Monday, November 30, 2020

WASAUZI WAMNYEMELEA KABUNDA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

BAADA ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kiungo mshambuliaji wa Mwadui, Hassan Kabunda, ameanza kunyemelewa na timu za Afrika Kusini.

Kiungo huyo ambaye ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja’, aliibuka mchezaji bora wa mwezi Februari msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na BINGWA, Kabunda alisema hadi sasa klabu saba, ikiwamo moja inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini zinamhitaji.

Kabunda alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi timu hiyo  ya Afrika Kusini inayomhitaji, kwani bado wapo kwenye mazungumzo.

“Nimepokea maombi ya timu saba zinazonihitaji, moja ni ya Afrika Kusini, namshukuru Mungu kwa hilo, lakini bado sijaamua niende wapi kwa sababu hatujafikia makubaliano, nadhani hadi ligi itakapomalizika,” alisema Kabunda.

Hata hivyo, alisema licha ya kutakiwa na timu kubwa za Ligi Kuu hapa nchini, anatoa kipaumbele kwa klabu hiyo ya bondeni na kama watakubaliana atasaini mkataba.

“Ndoto zangu ni kucheza nje ya nchi niwe kama Mbwana Samatta, anayecheza Genk ya Ubelgiji, lakini sitakurupuka kwenda timu yoyote bila kupata mkataba utakaoniwezesha kufanya kazi yangu kwa ufasaha,”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -