ina mikoa mingi hivyo shindano linapofanyika mkoa mmoja inakuwa haipendezi, waandaaji kuamua kufanyia shindano hili Mwanza ni kuithamini mikoa mingine tofauti na kukaa sehemu moja mara kwa mara. Mimi mwenyewe sijawahi kufika Mwanza, natamani kufika  huko niende kwenye ziwa na kula  samaki.

Elgiver Mwasha (Tanga)

Ukiona hadi Miss Tanzania inapelekwa Mwanza ujue imekuja kivingine, ikumbuke miaka yote inafanyika Dar es Salaam na ninaamini litafuata kanuni na sheria zinazohitajika nchini. Wakazi wa Mwanza wasikose kwa sababu ushindani  utakuwa mkubwa kuliko siku zote kila mtu ni mzuri hapa. Warembo tuna furaha kama mimi nilikuwa natamani kufika Mwanza, siku nyingi hivyo hii ni fursa kwangu kutimiza ndoto zangu za kuliona Ziwa Victoria.

Elneema (Morogoro)

Kubadilisha mazingira ni kitu kizuri, kwa mara ya kwanza naenda Mwanza nikiwa  mshiriki wa Miss Tanzania sehemu  niliyokuwa natamani kufika siku zote, nitapata uzoefu wa mkoa ule na kujifunza vitu ambavyo sivifahamu kutoka kwa wakazi wa Mwanza.

Irene (Mtwara)

Mwaka uliopita shindano halikufanyika,  kuhama sehemu ya kufanyia fainali hizo inaonyesha kuna mabadiliko na mwanzo mpya wa shindano la Miss Tanzania. Itasaidia kuwafanya watu wa mikoa mingine.

Irene Msabaha (Ruvuma)

Kama mashindano yanayohusisha Taifa  yanatakiwa kugusa mikoa tofauti si lazima kuwa kila mwaka yafanyike Dar es Salaam peke yake, ni fursa nzuri kwa watu wa Mwanza na uliangalia limetoka kufungiwa kwa hiyo inaonyesha kuna mabadiliko na wajaribu kupeleka na mikoa mingine. Nikiwa kama mshiriki nimelipokea vizuri ukizingatia nimesoma  ni mkoa niliupenda sana.

Ester Mlay (Temeke)

Kwanza kabisa sijawahi kufika Kanda ya Ziwa, ni furaha kwangu kufika kwa mara ya kwanza, pia tunabadilisha kutokana na muda mrefu kufanyika sehemu moja.

Moureen Komanya (Iringa)

Ni mwanzo wa kujua watu wengine wanalichukuliaje shindano la Miss Tanzania, baada ya miaka yote kufanyika Dar es Salaam. Kinachonivutia Mwanza ni Ziwa Victoria na samaki wake.

Sia Pius Lyimo (Kinondoni)

Si kitu kibaya Shindano  la Miss Tanzania kufanyika Mwanza kwa kuwa waandaaji wanataka kujua katika mikoa mingine linachukuliwaje licha ya kwamba sisi washiriki kutoka sehemu nyingine imetuletea changamoto kidogo kwa ndugu zetu wanaopenda kujumuika nasi, lakini naomba wakazi wa Mwanza kutupokea vizuri. Natamani nifike huko hata sasa hivi kwa sababu sijawahi kufika na kinachonivutia ni yale mawe yaliyobebana ziwani.

Leila Kwai (Iringa)

Wakazi wa Mwanza watarajie vitu vizuri ikiwa ni mara ya kwanza ili kujua ni kitu gani huwa kinatokea, ukiangalia asilimia kubwa ya washiriki wanatokea mikoa tofauti tofauti.

Miss Kilimanjaro

Natumaini huu ni mwanzo mzuri na haitaishia Mwanza, itaendelea pengine  na itawasaidia warembo kufika mikoa ambayo hawajahi kufika  kwa mfano mwaka huu wengi tupo hapa hatujawahi kufika Mwanza.

Bahati Mfinanga (Manyara)

Ni changamoto kwa mikoa mingine ivutike kuandaa mashindano haya na hamasa ya kujihusisha mambo ya urembo na kuwa mwamko wa kushiriki Miss Tanzania. Katika maisha yangu sijawahi kufika Mwanza itakuwa ni mara ya kwanza.

Lucy Michael (Geita)

Nafurahi sana Miss Tanzania kufanyika katika Kanda yetu, nahisi shindano hili litakuwa lenye bahati kwa kuwa  limeondoka Dar es Salaam ambako ndio matukio mengi yanafanyika.

Anna Steven (Dodoma)

Najua kwa jambo hili  watu wengi watavutika kutaka kujua kitu gani kinafanyika huko kwa kuwa liliwahi kusitishwa na ndio limerudi upya. Tena nasikia watu wa Mwanza wanapenda sana urembo hata wakiona basi la warembo wanafurahia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -