Sunday, November 29, 2020

WASAFI.COM ISIWE MALI YA DIAMOND PEKEE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

HIVI karibuni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Wasafi Classic, Nasibu Abdul ‘Diamond’, alizindua tovuti mpya ya kuuza nyimbo za wasanii mitandaoni ‘online’.

Diamond aliutaja Wasafi.com kuwa ndio mtandao wake utakaokuwa ukifanya kazi hiyo.

Hii si mara ya kwanza kutokea kwa tovuti kama hizo hapa Bongo, kwani kuna zilizoanza. Tuliwahi kuona nyingine kama Mkito.com, Africasonga na nyinginezo ambazo zote zilikuwa zikiuza nyimbo za wasanii mbalimbali kupitia mitandao.

Hii inadhihirisha ukuaji wa teknolojia habari na mawasiliano (Tehama) ambayo ndio imechagia soko hilo huru la mitandao.

Kwa kiasi kikubwa biashara ya kuuza kazi za wasanii online ndilo lililofungua milango ya soko la muziki na kupunguza utegemezi wa kununua bidhaa kwa kuonana na muuzaji.

Lakini pia, kupitia mitandao kazi za wasanii zimekuwa na uwezo wa kufika mbali zaidi tofauti na miaka ya nyuma au kutegemea maduka.

Hakuna asiyejua malalamiko makubwa ya wasanii ni kitendo cha kazi zao kuuzwa kiholela nchini, huku zikiuzwa kwa bei chee na kuwafanya kutofaidika na kazi zao wenyewe huku wengi wakiishia kuwa masikini.

Kila siku wasanii wamekuwa wakitupa lawama zao kwa Serikali kwa kushindwa kuweka mikakati madhubuti ya kuwakamata wezi wa kazi zao ambao kila siku wamekuwa wakiibua njia mpya.

Bado tatizo hilo halikuwa limepatiwa dawa ya kudumu ya wauzaji haramu wa kazi za wasanii licha ya Serikali kuanzisha mkakati wa kukamata wale wote wanaouza kazi hizo kiholela.

Wadau wengi wamekuwa wakiumiza kichwa juu ya wezi hao wa wasanii, lakini Diamond na timu yake wameamua kuingia kwenye mpambano hayo.

Ni wazi kuwa kwa kuwa na mtandao huo wa Wasafi.com, Diamond atakuwa amepunguza kwa kiasi fulani wizi wa kazi za wasanii.

Atakuwa ameungana na wadau wachache wanaofanya kazi hii ya kuuza kazi za wasanii online.

Kwa hali hii ni wazi jitihada zilizofanywa na Diamond zinapaswa kuungwa mkono kwani zinalenga kurejesha zama zile ambazo soko la sanaa Bongo likiwa juu kabla ya kuharibiwa na wezi hao wa kazi zao.

Hivi sasa, mashabiki wanaweza kupata bidhaa kama muziki, video au ‘program’ kwa kuzipakua haraka mara tu baada ya kuzilipia ambapo malengo makubwa ni kupanua wigo wa kusambaza muziki wa Afrika.

Inajulikana tovuti hizi huwa ni jamvi au meza ambazo wauzaji huweka taarifa zao za kina kama vile bei na aina ya bidhaa, idadi ya kiwango na hata mwaka wa kutengenezwa kazi hizo za sanaa ambazo ndizo zenye mashabiki wengi nchini.

Juhudi za kuufanya muziki wa Bongo Fleva kufika mbali zinapaswa kufanywa kwa pamoja, hivyo mtandao huu wa Wasafi. Com usiwe mali pekee ya Diamond na timu yake.

Wasanii wote wanapaswa kutumia mfumo kama huu wa kuuza kazi zao online ili kupunguza wezi hao wa kazi na kufanya kukuza kwa soko la muziki nchini.

Bila ushirikiano wa pamoja Wasafi.com itakuwa mali ya watu wachache ambapo itakosa tija, japo hailazimishwi kuamua kuuza kazi zao kwa kutumia lebo hiyo wa Wasafi.

Kuna mitandao mingi ambayo inahusika na uuzaji wa kazi hiyo mitandaoni, hivyo si lazima wote wawe kwa Diamond ila wasanii wanapaswa kutumia mfumo huu angalau kupunguza maharamia wa kazi zao.

Bila kutafuta suluhu ya kudumu, kila siku wasanii watakuwa wanalia na wezi hao wa kazi zao ambapo naamini kabisa kuwa sera hii ya online itafanikiwa katika kuwathibiti wezi hao.

Lakini uuzwaji wa kazi hizo online utakwenda sambamba na jitihada za wasanii kuzipenda kazi zenu na kujituma zaidi huku mkitoa kazi zenye ubora zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -