Friday, October 30, 2020

MOURINHO WASALIMIE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

SABABU 3 MOURINHO KUTIMULIWA KABLA YA KRIMAS

MANCHESTER, England

KUCHUKUA mataji manne ya Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya. Kutwaa mara mbili taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Imebaki historia kwake na sasa hana raha pale Old Trafford.

Sare ya bao 1-1 dhidi ya Wolves mwishoni mwa wiki iliyopita, ilichochea tetesi zilizopo kwamba atatimuliwa katika benchi la ufundi la Manchester United.

Ukiwa huu ni msimu wake wa tatu klabuni hapo, bado Mourinho hajatimiza ndoto za mashabiki wa Man United, yaani kurejesha furaha iliyokuwepo enzi za Sir Alex Ferguson ‘Fergie’.

Ni kweli aliipa mataji matatu (Ligi ya Europa, Kombe la Ligi na Ngao ya Jamii) katika msimu wake wa kwanza kazini lakini kitendo cha kutobeba ubingwa wa Ligi Kuu (EPL), kimemweka pabaya.

Tayari wachambuzi wa soka barani Ulaya wanatazamia kumwona mkufunzi huyo wa kimataifa wa Ureno akitimuliwa kabla au siku chache baada ya Sikukuu ya Krismas na hizi ni sababu zao.

Kwanza, kwa miaka mingi Mourinho amekuwa na tabia ya kuropoka na kuwakosoa hadharani wachezaji wake lakini kwa bahati mbaya, huo si utamaduni wa klabu aliyopo.

Kwa kipindi chote cha utawala wa Ferguson, mabosi wa Man United hawakuwahi kumsikia ‘babu’ huyo akimbwatukia mchezaji uwanjani au mbele ya waandishi wa habari, heshima ambayo Mourinho ameonekana kuipoteza katika siku za hivi karibuni.

Aliwahi kufanya hivyo akiwa Chelsea (2015-16) na mwishowe akakorofishana na baadhi ya nyota wake muhimu, akiwamo Diego Costa. Je, nini kilichofuata? Alitimuliwa akiwa amepoteza mechi tisa kati ya 16 za mwanzoni mwa msimu.

Safari hii, Mourinho amefanya hivyo Old Trafford na taarifa zilizopo ni kwamba, hana mahusiano mazuri na kiungo wao wa bei kali, Paul Pogba na mshambuliaji aliyekuwa akitabiriwa kuwa ‘Thierry Henry mpya’ katika soka la Ufaransa, Anthony Martial.

Hata hivyo, mbaya zaidi kwa Mourinho ni kwamba uongozi wa Man United hautakuwa tayari kumwacha awaharibie kwa kuwa nyota hao ni sehemu ya hazina ya Man United katika miaka ya baadaye. 

Pili, matokeo ya Man United hayaridhishi, achilia mbali kiwango kibovu ambacho imekuwa ikikionesha. Ikizingatiwa kuwa bado haijakutana na timu kubwa, mwishoni wa wiki iliyopita ilitweta mbele ya Wolves, licha ya mechi hiyo kuchezwa Old Trafford.

Katika mechi zake sita za mwanzoni mwa msimu huu wa EPL, imeshapoteza mbili, huku ikiambulia pointi 10 kati ya 18 zilizopaswa kukusanywa.

 

Tatu, lipo hili la Zidane Zidane kutokuwa na kibarua tangu alipoachana na Madrid msimu uliopita akiwa ameipa rekodi ya kuwa timu ya kwanza kulibeba mara tatu mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ukiweka kando mafanikio na mbinu zake, ambacho mabosi wa Man United wanaweza kuvutiwa naye ni ukaribu alionao na wachezaji. Tofauti na Mourinho ambaye mara nyingi huwa ‘serious’,  Zidane ni rafiki wa wachezaji.

Zidane amekuwa akitajwa kuwa sehemu ya mipango ya uongozi wa Man United katika kuziba pengo la Mourinho wanayetaka kuachana naye. Inaelezwa kuwa hata kuondoka kwake Madrid kulitokana na mazungumzo yake mazuri na Man United.

Huku akiwa mapumzikoni, kuna taarifa za kuaminika zilizodai kuwa tayari mchezaji huyo wa zamani wa Juventus, ameshawasilisha orodha ya mastaa wake watano anaowataka wasajiliwe pindi tu atakapotua Old Trafford.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -