Friday, September 25, 2020

Wasanii, waandaaji wa filamu jifunzeni kwa ‘Cop’s Enemy’

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA SISCA MACHABA (TUDARCo)

USIKU wa Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Cinema Century, Mlimani City, Dar es Salaam, ulifanyika uzinduzi wa filamu ya Kimataifa ya Cop’s Enemy ambayo imeshirikisha waigizaji kutoka Australia, Ghana na Tanzania.

Katika uzinduzi huo mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dk Kiagho Kilonzo ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa kwenye majukumu ya mkutano wa SADC.

Cop’s Enemy ambayo ni filamu ya Kimataifa iliyobeba simulizi ya kusisimua ya kijana anayepitia wakati mgumu kiuchumi na kulazimika kujiunga na magenge ya uharifu ili aweze kupata fedha za kumtibu mama yake, imeongozwa na Prema Smith kutoka jijini Sydney, Australia.

Ndani ya sinema hiyo iliyoandaliwa katika ubora wa hali ya juu, imechezwa kikamilifu wa waigizaji nyota  kutoka Australia kama vile Clarisse, Gabrielle Bartrett na Jean Yerma, Van Vicker kutoka Ghana na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Stanley Msungu wa Tanzania kwa msaada wa Neema Ndepanya na Zamaradi Mketema.

Huku mwigizaji mwenye asili ya Burundi aliyekulia Tanzania kwa sasa akiishi Australia, John K-ay, akicheza kama mhusika mkuu huku Van Vicker kutoka Ghana akicheza kama kubwa la maadui.

Pia, baada ya uzinduzi huo kufanya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Cop’s Enemy ilizinduliwa pia jijini Bujumbura, Burundi na kufanikiwa kukonga nyoyo za wapenzi wa filamu.

Miongoni mwa mambo ambayo wasanii na waandaaji wa filamu nchini wanapaswa kujifunza kutoka kwenye vilamu hii ni jinsi ya kuandaa mswada unaoweza kuwa na mvuto kwa shabiki.

Si mswada mzuri pekee wa filamu, bali waigizaji wanaoweza kuvaa vyema uhusika na pia vifaa vya kuchukulia maudhui vinapaswa kuwa vya kisasa ili kupata filamu bora itakayokidhi matakwa ya filamu.

Mfano mpaka Cop’s Enemy imekamilika na kuwafikia watazamaji, imegharimu shilingi milioni 200 za Tanzania ndiyo maana imetoka na ubora kiasi cha kuivutia mtandao wa kuonyesha filamu, Netflix, kufanya mazungumzo na John K-ay kwaajili ya kuionyesha sinema hiyo.

Hali kadhalika maandalizi ya uzinduzi. Wasanii wengi wa Bongo Muvi wamekuwa na kawaida ya kufanya mambo kwa mazoea, lakini katika filamu hii tunaona tutofauti mkubwa katika uzinduzi.

Meneja wa John K-ay, Raimon Sanga alisema kuna ziara itafanyika mwezi Octoba katika mikoa zaidi ya 10 kuitambulisha Cop’s Enemy. Mara nyingi tumeona wasanii wa muziki ndiyo wanafanya matamasha ya aina hiyo.

Ila kwa upande wa filamu, hakujawahi kufanyika matamasha yanayowafuata mashabiki wa filamu kwenye mikoa yao. Hapa pana jambo kubwa la kujifunza kwa waaandaaji na wasanii wa filamu kutengeneza mazingira ya kuwafikia mashabiki kupitia matamasha ya filamu.

Cop’s Enemy, ni mwanzo mzuri wa tasnia ya filamu Tanzania na Afrika Mashariki kwenda katika anga la Kimataifa huku watayarishaji na waigizaji wakipata mambo ya kujifunza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -